mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,704
Hakika viongozi wetu wa vilabu vya soka Tanzania ni wanasiasa kabisa.Kwa watanzania walio wengi Klabu ya Pyramid ya Misri ni klabu isiyofahamika lakini mara baada ya jana CAF kutoa ratiba ya michuano na Klabu ya Yanga kupangiwa kucheza na Timu ya Pyramid ya Misri baadhi ya viongozi wa Yanga wameibeza Klabu hiyo na kujinasifu kuifunga timu hiyo.
Watanzania mtakumbuka viongozi hao hao wa Yanga walituhakikishia kupindua Meza nchini Zambia dhidi ya Zesco matokeo yake ni kubamizwa goli 2-1 na kutupwa nje.
Nashauri uongozi wa Klabu ya Yanga wawe makini na kauli zao mpira wa karne hii ni tofauti sana sio ule wa ushirikina kama walivyozoea, Klabu za Misri ni klabu zenye uchumi mzuri hivyo zinaajiri na kusajiri Makocha na wachezaji wazuri tofauti na Klabu za Tanzania.