Viongozi wafuatao kuchunguzwa na sekretariet ya maadili ya umma, mali zao mashakani

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Taarifa ya habari tbc1, yadaiwa wako 80 ni mawaziri, makatibu, wabunge nk. Yadaiwa walidanganya mali zao. Majina kumi ya mwanzo yametajwa kwa mtiririko huu;
1. Anna Tibaijuka
2. Omary Nundu
3. Mathayo Davd Mathayo
4. Vuai Nahodha
5. Lazaro Nyarandu
6. Jaji Werema
7. Katibu mkuu kiongozi (huyu mpya)
8. Mr. Jundu
9.
10.

Samahani hao wawili sikuwakariri.
 
Halafu watawafanya nini watavua ubunge ........... wapi haya mambo yanwezekana ninacho kiona hapa posho na night za wajumbe baaaaaaaaaaaaasiiii
 
Wamethibitisha kama wamedanganya? Sheria iko straight kuwa kama ikithibitishwa wamedanganya mamlaka zilizowateua zinalazimishwa na sheria KUWAFUKUZA KAZI
 
Hii piramid inaanzia chini then katikati then chini yaaani juu inaogopa kabisa kwenda sijui kwa nn?
 
hii tume ni sawa na takukuru hawana meno zaidi ya kubweka
hakuna kutakachoendelea zaidi ya propaganda kedekede katika vyombo vya habari
huku wananchi wakidhani kuna uwazi.
 
Mali zao kutangazwa hadharani Desemba, sheria kufumuliwa
Wengi serikalini wajipanga kukwamisha utekelezaji
Kikwete aiga mfumo huo kwa Rais Obama

KILIO cha muda mrefu cha wadau mbalimbali wa utawala bora nchini, wakiwamo wanaharakati waliokuwa wakipinga usiri katika taarifa za mali za viongozi wa umma kinaweza kupata ufumbuzi. Raia Mwema imepata waraka maalumu unaotaka kuwapo kwa mabadiliko ya Sheria ya Maadili ya Viongozi, ambamo mali zao zitawekwa hadharani.
Waraka huo unaozungumzia utekelezaji wa mpango wa ubia katika kupanua uwazi serikalini (Tanzania Open Government Partnership), unaanza kutekelezwa mwaka huu hadi mwakani, ukifanana na uamuzi uliokwishafanywa na Rais wa Marekani, Barack Obama, pamoja na nchi ya Brazil.
Kwa upande wa Marekani, mpango huo unahusisha Ikulu ya Marekani (White House) kuweka wazi katika tovuti hadi mishahara ya watumishi wa Ikulu hiyo na taarifa nyingine za mali za watumishi wake, taarifa zao za maadili na hata rekodi za wageni wanaoitembelea Ikulu hiyo.
Lakini kwa upande wa mpango wa Tanzania ambao unatokana na mpango huo wa Marekani, ambayo itasaidia katika maandalizi ya mpango wa hapa nchini katika eneo la uwajibikaji na uadilifu (accountability and integrity) , Tanzania itazingatia maeneo sita.
Suala mojawapo linahusu kufanya mabadiliko ya sheria inayohusu utangazaji wa mali za viongozi wa umma, ili taarifa husika ziwe wazi hata kwenye tovuti ambako mtu yeyote anaweza kuzisoma.
Kipengele hicho kinaeleza: “Kuandaa marekebisho ya sheria na kanuni ili kuimarisha mchakato wa kutangaza mali za viongozi wa umma, ziweze kufikiwa na wananchi wengi kupitia mtandao hadi itakapofika Desemba mwaka huu.”
Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa mapendekezo hayo hususan kipengele hicho cha kuweka hadharani taarifa za umiliki wa mali za viongozi, kimeanza kupata upinzani ndani ya serikali.
Vyanzo vyetu vya habari serikalini vinaeleza kuwa wapo baadhi ya viongozi wanaopinga mpango huo kwa maelezo kuwa utaweza kuibua mtafaruku kati ya viongozi wa umma na wananchi, lakini wale wanaouunga mkono wanasisitiza kuwa hakuna sababu ya hofu kwa mtu mwenye mali alizopata kihalali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Mathias Chikawe, amekaririwa akishangazwa na wenye kuhofia hatua hiyo.
Mbali na eneo hilo, katika suala hilo la uwajibikaji na uadilifu, eneo jingine litakaloboreshwa katika mpango huo wenye ubia wa kimaitaifa unaohusisha Marekani na nchi ya Brazili ni kuboresha tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili iweze kufikiwa na kila mwananchi anayetaka kusoma taarifa mbalimbali za ukaguzi wa hesabu. Kipengele hicho pia kimepangwa kutekelezwa ndani ya mwaka huu, kama ilivyo kwa kipengele cha kuweka hadharani mali za viongozi.
Eneo jingine maalumu la mpango huo linahusu uwazi (transparency) ambamo sasa hadi kufikia Julai mwaka huu, katika bajeti ijayo, taarifa zote za misamaha ya kodi zitakuwa zikiwekwa hadharani kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha na taarifa hizo kuongezewa upya (update) angalau kila baada ya miezi mitatu.
Faida za mpango huo
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kati ya athari za mpango huo hasa wa kufichua mali za viongozi wa umma kwa wananchi ni pamoja na wananchi kuweza kufuatilia ukweli wa taarifa za mali za viongozi hao.
Hali hiyo inatajwa kuweza kuondoa udanganyifu unaoaminika umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu sasa na baadhi ya viongozi wa umma. Imeelezwa kuwa baadhi yao wamekuwa hawatangazi mali zao zote, na kwamba udhaifu huo umekuwa ukiwawezesha kuendelea kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi za umma bila hofu.
Wapo ambao wanaotumia mfano wa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye wakati anaingia madarakani, alikuwa na ujasiri wa kutaja mali anazomiliki ikitarajiwa kuwa angefanya hivyo pia wakati anang’atuka.
Hata hivyo, kinyume cha matarajio ya wengi, Mkapa aliamua kufanya taarifa zake za mali siri alipong’atuka, hatua ambayo kama Sheria ya sasa ya Maadili ya Viongozi wa Umma itafanyiwa marekebisho na taarifa za mali za viongozi kuwekwa kwenye tovuti kila mwaka, fursa ya namna hiyo aliyoitumia Mkapa haitakuwapo tena.
Hali ya utawala bora nchini
Taarifa mbalimbali, yakiwamo maoni ya wananchi wengi, zinabainisha kuwapo kwa hali ya mwenendo usioridhisha katika eneo la uwajibikaji, utawala bora na uwazi.
Wakati hali hiyo ya kutoridhishwa ikiwa bayana miongoni mwa wananchi, zipo hatua ambazo zimekwisha kuchuliwa na serikali, ingawa matokeo ya hatua hizo hayajawa na ufanisi wa kujivunia.
Hatua hizo pia zinahusisha uamuzi wa Bunge la tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, kufikia uamuzi wa kuanzisha Kamati za Kudumu za Bunge, kamati maalumu zinazoongozwa na wabunge wa Kambi ya Upinzani, zikitajwa kuwa ni kamati za uangalizi (watchdog committees).
Kamati hizo ambazo zinatajwa katika mpango-mkakati huo kama hatua za awali zilizopata kutekelezwa na nchi ni pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, ambayo kwa sasa inaongozwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John cheyo (kutoka UDP), Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, inayoongozwa na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.
Ingawa kwa sasa uamuzi huo wa kuanzisha kamati hizo maalumu za Bunge umewekwa kama masuala ya msingi yaliyokwisha kufanyika, lakini itakumbukwa kuwa Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, alipata upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi, akitajwa kuongoza Bunge katika mtindo wa kuhujumu Serikali.
Sitta kwa wakati huo alikuwa akiweka bayana kwamba anataka Bunge liwe na meno katika kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba, wa kuisimamia na kuishauri Serikali, lakini alipingwa na baadhi ya wabunge wenzake, hadharani na katika vikao vya faradha, kwamba “meno” aliyokuwa akiyatengeneza katika Bunge yalikuwa yanaitafuna Serikali. Ni Sitta huyo huyo aliyetishiwa kuvuliwa uanachama wake ili hatimaye apoteze uspika, lakini zikatumika mbinu nyingine za kumng’oa kutoka kiti hicho.
Ushindi kwa wanaharakati
Iwapo mkakati huu utafanikiwa kwa kufanyiwa marekebisho kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, namba 13, ya mwaka 1995, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa ni ushindi kwa baadhi ya wanaharakati nchini, ambao wakati fulani walifungua kesi kupinga usiri uliomo ndani ya sheria hiyo.
Wanaharakati hao kutoka baadhi ya asasi za kiraia walifungua kesi, huku wakiwa na kumbukumbu za kuwahi kufutwa kwa sheria ya “takrima”, iliyokuwa ikiruhusu wagombea wa nafasi za uongozi wa dola, nyakati za Uchaguzi Mkuu, hasa ubunge kutoa “takrima” ambayo kimsingi ni rushwa kwa baadhi ya wapiga kura.

Chanzo: RaiaMwema
 
Hakuna kitu kama hicho. Huyo mama yangu kama anataka kibarua chake kiiche kabla ya december atangaze bila chenga aone
 
Imefikia kipindi watanzania hatuaminiani hata kidogo, maana hata pale taasisi mbalimbali za serikali kama majeshi,PCCB,sekeretaeliti mbalimbali, tume n.k zinapotaka kufanya kazi yake watu wanavibeza na kudai eti vimeshinikizwa, propaganda,porojo, kwamba vinatafuta posho ama vinginenevyo. Kama tumefikia hatua ya kutoaminiana kiasi hicho, je nani sasa aje kutumikia umma wa nchi ambaye anaaminika na hatabezwa?Mm naona watu wanaobeza kila kitu nao ni walafi wa madaraka. Tuache watu wafanye kazi yao kwa uhuru wakienda kombo tuwahoji kwa mujibu wa taratibu na sio kuanza kuwapiga vijembe mwanzo wa kazi.

[h=2]katika hili la sekretariet ya maadili ya umma kwa unyeti wake tuache ushabiki wa kisiasa.[/h]
 
Taarifa ya habari tbc1, yadaiwa wako 80 ni mawaziri, makatibu, wabunge nk. Yadaiwa walidanganya mali zao. Majina kumi ya mwanzo yametajwa kwa mtiririko huu;
1. Anna Tibaijuka
2. Omary Nundu
3. Mathayo Davd Mathayo
4. Vuai Nahodha
5. Lazaro Nyarandu
6. Jaji Werema
7. Katibu mkuu kiongozi (huyu mpya)
8. Mr. Jundu
9.
10.

Samahani hao wawili sikuwakariri.

Mbona Lowasa haguswi?au hiyo kamati nayo ni yake?
 
Taarifa ya habari tbc1, yadaiwa wako 80 ni mawaziri, makatibu, wabunge nk. Yadaiwa walidanganya mali zao. Majina kumi ya mwanzo yametajwa kwa mtiririko huu;
1. Anna Tibaijuka
2. Omary Nundu
3. Mathayo Davd Mathayo
4. Vuai Nahodha
5. Lazaro Nyarandu
6. Jaji Werema
7. Katibu mkuu kiongozi (huyu mpya)
8. Mr. Jundu
9.
10.

Samahani hao wawili sikuwakariri.
tume kwa fedha na mali zilizpopo nje ya nchi kama Malta,USA,CANADA,ENGLAND,AUSTRALIA,SWIS nk wanauwezo wa kuzihakiki au tunadanganyana mana sidhani kuwa mapapa wanaweza kuweka mali zao hapa nchini na kama hawawezi wanahakiki nini sasa

Hivi hii
 
Imefikia kipindi watanzania hatuaminiani hata kidogo, maana hata pale taasisi mbalimbali za serikali kama majeshi,PCCB,sekeretaeliti mbalimbali, tume n.k zinapotaka kufanya kazi yake watu wanavibeza na kudai eti vimeshinikizwa, propaganda,porojo, kwamba vinatafuta posho ama vinginenevyo. Kama tumefikia hatua ya kutoaminiana kiasi hicho, je nani sasa aje kutumikia umma wa nchi ambaye anaaminika na hatabezwa?Mm naona watu wanaobeza kila kitu nao ni walafi wa madaraka. Tuache watu wafanye kazi yao kwa uhuru wakienda kombo tuwahoji kwa mujibu wa taratibu na sio kuanza kuwapiga vijembe mwanzo wa kazi.

katika hili la sekretariet ya maadili ya umma kwa unyeti wake tuache ushabiki wa kisiasa.
You are a GREAT THINKER wa ukweli.WATANZANI KILA KITU CHAO WANA BEZA, SIJUI LINI TUTAJIAMINI NA KUFANYA MAMBO YETU WENYEWE TOKA MWANZO HADI MWISHO HALAFU TUKALIFANYIA TATHIMINI KUONA TUMEFANIKIWA AU LA.Amkeni watanzania,tuweke pembeni frustration zetu tulijenge taifa.
 
hivi unaishi nchi gani ????

lini ulisikia hii sekretarieti ina meno , imeanza lini kazi , viongozi wa umma na hasa wabunge unajua dead line ya kuwasilisha taarifa za mali zao ni lini ?

Katika vyombo vya serikali visivyo fanya kazi yake cha kwanza ni hiki cha maadili ya umma wapo kama hawapo. hapo wanatafuta posho tu na night hakuna jingine Sasa kama huuamini fuatilia hiyo list nani atakaye chukuliwa hatua

Mfano; Waliambiwa shetani kapoteza fomu za mbunge mmoja wakaamini
 
You are a GREAT THINKER wa ukweli.WATANZANI KILA KITU CHAO WANA BEZA, SIJUI LINI TUTAJIAMINI NA KUFANYA MAMBO YETU WENYEWE TOKA MWANZO HADI MWISHO HALAFU TUKALIFANYIA TATHIMINI KUONA TUMEFANIKIWA AU LA.Amkeni watanzania,tuweke pembeni frustration zetu tulijenge taifa.
Tupe basi japo mfano mmoja wa hii sekretarieti ilicho fanya na maamuzi yenye tija kwa taifa zaidi zaidi nimeona mabango ya aina mavazi yasipaswa kuvaliwa kwa watumishi wa umma
 
Back
Top Bottom