Viongozi wa Uamsho wadai polisi waliwafanyia ukatili

Status
Not open for further replies.
karume alikuwa mtanganyika au mzanzibari?? kama alikuwa mzanzibari na unakubali alifanya hayo, iweje leo iwe haiwezekani tena kwa wazanzibari kuteswa zanzibar?

Nilikwambia, sio Karume tu mpaka Nyerere alifanya hayo, akawatoa kwenye magereza yao hadi kwake Tanganyika, na hadi hatukuwaona tena.... hilo nalo pia lipo japokuwa unalikwepa kuzungumzia , na hayo ya Uamsho leo nadhani ni mwendelezo wa yale muloyaridhi kwa Baba yenu wa Taifa,
 
kwani nani kabisha ya nyerere? wewe unabisha ya wazanzibari ndio tatizo! wazanzibari malaika?
 
Naam, ahsante Mkuu kwa kuyakubali maovu ya Mzee wenu mpenzi, na kwa upande wetu Wazanzibar tulipinga na tutapinga vikali ukatili na udhalilishwaji wa Wazanzibar wetu, hata Kama wanakosa kama inavyotajwa japokuwa halina ushahidi mpaka sasa, na pia tunapinga kile kitendo cha kuwato Zanzibar nchini kwetu kwenye mahkama na magereza yetu, hili kwako hujaliona...??
 
asante sana na wewe. sasa turudi kwenye mada, kuna ushahidi gani kuwa hawa jamaa wamefanyiwa hayo mambo zaidi ya maneno yao wenyewe? kwa nini tumuamini mtu ambaye tayari anashitakiwa? si na wao washitaki ili uchunguzi ufanyike? wanajua fika kuwa maneno yao kwa sasa yatapuuzwa tu, na sababu pekee wanayasema ni ili kutaka huruma za waislamu tu, ndio maana wanaunganisha mambo ya katiba humo humo, mambo ya tanganyika humo humo.....
 
Ndio, Kama ilivyo upande wenu kuamini jambo lililokosa ushahidi, sasa kwanini nasie tusiamini maneno yao tena hassa kwa watu walioaminika kiimanai Moyoni mwetu, au ndio tusema sote tuwe masukule kuaminishwa kila jambo....
lakini pia nikueke sawa, hao jamaa sio WASHTAKIWA ndio anza WATUHUMIWA, kwanini tusiwaamini....?
Ndio Kama Waislamu huruma ni ibada kwetu tena ni sadaka zaidi ya ile munayoitoa kila Jumapili , kwanini tusiwahurumie....?
Na suala la kuungaunga hoja ni kwa sababu mpaka sasa hawajui wamepalekwa mahakamani kwa kosa gani, maaana mpaka sasa ushahidi haupo ... Ni vyema kutafuta ushahidi sio kuwafhalilisha...
 
Ha ha ha ha ha ha ha Mwiba Mahakama za Zanzibar hazina tofauti na mahakana za Rwanda ni uchuro mtupu bado hazijawa tayari kushughulikia masuala mazito kama ugaidi.Mahakama za Zanzibar labda zinaweza kumudu kesi kama watu wanaokula hadharani kipindi cha mfungo mwezi wa Ramadhan.

Hao ni raia wa Zanzibar hivyo huko ugenini hata kuhukumiwa kunyongwa inawezekana kabisa ,usitegemee kutendewa haki na adui anaeibana Zanzibar kwa kila hali. Si unaona wanavyodhalilishwa ,jaji kasemaje amekuwa kama hasikii anayoambiwa na hapendi yanavyozungumzwa .
 
Last edited by a moderator:
Maskini zanzibar kwish nehi daa kumbe hao muamsho washafika huko kweli zanzibar hakuna rais kuna konokono sasa iweje kosa wafanye Zanzibar washtakiwe Dar es salaam duu kweli zanzibar hakuna mahakama kuna madanguroo ya kuhukumia ayaa Ila mungu yupo salama yao wasije kuwaua tuu maana wakiwaua na uchaguzi huu unaokuja Ccm hana chake Zanzibar
 
''CUF'' TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Bila ya shaka kila mmoja wetu ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ameshtushwa kwa kiasi kikubwa baada ya kupata taarifa ya kunyanyaswa vikalai pamoja na kufanyia matendo ya kulawitiwa viongozi wa Jumuia ya Uamsho Zanzibar.

Matendo haya katika hali ya kiubinadamu hayafai kabisa na nidhahir kwa kila mmoja wetu kuyapiga vita ili jamii na mataifa kwa ujumla wazisikie sauti zetu juu ya viongozi hawa wakubwa wa Dini ya Kiislamu.

Tukiwa kama taasisi kubwa ya hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF tunalaani vikali ukatili na ushenzi uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na wenzao 19,Kwa mujibu wa walivyoeleza watuhumiwa hao wakiwa Mahakama ya kisutu Shekh Farid Had Ahmed na wenzake Jeshi la polisi limewafanyia ukatili wa hali ya juu usiostahili kwa binadamu.

Mahabusu hao wanaozuliwa huko Daresalama wanadai kuhojiwa wakiwa uchi wa mnyama, kulawitiwa na askri wa Jeshi la polisi,kuwekewa vitu vyenye ncha kali kwenye sehemu za haja kubwa na mateso maengine mengi ikiwa ni pamoja na kupigwa hadi kuumizwa,Hata kama ni wakosaji matendo haya ni kinyume na haki za binadamu hayapaswi kufanyiwa binadamu kama hawa tena raia halali wa Nchi hii.

Tunauliza ipo wapi haki ya kisheria ya mwananchi wan chi hii ikiwa jeshi la polisi ndio wanaovunja sheria baada ya kulinda shera?

Inashangaza kuona vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Makaburu dhidi ya Watu weusi wa Afrika Kusini sasa Vinafanywa na Vijana wa Kitanzania dhidi ya Watanzania wenzao kwa kisingizio cha Ugaidi.

Sisi CUF hatuoni mantiki ya uvunjaji wa Haki za Binadamu kwa kiasi hiki kwa watu wanaotuhumiwa kwa kile kinachoitwa kujishirikisha na Matendo ya Kigaidi.

Hata kama watuhumiwa hao watiwa hatiani kwa makosa hayo, bado hukumu yao haitakua kulawitiwa kama ilivyoelezwa na mmoja kati ya Watuhumiwa hao mbele ya Mahakama.

Polisi mnapaswa kujua kwamba mnaowafanyia matendo hayo bado ni watuhumiwa tu wa matendo ya ugaidi je wakishinda kesi na kuonekana hawana hatia na nyinyi mchukuliwe hatua za kisheria?

Ikiwa matendo hayo yanafanywa kwa makusudi na Jeshi la Polisi dhidi ya Viongozi wa Dini ya kiislamu tena yenye asilimia 99 ya wakaazi wa Zanzibar hivi munataka wafuasi wao na Familia zao wafanye nini ?

CUF-Chama cha Wananchi kutokana na kauli mbiu yake ya ‘’haki sawa kwa wote’’ tunamtaka Rais kutoa kauli na Msimamo wa Serikali dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji huu uliofanywa na Jeshi la Polisi ili Wananchi wapate kujua hatua zitakazo chukuliwa na Serikali sambamba na kukubali Ombi la Watuhumiwa la kufanyiwa uchunguzi wa Afya zao kama lilivyo wasilishwa kwenye Mahakama inayosikiliza Kesi hiyo.

Tunatoa wito kwa Taasisi za kimataifa na kitaifa zinazoshughulikia mambo ya Uvunjwaji wa Haki za Binaadamu kufuatilia kwa Karibu suala hili na kuchukua hatua zinazostahili vingenevyo siku moja wanaweza kushuhudia maiti ikipelekwa mahakamani kama walivodai watuhumiwa hao mbele ya Mahakama ya kisutu.

Tumeshuhudia malalamiko ya watuhumiwa hao kupitia vyombo vya habari wanasema kwamba mpaka hivi sasa wale waliojeruhiwa bado wanaugulia maumivu na hawajapewa matibabu yoyote yale licha ya kufanyia matendo makubwa ya kishenzi wanaendelea kusota ndani tu hivi hamuoni kama hii ni hatari zaidi kwa watuhumiwa hawa?

Tukiwa kama wadau wakubwa wa Chama cha siasa hapa Nchini tuna imani kwamba taarifa yetu hii itafanyiwa kazi na hatua za kisheria kuchukuliwa haraka sana iwezekanovyo ili kuepusha majanga zaidi ndania ya Nchi yetu.

Chama cha Wananachi CUF kinawaomba ndugu na jamaa pamoja na waislamu wote Nchini kuendelea kuwa na subra tukiamini kwamba sheria itachukuliwa dhidhi ya viongozi hawa.

Imetolewa na
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi Habri na Uenezi CUF.
 
lete ushahidi kama hao ni magaidi miezi sasa bado wenzio wanahaika na upelelezi na hata ukija utakua wa kufuma fuma tu na nyuzi kibao

innocent until proven guilty huu ni msingi ambao wote tunakubaliana kwanini wao waadhibiwe hata kabla tuhuma zao hazijathibitishwa.
 
Kimsingi kitendo cha polisi, walichofanya kwa watuhumiwa hakikubaliki, na unyama huo unatakiwa ulaaniwa na kila mtanzania mwema na..

serekali iwavhukulie hatua polisi waliofanya unyama huo.
 
inajulikana wazi kua hawa si magaidi na inajulikana wazi huku kuwakomoa kwa msimamo wao wa kusema hadharani muungano huu ni wa dhulma.

na nnaamini serikali inafanya hivi kwa kudhani ati itawatisha wananchi kusema ukweli kua huu muungano ni magumashi.

ndio yanayomkuta mansour wanamheshimu kwa sababu mwanamapinduzi mwenzao na kaoa mtoto wa karume father.

kwa kweli wanajenga chuki hasa kwa upande wa zanzibar, na si chuki tu hii inaweza kupelekea reaction mbaya sana, wajue yanayotokea kwengine yalianza hivi hivi.

cha msingi serikali isipuuze haya malalamiko ya watuhumiwa iundwe kamati ikiwamo madaktari na kufatilia afya zao kisha itoe ripoti kwa umma na wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu

la si hivyo sisi ni mashahidi tutaona nn kitatokea ambacho naamini si chema kwa taifa letu
 
Sio vema vitendo kama hivo walivofanyiwa watuhimiwa
kama ni ukweli wamefanywa namna hiyo

Sent from my iPhone using JamiiForum

Kwa namna ambavyo watuhumiwa wametoa tuhuma hizo, nina hakika hawajasema ukweli!

Hizo tuhuma ni za kutunga na hivyo zipuuzwe!
 
kitendo cha polisi cha kuwadhalilisha watuhumiwa ni unyama uliopindukia! kama Serikali yetu inajali haki za binaadamu na kuheshimu utawala wa sheria basi iwachukulie hatua za kisheria wale wote waliohusika na ukatili huo! kinyume chake wananchi tutakosa imani na Serikali hii ya CCM!
 
Watuhumiwa ni wazushi kwa kuwasingizia polisi, wanataka huruma ya wananchi!
 
''CUF'' TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Bila ya shaka kila mmoja wetu ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ameshtushwa kwa kiasi kikubwa baada ya kupata taarifa ya kunyanyaswa vikalai pamoja na kufanyia matendo ya kulawitiwa viongozi wa Jumuia ya Uamsho Zanzibar.

Matendo haya katika hali ya kiubinadamu hayafai kabisa na nidhahir kwa kila mmoja wetu kuyapiga vita ili jamii na mataifa kwa ujumla wazisikie sauti zetu juu ya viongozi hawa wakubwa wa Dini ya Kiislamu.

Tukiwa kama taasisi kubwa ya hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF tunalaani vikali ukatili na ushenzi uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na wenzao 19,Kwa mujibu wa walivyoeleza watuhumiwa hao wakiwa Mahakama ya kisutu Shekh Farid Had Ahmed na wenzake Jeshi la polisi limewafanyia ukatili wa hali ya juu usiostahili kwa binadamu.

Mahabusu hao wanaozuliwa huko Daresalama wanadai kuhojiwa wakiwa uchi wa mnyama, kulawitiwa na askri wa Jeshi la polisi,kuwekewa vitu vyenye ncha kali kwenye sehemu za haja kubwa na mateso maengine mengi ikiwa ni pamoja na kupigwa hadi kuumizwa,Hata kama ni wakosaji matendo haya ni kinyume na haki za binadamu hayapaswi kufanyiwa binadamu kama hawa tena raia halali wa Nchi hii.

Tunauliza ipo wapi haki ya kisheria ya mwananchi wan chi hii ikiwa jeshi la polisi ndio wanaovunja sheria baada ya kulinda shera?

Inashangaza kuona vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Makaburu dhidi ya Watu weusi wa Afrika Kusini sasa Vinafanywa na Vijana wa Kitanzania dhidi ya Watanzania wenzao kwa kisingizio cha Ugaidi.

Sisi CUF hatuoni mantiki ya uvunjaji wa Haki za Binadamu kwa kiasi hiki kwa watu wanaotuhumiwa kwa kile kinachoitwa kujishirikisha na Matendo ya Kigaidi.

Hata kama watuhumiwa hao watiwa hatiani kwa makosa hayo, bado hukumu yao haitakua kulawitiwa kama ilivyoelezwa na mmoja kati ya Watuhumiwa hao mbele ya Mahakama.

Polisi mnapaswa kujua kwamba mnaowafanyia matendo hayo bado ni watuhumiwa tu wa matendo ya ugaidi je wakishinda kesi na kuonekana hawana hatia na nyinyi mchukuliwe hatua za kisheria?

Ikiwa matendo hayo yanafanywa kwa makusudi na Jeshi la Polisi dhidi ya Viongozi wa Dini ya kiislamu tena yenye asilimia 99 ya wakaazi wa Zanzibar hivi munataka wafuasi wao na Familia zao wafanye nini ?

CUF-Chama cha Wananchi kutokana na kauli mbiu yake ya ‘’haki sawa kwa wote’’ tunamtaka Rais kutoa kauli na Msimamo wa Serikali dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji huu uliofanywa na Jeshi la Polisi ili Wananchi wapate kujua hatua zitakazo chukuliwa na Serikali sambamba na kukubali Ombi la Watuhumiwa la kufanyiwa uchunguzi wa Afya zao kama lilivyo wasilishwa kwenye Mahakama inayosikiliza Kesi hiyo.

Tunatoa wito kwa Taasisi za kimataifa na kitaifa zinazoshughulikia mambo ya Uvunjwaji wa Haki za Binaadamu kufuatilia kwa Karibu suala hili na kuchukua hatua zinazostahili vingenevyo siku moja wanaweza kushuhudia maiti ikipelekwa mahakamani kama walivodai watuhumiwa hao mbele ya Mahakama ya kisutu.

Tumeshuhudia malalamiko ya watuhumiwa hao kupitia vyombo vya habari wanasema kwamba mpaka hivi sasa wale waliojeruhiwa bado wanaugulia maumivu na hawajapewa matibabu yoyote yale licha ya kufanyia matendo makubwa ya kishenzi wanaendelea kusota ndani tu hivi hamuoni kama hii ni hatari zaidi kwa watuhumiwa hawa?

Tukiwa kama wadau wakubwa wa Chama cha siasa hapa Nchini tuna imani kwamba taarifa yetu hii itafanyiwa kazi na hatua za kisheria kuchukuliwa haraka sana iwezekanovyo ili kuepusha majanga zaidi ndania ya Nchi yetu.

Chama cha Wananachi CUF kinawaomba ndugu na jamaa pamoja na waislamu wote Nchini kuendelea kuwa na subra tukiamini kwamba sheria itachukuliwa dhidhi ya viongozi hawa.

Imetolewa na
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi Habri na Uenezi CUF.

Hao polisi wapelekwe mahamakani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom