Viongozi wa vyama vya wafanyakazi mnajimaliza wenyewe!!kuelekea mgomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi mnajimaliza wenyewe!!kuelekea mgomo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by major mkandala, Mar 22, 2010.

 1. m

  major mkandala Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  POLEN SANA ILA MNGEANZA KUSAFISHANA KWANZA KABLA YA MGOMO MCHAWI YUMO HUMO HUMO NDANI

  Wakati chama cha wafanyakazi kikipanga mgomo na kukataa uwakilishi wa serikali siku ya mei mossi...napenda kutoa wito wao kwa wao kwanza kuanza kusafishana....vyama vya tucta ,cotwu,chodawu vimekuwa mstari wa mbele kununuliwa na waajiri hasa wakati linapokuja mfanyakazi kudai haki yake,..swala hili nimeliona likipenyeza karibu kila shirika na yasiyo ya umma.viongozi hawa wamekuwa wakinunuliwa kwa pesa ndogo sana na waajiri kufikiria kusaini ama mkataba ama waraka wa kuwafukuza watu pasipokujua wanakuja watoto wao wanakuja kuathirka na mkataba ule ule waliosaini wenyewe ;so pengine serikali kukaa kimya wanajivunia baadhi yenu wakijua hata huo mgomo ausaidii kitu kama wataweza kuwakamata mkononi MWENYEKITI na KATIBU wa vyama vya wafanyakazi sehemu husika...michezo hii imeathiri maisha ya wengi huku wengine wakifurahia kuwa wajasiriamali..swala linaloumiza ni jinsi ya malipo wanayolipwa wanapostaafu ama kuachishwa kwa manufaa ya umma...ni vyema nyie wenyewe mkaanza kujisafisha ....ninao mfano mdogo sana hapo chini...
  WAFANYAKAZI 128 wa Kiwanda cha Nyuzi cha New Tabora Textiles Ltd akiwemo Mwenyekiti wa Tawi la Chama cha Wafanyakazi (TUICO) kiwandani humo, Ramadhani Wakulichombe, wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kugoma kupinga menejimenti ya kiwanda hicho kuiingiza Jumapili kama siku ya kazi, badala ya mapumziko.

  Hatua hiyo ilifikiwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Idara ya Kazi mkoani hapa, Novemba 3, mwaka jana, baada ya TUICO kufungua kesi katika Idara ya Kazi baada ya wafanyakazi wote 345 kiwandani hapo kushindwa kuafikiana na Menejimenti ya kiwanda juu ya kufanya kazi Jumapili ambayo kawaida ni siku ya mapumziko.

  Aidha, katika hukumu hiyo, Tume hiyo chini ya kifungu cha 89 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004 pamoja kanuni na mwongozo wa usuluhishi na uamuazi, kimezingatia tangazo la serikali la Namba 67 la mwaka 2007 kuwa wafanyakazi 128 kati ya 345 walikaa nyumbani kupinga kufanya kazi siku ya Jumapili huku wafanyakazi 217 wakiridhia na kurudi kujaza mikataba ya kufanya kazi siku hiyo.


   
 2. m

  major mkandala Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aidha, awali kabla ya hatua hiyo, Tawi la Tuico chini ya Mwenyekiti wake, Wakulichombe walikaa na menejimenti ya kiwanda hicho na kupinga uamuzi wa kufanya kazi Jumapili na kwamba endapo wanataka siku hiyo iingizwe kazini, basi ni vyema kila mfanyakazi akapatiwa nyongeza ya Sh 30,000 mbali ya mshahara wake.

  Mazungumzo hayo yalikubaliwa kabla ya menejimenti hiyo kughairi kutoa nyongeza hiyo hali ambayo ililazimu uongozi wa Tuico Taifa na Mkoa wa Tabora, kuingilia kati katika mazungumzo hayo ambayo kwa mujibu wa kikao hicho, walikubaliana kwa pamoja kulipwa nyongeza hiyo katika makubaliano ya Januari 14, mwaka jana.

  Hata hivyo, menejimenti ilibadili tena maamuzi hayo na wafanyakazi 345 walikubaliana na tawi lao la Tuico, kugoma na kukaa nyumbani Juni ambapo wakiwa katika mgomo huo, baadhi ya wafanyakazi waliamua kurudi kazini baada ya menejimenti kutishia kuwafuta kazi na kuajiri wengine.

  Aidha, kutokana na wafanyakazi 217 kuamua kurejea kazini, wafanyakazi 128 walifungua kesi Idara ya Kazi Tabora, Agosti na hukumu kutolewa Novemba 3, mwaka jana, wakidaiwa walikiuka sheria za kazi kwa kukaa nyumbani siku 20 bila kufika kazini, na kukaidi kujieleza mbele ya menejimenti juu ya hatua hiyo.

  Wakulichombe alisema pamoja na hukumu hiyo, bado anaona kama haki haikutendeka kwani maamuzi yanalenga hisia zaidi kuliko taratibu za kazi na ajira.

  Wakulichombe ambaye alikuwa ni Idara ya Fedha, alisema alikuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyakazi wenzake na kilichopo hadi sasa ni hujuma iliyofanywa na baadhi ya viongozi wenzake wa Tawi la Tuico kwa kukaa kikao cha siri na menejimenti ya kiwanda hicho na kuhujumu maamuzi halali ya wafanyakazi wenzao.

  Aidha, alisema licha ya hukumu hiyo kutolewa na wafanyakazi 128 kutakiwa kulipwa haki yao baada ya kuachishwa kazi, kama hukumu inavyoagiza, hadi leo hawajalipwa fedha hizo kama sheria inavyoagiza na suala hilo kila wakifuatilia limekuwa ni danadanada kutoka kwa menejimenti ya kiwanda.

   
 3. m

  major mkandala Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WITO
  hili ni moja tu ya mifano ipo mifano mingi inayosikitisha...zaidi ya yote imefika watanzania kuacha kutegemea MISHAHARA ya maofisini...pesa ile ile ndogo unayo uwezo wa kuanzisha biashara ambayo iatweza kukupa sh 5000 mpaka kumi kwa siku na hivyo kuondokana na uzandiki wa mishahara..wazee wengi wanakuja kuteseka pale inapotokea swala kama hili ..ni kweli huzunikukuta mtu amemaliza miaka 32 akifanya kazi sehemu na kulipwa million 7 ...hiyo hiyo million 7 kama ungekuwa na biashara miaka 20 ya mwisho ungekuwa umezalisha sh ngapi??watanzania tuache kuumizwa...tyuhangaike....fungua genge hapo kwako ..faida unayopata utaifuraha mwenyewe kama si mwoga kopa..watanzania wengi wanakosa maisha bora kutokana na kuogopa kukopa ama kushindw a kutokana na masharti ya benki..tusiwe waoga...asilimia 70 ya wafanya biashara akiwam\mo Nugu yangu MENGI ni mpenzi wa mkopo na ndio maana tunaona anatoka mpaka sasa....jaribu kukopa usifike wakati unaambiwa kazi basi unakuwa kichaa..na wengine wanaachwa na ma boyfriend zao basi shida tupu..ukiwa na nguvu zako kuwa mjasiriamali..ukipunguzwa endeleza maisha yako ya kwa kutanua wigo wa biashara....

  Polen sana ;ila muwangalie mgomo una manufaa gani kama baadhi yenu mnanunuliwa na maamuzi makubwa yanafanyika...
   
Loading...