Viongozi wa Tanzania hawaeleweki dhamira yao ya utumishi imesimamia maslahi ya Taifa au imesimamia maslahi ya mabosi wao

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Tanzania yetu ya watanzania ina Watanzania wenzetu ambao ni viongozi wa ajabu Sana katika utendaji wao wa shughuli za kila siku.

Huwezi kuwajua misimamo yao imesimamia wapi Wala ukitazama vision yao kwa Taifa ni kinyume na matarajio na matakwa yao katika utumishi wao.

Leo unaweza kuwa na KATIBU MKUU wa Wizara wenye mtazamo tofauti anapokuwa Waziri na anapokuwa Kiongozi Mkuu.

Pamoja na kuwa wapo chini ya mtu lakini legacy yao imesimamia nini, kwanini wanakuwa dynamic kwa kubadilika kutokana na upepo unapoelekea.

Iko wapi dhima yao katika utendaji uliotukuka kwa kushauri Mambo yenye tija kwa Taifa na kuyasimamia,hata Kama watabaki pekee yao.

Mathalani mzee Edwin Mtei alitofautiana na Mwalimu Nyerere juu ya mfumo wa kiuchumi ambao baada ya kukinzana kimsimamo mzee huyu aliachia ngazi kuonyesha msimamo wake juu ya jambo fulani kwa Taifa, leo viongozi wetu wanashindwa nini.

Mtizame Prof Assad, alisimamia alichokiamini bila kulamba nyayo za mkubwa, madhara yake ni kuondolewa kwa zengwe bila kuzingatia sheria ina kinzana na utashi wa mkubwa.

Hawaeleweki dhamira yao ya utumishi imesimamia maslahi ya Taifa au imesimamia msimamo na maslahi ya mabosi wao.

Hi ina kiathiri chama chao kwa kuwa madhumuni ya chama chao ni kushika dola tu, Hawana dira ya Taifa yenye malengo sawia japokuwa wote wapo ndani ya serikali moja.

Kwa mantiki hiyo leo ukimuuliza makamu wa rais nini dira yake katika utumishi wa umma akiwa amehudumu kwenye serikali tatu ndani ya chama kimoja sidhani Kama atakuwa na jibu sahihi la swali hilo,kwa kuwa ameshindwa kusimamia na kushawishi serikali zote tatu kusimamia kile alicho kitafiti kwa hoja endelevu.

Amekuwa na tabia ya camouflage ya kubadilika Kama kinyonga kujifichia kwenye kichaka cha kuchumia tumbo lake bila kujali matakwa ya Taifa kwa wakati ule.

Akiwa mshauri wa rais Kikwete waliasisi wazo la kilimo kwanza kuelekea mapinduzi ya kijani,ambayo yangekuwa chachu kwa serikali ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa viwanda na soko huria lenye tija.

Bila kujali changamoto walizopitia kukamilisha malengo ya mradi huo uliogharimu fedha nyingi za walipa Kodi akiwa ndani ya serikali nyingine akiwa waziri wa fedha hakujali upotevu wa mamilioni ya kilimo kwanza kupotea bila implementation,wakaibuka na msongo mwingine wa serikali ya viwanda na uchumi wa kati.

Bila kuzingatia maarifa ya elimu yake data za kukuwa kwa uchumi na kufikia uchumi wa kati zikapikwa kinyume na uhalisia wenyewe. Tanzania ikavuka mstari wa umaskini wa kutupwa kwa muda mfupi kabla ya muda ulio tarajiwa (breakeven). Yote yakitekelezeka kwa muda mfupi chini ya uratibu wa ofisi yake.

Leo akiwa makamu wa rais anakuja na MPANGO wa kutokomeza umaskini kwa Watanzania zaidi ya million 14 ambao ana kiri kuwa wapo chini ya mstari wa umaskini wa kutupwa.

Swali ikiwa tupo kwenye uchumi wa kati,namba hiyo ya Watanzania maskini walio chini ya mstari wa umaskini wa kutupwa inatoka wapi.

Ikiwa uchumi wetu kwa takwimu zake akiwa bungeni mwaka 2020 kuwa umefikia 7%,lakini leo upo 4.2% anaweza kutueleza nani mkweli kati ya MPANGO waziri wa fedha na MPANGO makamu wa Rais.

Ukitafakari mnyumbuliko wa utendaji kazi wake na scenario zake utaona jinsi gani nchi yetu inavyogeuzwa shamba la Bibi na kikundi kidogo kilichojaa uroho wa madaraka.

Lakini inaonyesha jinsi gani ombwe la uongozi katika nchi yetu linavyo chukua Kasi ya ukuaji kila kukicha. Hakuna mzalendo wa kweli kwa Taifa hili Wala hakuna mwenye uchungu na fedha za wananchi.

Kuna haja ya kusimamia maarifa yetu kwa kutanguliza maslahi mapana ya Taifa na hofu ya Mungu kuliko kuifanya elimu yetu ionekane haizalishi wasomi wenye maarifa. Wasomi always wako smart,tukiendeleza ukanjanja huu kizazi kijacho kitarithi nini kutoka kizazi hiki.

Watch out,saa ya ukombozi ni sasa.
 
Aiseee, umeipanua mno hoja yako na kuichanganyachanganya sana, hadi inakuwa vigumu msisitizo wake ni juu ya nini hasa!

Kama huamini na ukilalamika, nitainyambua uone ulivyoichanganya na kuiondolea lengo mahsusi; ambalo hata mimi ningekuunga mkono kwa kulisemea.
 
Back
Top Bottom