Viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiongozwa na Mhe. Mbowe ziarani mikoa yote Tanzania

Dili na usani wa kiwango cha juu. Siku hizi wanasema " katika ubora wake".
 
ACT INAZID SAMBARATIKA HUKU CHADEMA INAZID IMARIKA

SAFI SAAANA
ACT kimeanzishwa kwa pesa za NSSF kwa ushauri wa kitengo, madhara yake fao la kujitoa limeondolewa. Mfadhili sasa hivi kabanwa lazima kife.
 
Vyama vya siasa visivyohimiza watu kutulia na kuwasaidia wafanye kazi badala yake wanahimiza matembezi tu. ...Tunao wabunge wengi wa upinzani wasio na tofauti na wale wa kijani na ifikapo 2020 kwakweli hatutokuwa na msamalia, kipimo si mlitembea wapi na wapi ama wapi mpaka wapi ..tutakupima kwa mafanikio ya ahadi zako zilizotoka kinywani mwako.

Waache waendelee kuzurura tu.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Viongozi Waandamizi wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe leo wameendelea na ziara ya kikazi inayohusisha vikao vya ndani katika majimbo ya Kanda ya Kati (Dodoma, Morogoro na Singida), ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama kwa kanda hiyo utakaofanyika Novemba 23, mwaka huu.

Mwenyekiti Mbowe anaongoza timu inayokwenda katika majimbo ya Mkoa wa Morogoro, akiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu Prof. Mwesiga Baregu, ambapo jana walikuwa majimbo ya Mlimba na Kilombero na leo wamefika majimbo ya Mikumi na Kilosa.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Tanganyika), Prof. Abdalla Jumbe Safari anaongoza timu iliyoko mkoani Dodoma, akiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim, jana walifika majimbo ya Kongwa na Mpwapwa na leo wamefanya ziara katika majimbo ya Chemba na Kondoa Kaskazini na Kondoa Kusini.

Timu ya tatu inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika akiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambapo jana walikuwa katika majimbo ya Singida Mashariki, Singida Magharibi, Singida Mjini na Singida Kaskazini na leo wamefika majimbo ya Manyoni Mashariki na Manyoni Magharibi (Singida) na Bahi (Dodoma).

Katika ziara hiyo, Viongozi Wakuu pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu wameambatana na wabunge ambao wamegawanywa katika timu mbalimbali na kupangiwa majukumu kwenye kanda 8 za upande wa Tanganyika, kati ya Kanda 10 za chama nchi nzima.

Siku ya Jumanne, Novemba 22, timu zote zitaendelea na ziara katika majimbo mengine katika mikoa hiyo mitatu kadri ya ratiba ya ziara nzima ilivyopangwa.

Novemba 23, mwaka huu Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Kanda ya Kati watakutana kwa ajili ya kikao cha uchaguzi, kuchagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mweka Hazina wa Kanda.

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Changamka Makamanda hu si wakati wa kulala.
Aluta cotinua.
 
Tumeona operesheni SANGARA, M4C, UKUTA nk lakini hazina mafanikio, hiyo ni kiki ya kutafuna ruzuku tu.
una uhakika hazina manufaa.... leo hii mkoa gani tanzania bara ambako chadema haijafika?? na je kuongeza wabunge na madiwani nako sio manufaa?? kura za urais kuongezeka nako sio manufaa?? muwe mnaangalia takwimu ndio mto conclusions maana chama chenu cha ccm kura zenu zinapungua kila mwaka compare jk 2005-2010- na Jpm 2015 ndo utapata majibu kama zina manufaa ama la
 
Tatizo lenu ni kabadili gia angani, litawasumbua Sana. Ili uwe makini lazima uwe na mipango muda mrefu. Lakini kilichofanyika 2015 ni sawa kurudi hatua 10000 nyuma. Kama tungebaki na msimamo wetu na kauli mbiu yetu UFISADI nadhani ushindi ungekuwa mkubwa kuliko huu, mfano ni kwenye uchaguzi wa serikali Zach mitaa. Kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuufurahia ujinga ule ni afadhali ubaki bila kuwa na chama kuliko mtu mmoja (m/kiti) Kwa maslai binafsi kubadilisha mfumo ndani ya chama. Nawatakia safari njema nyie nyumbu wa changadema kuelekea 2016.
 
Back
Top Bottom