Viongozi wakuu wa nchi hii wameshindwa kushawishi wananchi

thereitis

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
297
41
Kuna tofauti kuu kati ya uongozi(Leadership) na utawala(administrator). Sifa kuu ya kiongozi ni uwezo wa kushawishi watu anaowaongozi kutenda jambo ambalo yeye kama kiongozi anaone lina manufaa kwa anaowaongozi. Mtawala hana sifa hiyo; majukumu yake makuu ni kuhakikisha mambo yanafanyika kwa kutumia mamlaka aliyonayo mfano kutumia askari kudhibiti wale wanaoenda kinyime na mipango ya utawala.

Siku za karibuni tumeshuhudia maandamano au vurugu za polisi dhidi ya raia wasio na silaha - Arusha, Mbeya, Mwanza na Dar ni baadhi ya maeneo ambapo vurugu zimetokea. Vurugu hizi zinadhihirisha nini? Je Viongozi wetu wamekosa ile sifa kuu ya kushawishi wananchi?
 
mbona hakuna maandamano kilimanjaro nyumbani kwa mwenyekiti wetu, au haungwi mkono nyumbani kwao au ni mbinu ya kulinda miundombinu yao isibomolewe na waandamanaji?
 
Ndugu yangu,
Hilo swali linasumbua sana kuhusu aina ya viongozi tulionao. Ni hakika tuna WATAWALA NA SIYO VIONGOZI, kwani tulionao hawana uwezi wa kutuonyesha njia sahii ya kupitia na badala yake wamekuwa wakitumia DOLA ili wafanikishe malengo yao. NI HAKIKA KWASASA TZ HATUNA VIONGOZI HASA KTK UONGOZI WA NCHI na badala yake tuna WATAWALA, ambao ni MADIKTETA wanaufikiria tu matumizi ya dola mara zote.
 
zipo haki mbili ya kuandamana na ya kuzuia kuandamana inategemea ni haki ipi inashinda nyingine rejea somo la Human rights and government right
 
Back
Top Bottom