Viongozi wa vyama vya wafanyakazi mnatusaliti, mnatuuza na kutupuuza

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,047
1,503
Wafanyakazi, salaam!
Nimefika hatua ya kuandika hii kutokana na jinsi viongozi wa vyama vya wafanyakazi hawa kukaa kimya wakati:-
1. Wafanyakazi wakiwekwa sello mahali na sehemu mbalimbali kutokana na orders za viongozi wateule wa serikali,

2. Wafanyakazi kusimamishwa hivyo bila tuhuma zao kuthibitishwa,

3. Wafanyakazi kushitukizwa eti viongozi wanapima uwepo wa watumishi kazini nk nk nk

Kwa ufupi mlichaguliwa ili kulinda maslahi ya watumishi na kuungana na taasisi zinazowasumbua. WAJIBIKENI
 
Msakila,tupo kwenye zama za UUtakatifu.. ..na wewe ndio kada wake!
Hofu ni dhambi kubwa sana, inaweza kusababisha kukosa haki yako na ya wengine. inaweza kuharibu mfumo wa maisha kwa taifa. Acheni hofu viongozi wetu simamieni haki za watu wenu kwa mujibu wa sheria.ulichaguliwa kwa sababu watu walikuamini. thibitisha yao kwa kuwatendea Yale yapasayo
 
Vyama hivi ni bure kabisa,vinashindwa ishauri serikali. Watumishi tunasumbuliwa kwa kisingizio cha uhakiki,hatupandi madaraja,hatulipwi likizo,hatuendelezwi kupitia semina nk. tunazuiwa kwenda sehemu mbalimbali duniani kujifunza,hatushirikishwi kufikia maamuzi,kutupwa sero ni kirahisi nk nk. Nashangaa viongozi wa vyama vyetu eti wanakaa kimya kwao kazi yamhm nimaandalizi ya siku ya wafanyakazi. Shame on them
 
Jamani hatuna viongozi kabisa. Wao wanalipana posho kutokana na jasho letu lakini hawako tayari kuwajibika. Tazama, haki zetu watumishi zimegeuka agenda za kisiasa, hatuheshimiwi na wametujengea taswira mbaya sana kwa jamii tunayoihudumia. Sasa kwa waadilifu inaonekana ni laana kuwa mtumishi wa umma. Hivi, ninyi mnaulewa wajibu wenu kweli? Hakika najiondoa uanachama wa hivi vyama karibuni! LoH, shame on you!.
 
Mbele giza sio chochote chakumnufaisha mtumishi watetezi wawatumishi wamekuwa domo zege sjui uwoga au wanakula mlungula ili kutusaliti hata bank kwenyewe kukopa shida ila mungu anawaona tu endeleeni kula jasho letu nyie viongozi wa vyama vya wafanyakazi ila siku yenu ipo tu
 
Hawana uwezo Wa kutetea wafanyakazi tatizo njaa au uroho lkn inawezekana woga pia
 
Mie sitaki hata kuwasikia wajinga wakubwa hawa mkienda kuwalalamikia matatizo yenu wakija ofisini wanamalizana na waajiri akitoka huko ndani anawapiga bra braaa kibao mnabaki na matatzo yenu
 
Back
Top Bottom