Viongozi wa umma kutaja mali zao ni kinyume cha katiba?

moshingi

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
278
92
Jana nilimuona yule mama Jaji akipiga mkwala kwenye luninga kuwa ifikapo tarehe 31/12/20011 lazima kila kiongozi wa uma awe
amejaza fomu maalumu za kutaja mali na madeni aliyonayo bila kuficha lolote. Pamoja na kwamba naafiki maudhui ya sheria
ya maadili ya viongozi wa uma inayowapa viongozi wetu sharti hilo ili kuwadhibiti viongozi hao wasijinufaishe isivyo halali kupitia nyadhifa zao, lakini hakuna ushahidi wa jinsi sheria hiyo ilivyofanikiwa kuzuia viongozi wetu wasituibie. Hata hivyo kipengele cha kutaja
mali ni kama vile kipo kinyume cha katiba hususani haki ya faragha"Right to Privacy". Mali na madeni aliyonayo mtu ni sehemu ya faragha yake. iweje alazimishwe kutangaza? Great thinkers tujaribu kulitazama hili kwa undani.
 
Hii ni perspective ya wazungu zaidi. Kwa mfano hiyo ya 'Gender Identity and Sexualty' kukubalika kwake siyo universal. Ni ubazazi wa wazungu. Kama ningeiandika from the African perspective ningefanya nyongeza kama:

  • Right of old people to be looked after by their children and society in general,
  • Right of parents to be respected by their children and old people to be respected by young people,
  • Right for every child to receive a decent education without regard to his/her economic/social circumstances, etc.
 
Nasikitika jinsi wa jf mmekuwa kimya bila kuchangia uzi huu kwa wingi ili tupate picha halisi ya;
(i) Je ni kwa kiwango gani sheria hiyo imetusaidia kuwazuia viongozi wetu wasituibie, mbona
tumeendelea kusikia habari kama EPA, RICHMOND, KIWIRA, nk.?

(ii) Mbona hatusikii mali walizochuma mara wanapomaliza utumishi?

(ii) Je haki ya faragha ipo dhidi ya haki ya kupata habari?( na kinyume chake)

Hata hivyo Mkuu uliyenijibu kwa kuniwekea link kibao sina hakika kuhusu uelewa wako wa kisheria,
kama mali na madeni siyo faragha ya mtu, je ni kwanini kifungu cha 81 cha sheria ya ushahidi ya Tanzania
inawakataza maafisa wa benki kutoa habari yeyote kuhusiana na akaunti ya mteja isipokuwa kwa amri ya mahakama.
Zipo sheria nyingine kibao hapa nchini zinazolinda habari za mali na madeni ya mtu zisisambazwe isipokuwa kwa hiyari yake.

Karibuni Great Thinkers hili bado ni jambo muhimu sana linafaa kujadili, hii ni zaidi ya siasa.
 
Sheria hii haijawahi kuwasaidia Watanzania...bado tunaendelea kusikia habari mbaya sana
tunaibiwa kila siku, viongozi wanahusika lakini hawafikishwi mahakamani...hii sekretarieti
inakula kodi zetu bure kwa vile haina meno!!
 
Back
Top Bottom