MZK
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 223
- 303
VIONGOZI WAKUU WA CHADEMA WAMALIZA MGOGORO RUVUMA
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, ujio wa wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA katika mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na makamo mwenyekiti wa chama Prof. Abdallah Safari, waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa na naibu katibu mkuu visiwani Salum Mwalim wamefanikiwa kumaliza mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu mkoani humo na hatimaye kamati tendaji ya chama hicho wilaya ya Songea mjini kukubali kuachia ngazi na kupisha wanachama wengine kushika nafasi hiyo.
Baada ya hatua hiyo ukumbi ulitawaliwa na nderemo na vifijo kuashiria mwanzo mpya wa uongozi katika chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.
Baadhi ya wanachama wamesikika wakitoa maoni yao na kupongeza viongozi hao wakuu wa chama kwa busara yao iliyotumika kumaliza mgogoro huo.
NB: Kwenye picha ni Viongozi wa wilaya ya Songea mjini wa CHADEMA waliokubali kujiuzulu, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati kuu walioko mkoani Ruvuma katika ziara maalum ya kukijenga chama