Viongozi wa ukawa na meya wa kinondoni someni hii

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Meya wangu wa manispaa ya kinondoni mstahiki Boniface Jacob nakumbuka ulitoa taarifa kwenye ukurasa wako wa facebook ya kwamba kuna pesa imetengwa kiasi cha TSH,milioni 200.ulisema pesa hiyo imetengwa kwa ajili ya kuwakopesa vijana na wanawake wa manispaa ya kinondoni tu,sasa ni hivi,ile pesa ulisema itapitia benki ya DCB,sasa kwa taarifa yako asilimia kubwa ya wananchi tumeshindwa kwenda kukopa hiyo pesa kwa sababu mashariti ya kukopesha kwa ile benki ni makubwa sana,sehemu kubwa ya wananchi wa kinondoni wameshindwa,kwa hivo hiyo pesa itapigwa juu kwa juu kama hamtakuwa makini kwa sababu wakopaji hawapo kutokana na mashariti ya ile benki,kwa heri
 
Nashauri wakaazi wa kinondoni wajiunge kwenye vikundi watu 5 na kuandika mpango kazi wao.....wakienda kwa style hiyo watapata ule mkopo! Usiende mwenyewe maana dhaman huwa kubwa na sisi wa Tanzania hatuna hizo dhamana!
 
Back
Top Bottom