Viongozi wa tanzania ni wezi wasio na aibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa tanzania ni wezi wasio na aibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chagula, Jan 1, 2011.

 1. C

  Chagula Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :yuck: Tangu 30.10.2010 siku ambayo watanzania walipiga kura mimi nimekuwa nafatilia matokeo na hoja mbalimbali kuhusu huo uchaguzi wa 2010.

  Chama tawala cha CCM, kilionyesha dhahiri kuwa wananchi wamechoka nacho na wanataka mabadiliko. Si kwa sababu CCM imezeeka la, ni kwa sababu CCM imejaa viongozi wabovu, wezi, mafisadi na laghai wanaojali ubinafsi na familia zao badala ya kujali TAIFA lililowaamini na kuwapa uongozi.

  Chama tawala cha CCM chini ya mwenyekiti wake Kikwete na katibu wake Makamba, kimeonyesha wazi kuwa ni chama cha ufisadi na ulaghai tu.

  Angalia mambo yoote na tume zoote na uchunguzi woote wa kuhusu ufisadi, zimefikia wapi? EPA, Benki Kuu, Richmond, Reli ya kati, bandali ya Dar na site za kuhifadhia makontena yaliyoshushwa kutoka melini meli, ni serikali au watu binafsi wanaoendesha biashara hii baada ya kuliibia taifa? Ugavi wa umeme na makampuni mbalimbali ya kukodishwa kutoa umeme kwa vile TANESCO haitoshelezi ugavi wa umeme, mikataba bandia ya ujenzi wa barabara n.k.
  Mawaziri, makatibu wakuu, n.k. wooote kila mtu ana kamradi kake ka kuneemesha familia yake na yeye mwenyewe. Tangu lini nchi ikaruhusu wachimba madini waje wachimbe halafu taifa linalomilki ardhi na madini lipewe asilimia 2 tu? Kwa nini na namna gani BM ana mkataba wa miaka 100 kwenye migodi ya madini?Tangu lini taifa likategemea dolla 50 wanazolipa wageni wakiingia nchini kwa kupitia uwanja wa ndege? Tangu lini mtoto wa waziri au rais akawa mfanyabiashara maalum kiasi kwamba akapewa tenda ya kugawa vifaa vya ofisi katika maofisi ya serikali? Tangu lini taifa likatrngeneza bujeti yake kwa kutegemea vijisenti kutoka kwa wafadhili? Tangu lini mke wa waziri au rais akawa na mamlaka bila elimu kamili ya kupokea, kugawa na kumiliki misaada yoote ya kutoka kwa wafadhili na kudai eti zinatumika kusaidia watoto yatima au kujenga mashule n.k.Tangu lini kiongozi akawa na nyumba na mashamba na viwanja sehemu mbalimbali za jiji la Dar na sehemu mbalimbali nchini, kwa mfano shule ya mke wa BM iliyoko wilaya ya bagamoyo. Alipata wapi pesa za kujenga shule kama hiyo?
  Kwa nini viongozi wa nchi ndiyo wao wenyewe ambao ni wafanyabiashara? Kwa nini viongozi wa nchi ndio wao wenyewe wenye mashamba makubwa kuliko hata vijiji?
  Haya yote pamoja na mikataba mbalimbali ya binafsi ya kutumia majina ya watu wengine, nchi inaliwa waziwazi, wananchi wanaendelea kukonda.

  Nawaomba wanasiasa na viongozi wote wa Tanzania, wajiangalie kwenye kioo na kujiuliza "JE HII NI HAKI"?, JE HII NDIYO MAANA YA OPEN MARKET ALIYOTANGAZA RAIS MSTAAFU MWINYI? JE HIVI NDIVYO NCHI YENYE DEMOKRASIA INAVYOONGOZWA? JE NI LINI TANZANIA ITAJITEGEMEA KIUCHUMI KAMA BOTSWANA BILA KUTEGEMEA MISAADA KUTOKA KWA WAFADHILI? JE NI LINI VIONGOZI WA TANZANIA WATAACHA KUMEGA PESA ZA MISAADA WANAZOLETEWA ILI ZISAIDIE KWENYE MIRADI YA WANANCHI?

  Namuomba Mwenyekiti wa CCM na katibu wake wajiulize, ni kwa vipi nchi itaepukana na rushwa na vitendo vya ufisadi? Ni kwa njia ipi Tanzania itaweza kuendelea na kujitegemea kutokana na rasrimali zake badala ya kuombaomba huko Ulaya na Asia?
   
Loading...