Viongozi waliotibiwa hospitali za nje ya nchi

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Wakati sakata la mgomo wa madaktari likipamba moto tunaweza kuwa na orodha ya viongozi wa Kitanzania waliotibiwa kwenye hospitali za nje ya nchi kwa gharama za walipa kodi? Pia tunaweza kuweka aina ya magonjwa na matibabu waliyoyapata huko nje na kama hayo magonjwa yangeweza kutibiwa kwenye hospitali za Tanzania. Kwa madhumuni ya mjadala huu, hata mafua ni ugonjwa na check up ni matibabu.
 
wenzenu kuna hospitali zina mikataba ya kuwatibu huko magharibi ya ulaya ,india na south africa licha ya kuwa na wauguzi binafsi na jambo la maana tungejiuliza Kagame anatibiwa wapi,Zuma je?Castro je?hapa pana laana ama upofu tu jamani?
 
Lundo la wabunge na mawaziri limetimkia nje hapo juzi tu na kutumia mabilioni tena yanatolewa fasta tu alafu serikali haina pesa za kulipa waalimu mikopo madenti na madokta
 
Lundo la wabunge na mawaziri limetimkia nje hapo juzi tu na kutumia mabilioni tena yanatolewa fasta tu alafu serikali haina pesa za kulipa waalimu mikopo madenti na madokta

Ingekuwa bora kama ungetutajia na majina.
 
Jk,Salma,Msuya,Mwandosya,Sitta,Membe only check up,Zitto,Sumari marehemu,mbunge wa kalenga marehemu,Kaboyonga,Getrud Mongera,Anna Makinda,Anna Abdallah,Msekwa list ndefu jamani
 
Jk,Salma,Msuya,Mwandosya,Sitta,Membe only check up,Zitto,Sumari marehemu,mbunge wa kalenga marehemu,Kaboyonga,Getrud Mongera,Anna Makinda,Anna Abdallah,Msekwa list ndefu jamani

Dr kitime alimpeleka mke kutibiwa mafua
 
Zitto Kabwe- India, matibabu kipanda uso
John Malecela - Uingereza, matibabu Oparesheni ya Moyo
Harison Mwakyembe - India, Pollium poison
Samuel Sita - alikwenda India kumtembelea Mwakyembe kwa kutumia kodi za Wananchi na kujiongezea maposho.
Mwandyosa - India.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Senior member kwa hili NAKUUNGA MIKONO YOTE MIWILI, hili la Tabaka fulani la watu fulani kwenda kutibiwa India au kwinginge kwa kodi ya Wananchi????
Hivi kuna faida gani kutrain Madaktari na kuita Muhimbili University kama madaktari hawatumiwi??? kama ni hoja ya vifaa hivi mapesa yooote haya yanayotumika kwa gharama za matibabu, malazi, makulaji na wasindikizaji, kununua magari ya kifahari kwa wabunge mawaziri na mengine mengine, mapesa haya yameshindwa kuingiza vifaa japo kimoja baada ya kingine? maana tokea watu walivyoanza kwenda kutibiwa London, na sasa India kweli ingeshindikana? mimi si mpiga kura, lakina naamini kweli hawa wakubwa hawepewi kura bali wanapewa KULA, mimi si mjuzi wa mambo lakini fatilieni nchi Tajiri kama ville, USA,UK, UFARANSA n.k kama wabunge au mawaziri wao wanapata migari ya fahari kama hapa kwetu?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mbona wote tu mkuu, labda ungesema other way round kiongozi gani hajaenda india list ingekuwa nzuri..ila kwasasa ni wote mwenye cheo cha u-kurugenzi..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom