Viongozi wa ushirika kortini wa uhujumu uchumi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Viongozi wa ushirika kortini wa uhujumu uchumi Send to a friend Saturday, 16 April 2011 08:37

Daniel Mjema,Moshi
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Kilimanjaro, imemburuta
mahakamani, Diwani wa Machame, wilayani Hai Rajabu Nkya (CCM) na watu wengine wawili kwa tuhuma za
uhujumu uchumi.

Desemba 6 mwaka jana, Mwananchi lilifichua tuhuma za kuwapo kwa vitendo vya ufisadi wa Sh52 milioni, katika Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nkuu-Machame, ukimhusisha Nkya ambaye ni Mwenyekiti wa
chama hicho.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alikanusha vikali tuhuma hizo na kwamba ni chokochoko zinazochochewa na baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho walioondolewa madarakani.

Lakini jana Takukuru ilimfikisha Nkya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Hai,Denis Mpelembwa na kumsomea mashtaka mawili likiwamo la uhujumu uchumi na kushindwa kutimiza masharti ya
dhamana.

Washtakiwa wengine katika waliosomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Maghela Ndimbo, ni Katibu wa chama hicho, Esther Shoo na mfanyabiashara Awadhi Lema.

Katika shtaka la kwanza linalowahusu Nkya na Shoo, mwendesha mashtaka alidai kuwa kati ya Machi na Oktoba mwakan 2007, washtakiwa walikisababishia chama hicho hasara ya Sh38 milioni, kwa kununua trekta kuukuu (mtumba).Ilidaiwa kuwa trekta hilo lilinunuliwa kutoka kwa mshtakiwa Lema.

Ilidaiwa kuwa kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao ni matumizi mabaya ya ofisi ya chama hicho, kosa ambalo ni kinyume cha kifungu namba 31 cha sheria namba 11 ya kuzuia na kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho hicho, washtakiwa wote watatu kwa makusudi wanadaiwa kukisababishia chama hicho hasara ya Sh21,176,725 kosa linaloangukia kwenye uhujumu uchumi.

Washtakiwa Nkya na Lema walikanusha mashtaka yanayowakabili lakini mshtakiwa Shoo, akakiri kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi.

Aprili 28 upande wa mashtaka utamsomea maelezo ya kosa.

Kwa kuwa kosa linaloangukia chini ya sheria ya uhujumu uchumi linamtaka mshtakiwa kuweka mahakamani fedha taslimu ambayo ni nusu ya kiasi alichosababisha hasara au hati za mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Kutokana na sharti hilo, ni mshtakiwa Nkya aliwasilisha hati ya nyumba ambayo ilikataliwa na mahakama kwa kuwa ilikuwa haijaambatanishwa na ripoti ya mthamini na washitakiwa wengine waliobaki kushindwa
kutimiza sharti hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom