Viongozi wa Tanzania waanze kongea na Watanzania wanaoishi Nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa Tanzania waanze kongea na Watanzania wanaoishi Nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Apr 19, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Kwa mawazo yangu imefika wakati wa viongozi wa Tanzania wa CCM na wapinzani kuanza kuwahusisha Watanzania wanaoishi nje kwenye agenda za maendeleo ya nchi. Ingawa Watanzania sio wengi kama Wanigeria au Wahindi viongozi wa Tanzania wanatakiwa kufanya ziara hata kama ni mara chache kupata mawazo tofauti ya kujenga taifa letu. Tunaona wabunge wakija nje kwa misaada tu lakini kuna Watanzania wengi wanaoweza kuchangia kimawazo kuendeleza nchi yetu. Imefikia wakati wa wabungu na viongozi mbalimbali kufanya ziara za kimaendeleo za kudumisha Uzalendo kwa kutembelea jumuia mbalimbali za Watanzania nje ya nchi. Kitu kikubwa kinachotusaidia sisi kujua nchi inaendaje ni Internet/blogs lakini tungependa viongozi kuja na kuongea nao kwa undani.
  Kuna vitu ambavyo Watanzania inabidi tusivifanye vya siasa kama elimu, barabara, ulinzi, afya, maji na nishati. Imefika wakati wa kuokoo nchi yetu na jitihada zinatakiwa zitoke kwa kila Mtanzania duniani.
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Wazo jema bila shaka viongozi wetu wa kimageuzi wapo hum jf Slaa,Mbowe,Mnyika nk na hata wale nyoka walio update sumu ya wamo!!
   
 3. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Mh!.. Yaani tuwaongezee safari nyingine za kwenda nje!??... Gharama zitakazotumika kulipia hizo safari za kufuata mawazo (ambayo yanaweza yakawa positive or negative) zitakua na thamani kubwa kuliko hayo mawazo yenyewe.... By the way kuna watanzania wengi tuu wanaoishi hapahapa ambao wana mawazo positive yenye kujenga nchi ni vema yangezingatiwa yao kwanza... ( unless unaamini watz walioko nje wanamawazo positive kuliko hawa waliopo hapa)!...
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Watu hawafanani na kila wazo ni muhimu kwa nchi yetu kwasasa. Mimi naomini gharama si shida kama kuna mbunge anataka kuja kuongea na watanzania na hana budget anaweza kuomba pesa na watu watamchangia. Ukiiaangalia vizuri gharama si tofauti sana na kufanya ziara mikoani Ticket ya ndege kuja USA ni kama $1500-$2000 na Hotel za kawaida ni $80-$200 kwa siku hivyo kiongozi akija kwa siku nne anaweza kutumia $3,000 na hii safari inaweza kuwa moja au mbili kwa mwaka!! je kuna ubaya gani??. Mimi naamini elimu haina mipaka hivyo ni kama kujielimisha kwa kiasi fulani hivi. Vilevile hii haina maana hawa viongozi wasifanye ziara kwenye majimbo lakini tunaomba tuwe kwenye ratiba. Dunia imekuwa ndogo sana hivyo inabidi tuache fikra kwamba kwenda nje ni kupoteza pesa kwani kuna viongozi wanatumia pesa nyingi zaidi ya hata kwenda nje kwenye safari za hapohapo mfano ndege ya kwenda mwanza na kuridi ni $300
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni wazo zuri sana, mawazo ya watu walio nje ya nchi inapendeza yakichanganywa na ya watu nyumbani tunaweza kutoa kitu kizuri sana kwa manufaa makuu ya nchi, kwa mfano kutengeneza program za kuendeleza utaalamu zaidi wa masuala mbalimbali ambayo kwetu yanapwaya.... Pia naamini nchi nyingi sana zinazoendelea kwa kasi (yetu imesimama) wametumia hiyo njia na imefaa sana, na kwa kiasi fulani nasikia enzi za mwalimu kulikuwa na mpango wa kupeleka watu wetu huko nje kujenga utaalamu zaidi!
  Lakini kwa jinsi tunavyosimamia vipaumbele vyetu kwa sasa (utawala uliopo), hilo wazo inabidi liendelee kuwekwa kwenye harakati hizi hai, na iwe miongoni mwa agenda katika "TANZANIA MPYA".
  Ni kitu ambacho kinawezekana kwa serikali makini na ya watu!
   
 6. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  I doubt that...

  Nauli = 4000$ * 2 (kwenda na kurudi) = 8000$ approximately... 12,000,000/=Tsh
  Hoteli = 200$ * 4 days = 800$ approximately... 1,200,000/= Tsh
  Total per trip = 13,200,000/= Tsh
  Umesema angalau 'safari mbili kwa mwaka' = 26,400,000 + Time (kwa mbunge mmoja)
  Kwangu mimi hii hela ni kubwa aloo... 26,400,000 inaweza kulipia ada za watoto 1320 kwenye shule za kata!...

  Kwenda nje kufanya jambo lolote ambalo hapahapa nyumbani linaweza kufanyika tenakwa gharama ndogo ni kupoteza pesa....
  Dunia imekua kijiji.. Now days wafanyabiashara wakubwa na hata wanasiasa walioendelea wanatumia technologia kuwasiliana. Nimewahi kuona kwenye tv matangazo ya vifaa vinavyowawezesha watu kufanya mikutano wakiwa mbalimbali (geographically) nnaimani vipo na vinafaa...

  Kwa basi haizidi 80,000 (as an alternative way)!.. Nipe alternative ya kufika huko!...
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Avatar umesafiri lini kwenda nje na hizo namba unatoa wapi??

  Round trip $1500-$2,000 hii ni kwenda na kurudi. Kuna wakati wa low season Jan-April na Octo-Nov ticket za round trip zinaenda mpaka $1,200. Hotel 2 hadi 3 star kwa chumba kimoja ni kama $125 hivi bila kupata deal kwa siku. Chakula ni kama $30 kwa siku nzima.

  Hivyo Gharama za juu kabisa

  $2,000+($200*4)+($30*4) = $2,920 na usafiri utatolewa na wenyeji. Hii ni kwa safari moja na safari mbili ni $5,840. Na Hizi ni gharama za juu. Naona watu wengi inakuwa vigumu kuamini lakini sisi tunaishi huku kwa miaka mingi na naomba tuaminiane. Kama hujui unaweza kulipa pesa nyingi lakini kama kiongozi akitumia jumuia watampatia deal kama hii hapa huu ndiyo ukweli. Sasa kama kiongozi atataka kukaa 5* na atembee kwenye limo hapo itakuwa tofauti!!. Haya mambo si ya kuyakuza sisi na Watanzania wengine tunasafiri kila siku kikazi au kifamilia na tunajua gharama.
   
 8. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Okey... Unaonaje mawazo yenu mkayafikisha kwa mabalozi wa Tanzania waliopo katika nchi mlizopo!?..
   
 9. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Hahahahaa!... Mi masikini ndugu yangu, sijawahi kwenda nje na sizijui gharama za ndege!
  Suala la namba nimelitoa hapa (yasome vizuri hayo uliyoyaandika)..
  $5,840 is approximately to 8,760,000Tsh.. Kwa trip ya kusikiliza maoni ya watz wa USA....
  Kuna waTZ wengine wako Dubai, China, India, Uingereza, Finland, German, France, Nigeria, South Africa, Congo, Malaysia, Mexico.... Etc etc etc nao inabidi wakasikilizwe (unless unaamini mawazo ya nyie mliopo USA ndio yanayotakiwa)...

  Nimeipenda sentensi yako uliyoyaandika 'sisi na watanzania wengine'.... U sound like ur not an ordinary Tanzanian...
   
 10. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  You got him by the balls
   
 11. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu umesahau wanakula pediem ya hali ya juu sana nafikiri ni kama $400-500 kwa siku kila wakitoka nje ya nchi. Hivyo mjumuishe kwenye mahesabu
   
 12. t

  tambarare Senior Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui kama mnaelewa ccm hawataki hayo maendeleo mnayoyawazia wao wanataka kutawala milele no matter what? ndio maaana kwa mfano katiba watu wanataka mpya lakini wao wanataka kuweka vidaka hii iliyopo ambayo inatufanya tuwe maskini wa kutupwa-katiba haina uwajibikaji-mwinyi mara mbili mabomu yamelipuka bado yupo madarakani haoni soni kwa watanzania
   
 13. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamakweli sasa tuna taniana jamani viongozi wetu wafwate mawazo nje ya nchi jamani acheni utani na fedha za walipa kodi. Hivi ni mawazo mangapi yaliyotolewa hapa hapa nyumbani yameshindwa kutekelezwa au kufwatiliwa yaka saidia nchi yetu. ya nje ndio yatakuwa ya maana sana. embu tuangalie kitu kimoja tu DOWANS kuna wanasheria wangapi walikuwa wanaomba wasaidie/ wahusishwe ili wasaidie kutetea hiyo tunzo lakini awajashirikishwa mpaka leo atujui nini kinaendelea jamani ACHA TENA NA SEMA ACHENI FEDHA ZA WALIPA KODI inaniuma sana kwani kwenye mshahara wangu tu nakatwa fedha nyingi tu watu wachache wanakula jamani hii nchi niyetu sote na sie tunayo mawazo hapa hapa nyumbani. Tuna washukuru sana wenzetu WATANZANIA WOTE walioko nje na tuna amini mna michango ya maana sana na kwa kuwa nyie mko nje na mnaona maendeleo ya wenzetu lakini je unafikiri kama wanashindwa kupokea mawazo ya watanzania walioko nyumbani watawezakupokea yakwenu?
   
 14. n

  nndondo JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na umuhimu wa kuwashirikisha watanzania wa kwenye diaspora kwenye shughuli za maendeleo lakini nakataa dhana ya kuwachukulia kama wadau wakuu katika shughuli hizo na kuitisha mkakati maalumu zaidi ya hii iliyopo. Kwanza tukubaliane kwamba si kweli kwamba kama ilivyo Nigeria ama Kenya, kuna mchango mkubwa wa kiuchumu unaotokana na kundi hilo, michango yao ni ya kawaida tu ya kijamii kwa familia zao kwa hiyo ni kundi la kawaida tu. Sikubaliani na kuliangalia kundi hili kama vile liko juu ya watanzania wengine walioko hapa, kwa nini tuwe na ujumbe maalumu kwao? tayari kuna diaspora meetings zinazoelekea huko ukiwemo mkutano wa mei mwaka huu huko london, mwaka jana kulikua na mikutano dakota marekani na kwingine, pia kuna ofisi zetu za balozi CCM wamekua wakionekana kuwa na matawi nchi hizi na zile. Ni yale yale, serikali itufanyie hili na itufanyie lile, sisi huku nyumbani tuko busy sana, ni kichekesho kusema eti watu waombe wachangiwe nauli kwa nini wao wasiji organize kualika washiriki wa kuwapa habari za huku nyumbani? siku hizi new media inatoa nafasi ya kuwa karibu sana toka continent moja hadi nyingine, mstsimbe na TPN wamekua na mkakati wa hao watanzania walioko nje, jamani hayo maendeleo hawawezi kuchangia mpaka watambulike kwamba wao wako nje? mimi sikubaliani na hizi attitude za kikoloni mamboleo narudia tena kusema kuna opportunities nyingi tu already za kuwawezesha kushiriki katika mikakati hii kama wanataka, tumeona watu kama wakina mwanakijiji wakiwa very active kwenye harakati mbali mbali japo wako nje pasipo kulilia kutambulika ama kutafutwa kama kundi maalumu, hizi ni cheap talks I am not interested na tuzipige vita, ndio maana nilikutana nao wengine waliorudi wakiandaa mkakati wakutaka haki ya kupatiwa kiti bungeni manake wao wako nje, crap na ushamba tu
   
Loading...