Viongozi wa vyama vya siasa, Serikali na Bunge acheni unafiki shule zote za Serikali ziwe English medium watoto wenu mbona wanasoma English Medium?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kuna maana gani viongozi wa Serikali, bunge na vyama vya siasa kusomesha watoto wao English medium schools halafu wanaacha watoto wa wengine wasome Swahili medium? Huu ni unafiki mkubwa.

Badilisheni shule zote za Serikali ziwe English medium.

Wanafiki wakubwa nyie msio na haya

Hizi ndizo salamu zangu kwenu za mwaka mpya
 
Kwa mala ya kwanza umeongea hoja zenye mashiko! Ungekuwa rafiki yangu wa kuaminika ningekupa chronological flow! Na ushahidi kuwa kwa upande mmoja kiswahili kimeliunganisha taifa lakini lengo la awali halikuwa zuri?!

Kama lengo la awali halikuwa jema, kiswahili ni moja ya 'laana' especially kwenye mfumo wa elimu!

Reference kama wewe ni mchunguzi, jua je ni lini Mwalimu alibadiri gia kutoka kuwa bepari mpaka mjamaa, 1966 while mapinduzi yalikuwa 1964, and Azimio 1967!

Curses kwa nchi hii ni 1. Azimio la Arusha, (kudhurumu Mali za watu) 2. Kiswahili 1967 ili kuudhoofisha mfumo wa elimu etc.

Yote hayo yalipangwa baada ya jaribio la mapinduzi 1964.
 
Akili kama hii ikiingia 2020 inabidi tulie kilio Cha kusaga meno kwa sababu tutaangamiza taifa letu
Mijadala kama hii ni bora ungekuwa unapitia coments ili ujifunze kitu, kuliko kuandika usichokijua!

Historia usiyoijua ni 1964, kulitolea jeribio LA mapinduzi na walimpindua Mwalimu, kati ya makundi yaliyosemekana kushiriki, ni Wasomi, Wafanya biashara na Wanajeshi weusi.

Baada ya kuzima mapinduzi, mwalimu alishauriwa na makachero ya uingereza adhibiti hayo makundi, kwanza akabadili gia, alikuwa bepari akawa mjamaa toka 1966 baada ya kwenda China, mbili akabadiri lugha ya kufundishia 1967, kutoka english to Swahili ili kupunguza wanaojielewa a.k.a wasomi, tatu akatangaza azimio la Arusha ili kudhibiti wafanya biashara na kuwapora Mali zao etc!

Kaa pembeni ujue mambo sio unatumia usichokijua
 
Hii itakua ngumu mno! watoto wetu watafeli mpaka basi

English medium ni mfumo mzuri sana nami pia niseme wazi mwanangu yupo huko anapiga zake ngeli

hii haitewezekana kwa sababu ya walimu wengi wanaofundisha kayumba English ni tatizo kubwa kwao, labda useme wote watimuliwe waajiriwe wengine nchi nzima wataofit na mfumo wa english media

Vyuo vya walimu pia hasa hivi vya certificate vibadilisho

Elimu bure hii ya kiswahili serikali inashindwa, itaweza vipi elimu kwa english media?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom