Viongozi wa wilaya CHADEMA Singida wahamia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa wilaya CHADEMA Singida wahamia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albano, Aug 11, 2011.

 1. A

  Albano Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti CHADEMA wa Wilaya ya Iramba ndugu Emmanuel Edgar Ntundu na Mwenyekiti wa Chadema singida Mjini ndugu Nakamia John wameahamia CCM. wengine ni Ela Samson Dyelu mwenyekiti wa baraza la wanawake, ndugu Henri Stephene Kingu katibu mwenezi wa wilaya ya Iramba na mwenyekiti wa Tawi la Ruruma. Habari zaidi mtazipata baadae!
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hao wengine waatakaochaguliwa itabidi wapelekwe Arusha ,Mbeya,au Mwanza , wakapate semina elekezi ya kukataa kufinyangwa fikra mkoa mzima wa Singida wa mwisho kwa pato la taifa lakini watu wake ufahamu uko chini kabisa wanatia aibu,inabidi Bavicha waende huko mwezi mzima somo watalielewa tuu
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  Hao ni ccm walorudi ccm
   
 4. S

  Salimia JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Go Mwigulu,, go!
   
 5. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Njaa ndo tatizo, hovyo tuu! Waende!
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wanarudi walikotoka.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani wameogopa kibano kama walichopata Madiwani wasaliti huko Arusha. Usaliti ni dhambi mbaya sana.
   
 8. S

  Salimia JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wote walikuwa huko huko mkuu including Dr. wa ukweli
   
 9. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huo ufahamu kuwa chini unapimwaje?
  Akina Shitambala nao ni wenyeji wa Mkoa wa Singida?
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Madiwani wa Arusha waliofukuzwa uanachana Chadema
  walipokuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chadema Dodoma


  Hawa ni timu moja, kwani inajidhihirisha kuna walichofuata baada ya kukosa wanarudi walikotoka, na vema wamehama mapema ili chama kianze kujengwa upya na kuwa makini na wanaowekwa madarakani.​
   
 11. v

  vngenge JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Du ama kweli siasa kazi kwelikweli! Huku kunajengwa kungine kunabomoka, tatizo wengi wanakosa dhamira ya dhati hivyo mafunzo ya uongozi na uanachama ni muhimu hasa maeneo ambapo chama kinaanza kuchipua. Hii itajenga msingi hata ikifika 2014 uchaguzi serikali za mitaa wanachama watakuwa wamekomaa kiitikadi hivyo kuwa ngumu kurubuniwa na wataweza kusimamia ipasavyo maslahi ya chama, kwa kuimarisha mtandao wa chama na mafunzo naona ndo njia pekee ya mafanikio-ni mtazamo tu!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Someni na kuelewa mbinu chafu za CCM kutumia pesa za walipa kodi kwa ajili ya kununua wanasiasa.

  Wakati Chadema wametangaza kuwa na mkutano na wananchi Arusha, CCM imetumia kila walichonacho kuwanunua viongozi wa Chadema na kuhitimisha uhamaji wao siku hiyo hiyo wakati Chadema wanafanya mkutano Arusha.

  Hii hata kwa akili ya mtoto mdogo ambaye bado ubongo unaendelea to develop anajua mchezo uliofanyika. Lakini hatima yake ni nzuri kwani viongozi wenye tabia ya upopo bora waende ili tubaki na wapiganaji mahiri tu.

  Nakumbuka Biblia agano la kale jamaa alipotaka kupata wapiganaji wazuri aliamua kuwapa mtihani wa kwenda mtoni kunywa maji. Wale walikunywa kwa kuinama kichwa majini na kunywa maji kama ng'ombe waliteuliwa kwenda vitani, na wale ambao walikuwa wanachota maji kwa mikono na kunywa waliachwa kwamba hawafai katika mapigano.

  Kwa wapenda mageuzi ya kweli bora wabovu waende ili iundwe timu yenye uchungu wa nchi hii na kuweka kando maslani ya kuchumia tumboni.
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  mi nilivyosikia Singida nikastuka kwa kujua ni muheshimiwa Mnadhimu Tundu Lissu...
  Dah ok kama ni hao awa vuzi litengane na nywele...
  Watuachie nywele zetu tu
   
 14. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni habari ya kushtua, lakini, in a long term, inayoashiria afya kwa Chadema. Ni bora magugu yajiondoe na kubaki na watu makini na wenye dhamira ya kweli.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pesa nyingi nchi hii zinaporwa kwa ushirikiano mkubwa sana na mtandao wa viongozi wa serikali, vyombo vya usalama, watu binafsi kwa ushirikiano mkubwa sana na kwa usiri mkubwa. Mataifa ya nje yanajua kinachoendelea kuliko watanzania wenyewe. Kwa mataifa ya nje mtandao wa fedha kwenye mabenk ni wa wazi na wanahoji uhalali wa pesa hizo kama inatia shaka la mapato ya mtu kuwiana na hali ya pesa alinanazo.

  Vyombo vya usalama wa nchi ya Tanzania kama usalama wa taifa wasingekuwa ndani ya mtandao huo ingekuwa rahisi kunasa watu wanaojilimbikizia pesa nje. Na kuna uwezekano mkubwa kundi la watu au chama cha siasa kutunza pesa nyingi zilizochotwa serikalini kwa kutumia jina la mtu fulani.

  Kumbukeni kashfa zinazofumuliwa kama mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi Tanzania kukutwa na pesa kiasi kile kwa mtu binafsi si rahisi kwani hata matajiri wakubwa duniani inawachukua miaka na katu wengi hawafikii na kiasi hicho kwa matajiri. Na matajiri utajiri wao hujumuisha mali walizo nazo pamoja na property zao, kwa si rahisi mtu kutunza pesa taslim kiasi hicho kwani ni jambo la kushangaza.

  Hili ni jambo la kujiuliza pesa nyingi hivyo kuhifadhiwa na mtu binafsi na inapoibuliwa hakuna jitihada za serikali kushuhulikia. Na kinachofanyika ni kushoofisha jitihada za kufunua uchafu huo na kufifisha kashfa hizo kwa nguvu zote, na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali katu havigusii jambo hili. Hakika tumefika pabaya na huko mbele yatatukuta kama yalivyowakuta wenzetu.

  Tukumbuke kwamba haki ya watu haiwezi kuendelea kuchezewa
  na wachache kwa maslahi binafsi.

   
 16. m

  mganga salum New Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila k2 kina sababu wacha makapi yarudi kwao...used spare haidumu..sidhani kama walikuja kwa heri.. Ni bora warudi
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Rushwa imetamalaki singida, mwigu na dewji wanapofusha akili wasingida kwa rushwa, bali nawaambia sasa hawawezi kuwapotosha walioongoka, wahangaika na hao wana wa upotoe. wamepata wapi ujasiri wa kurudi utumwani??? wamebadili uzaliwa wa kwanza kwa kunde!!!
   
 18. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hata chadema wanamchezo wa kuwanunua wapinzani wa vyama vingine mf. Lwakatare cuf, Lema TLP, kasulumbayi cuf, arfi cuf, hiyo ndio dhambi mliyotenda na bado itaendelea kuwatafuna na bado kwa kuwa nyie mnawanunua hawaji kwa cdm kwa mapenzi bali kwa kuwa walipewa pesa
   
 19. I

  Isango R I P

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama kweli wamehama, namshukuru Mungu, wengi wao walihongwa na tajiri mmoja mbunge ambaye huwa hafiki bungeni mara kwa mara, wakatusumbua sana katika uchaguzi Mkuu uliopita. utararibu wa viongozi wa CCM kununua wanachama, viongozi, au bendera za Chadema, Singida Mjini ni biashara, na mbunge wa jimbo hillo anafadhili sana mambo hayo. Wengine mtaamini hata jinsi anavyohonga watumishi wa serikali. Bungeni haendi, anapokuja kuonana na watu badala ya kusikiliza hoja zao, matatizo yao, anagawa 50,000 kwa mikutano maalumu anaondoka. Mmojawapo ya waliokuwa wanahongwa ki urahisi ni hao waliohama. Hilo ni kosa lenye heri kwa CHADEMA
   
 20. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  Bora ya kaisari yameeenda kwa Kaisari, hivi hawa wanatupimia na kudhani kuwa sie tunarubunika kirahisi hivyo????
  Wananchi tunaijua vizuri sana Si Si EM iliyojaa matapeli.

  Chapa rapa!!

  Peoples.........Power
   
Loading...