Viongozi wa Wilaya Temeke mjitathimini hi barabara kutoka Mbande kuelekea Chanika inakutieni doa

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,699
3,088
Jana nimepita hi barabara kwa kweli nimesikitika sana na kuwaonea huruma watumiaji wa hii barabara na mwisho nikauchukia uongozi wote wa wilaya ya temeke

Barabara muhimu kama hii inayotumiwa na watu wengi inakuwa na mihandaki kiasi kwamba magari ya abiria na ya watu binafsi yanazimika katika hayo mahandaki na kuongeza shida kwa watumiaji wa hii barabara

Hu ni mwaka wa 10 sasa hii barabara kila mwaka inajazwa kifusi na kusawazishwa vizuri inabaki kuwekwa rami tu lakini rami haiwekwi na ikija mvua inaondoa kifusi chote alafu wanaanza tena kujaza kifusi na kuijenga kila mwaka wanafanya hivi Mara mbili au tatu sitakosea nikisema hii barabara kuna watu wameguza kuwa mradi wa kupiga pesa

Hi barabara inapande mbili Ilala na Temeke lakini cha kushangaza kipande cha Ilala chote kimejengwa kwa rami ila kipande cha Temeke ndio kila mwaka kinajengwa lakini hakikamiliki ikija mvua inaharibu mvua zikiisha wanaanza tena kujaza kifusi

Inawezekana mda huu tayari cheki ya kujaza kifusi inaandaliwa maana kwa hali jinsi ilivyo ni lazima kifusi kijazwe haraka

Nawatakia kazi njema viongozi wote wa wilaya ya Temeke
 
Hii ni kweli kabisa,,, nimepita hapo mara nyingi….ni ufisadi mkubwa umetawala
 
Hii barabara ni shida sana, halafu Watu wa huko wapo kimya tu kuanzia viongozi mpaka wakazi wenyewe.

Zamani magari makubwa kama eicher yalikua yanatoka Gerezani mpaka kisewe sasa hivi mengi yamebadili route yanaenda Kisemvule kwa sababu ya Barbara mbovu.

Hiyo barabara ni kubwa sana, Watu wa kisewe, kitonga, msongola wanapata tabu sana.

Uongozi wa wilaya ya temeke tengenezi hiyo barabara, mbona wenzenu upande wa ilala wameweka lami.
 
Back
Top Bottom