Viongozi wa tahliso wajitambulisha kupitia vyombo vya habari. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa tahliso wajitambulisha kupitia vyombo vya habari.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Vitendo, Jan 23, 2010.

 1. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  VIONGOZI WA TAHLISO WAJITAMBULISHA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
  Wednesday, 20 January 2010

  Mr.Lawrence Mwantimwa Rais wa Tumaini University Dar es salaam,wa katikati ni Mr.Noel Issaya Katongo Rais wa Moshi University pia ni Mwenyekiti wa TAHLISO wa mwisho ni Mr.Prosper George Ngoro katibu mkuu TA

  Lengo ni kujitambuklisha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na jamii ili iweze kutufahamu,kwa hapo awali ulikuwa ukisema TAHLISO watu wanakuwa hawajui,kwa hivyo TAHLISO(Tanzania Higher Learning Institution Organization) ilikuwa imepoteza picha na mwelekeo katika ya jiji na sisi kwa kuliona hilo kama uongozi mpya ambao unajumuisha Maraisi wa vyuo mbali mbali Nchini.

  Tumeamua kujitambulisha kwa jamii alisema kuwa wanafunzi wa Elimu ya juu tumekuwa tukitoa malalamiko sana kwa Serikali pasipo kujiuliza sisi wenyewe tunafanya nini kuisaidia jamii,lengo letu ni kuweza kurudisha mahusiano kati ya jamii na vyuo vikuu kwa sasa hivi jamii inaonekana kutotambua hasa mchango wetu kama wanafunzi wa vyuo vikuu sababu hatukuweza kufanya shughuli za kijamii kwa kiasi kikubwa.

  Kwa hiyo kama TAHLISO tumekuja na Program mbali mbali ambazo zitahusisha jamii yetu katika maendeleo,kwa mfano kwa kuwakusanya Madaktari kutoka Vyuo mbali mbali na kwenda kushiriki katika kutoa elimu ya afya kwa jamii hasa vijijini,pia kuna Vyuo vya sheria kwa nini kama wanafunzi wa sheria ule muda wa likizo zetu tusijikusanye kwa pamoja na kuzunguka vijijini kuongea na jamii juu ya masuala ya kisheria,ila kwa sasa tunakabiliwa na changamoto katika masuala ya mazingira pia tunahitaji kuiyelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira,kama TAHLISO tumeamua kushiriki katika upandaji miti na zoezi hilo litafanyika Tarehe 22 mwezi wa pili huko mkoani Kilimanjaro, Project itakayofuata ni Masuala ya Afya ambayo itakusanya Wanafunzi wote wa Vyuo vya Udaktari kushiriki project hiyo ya kutoa elimu ya Afya kwa jamii ambayo tutaanzia na mkoa wa Lindi mwezi July,pia tunafikiria kwenda Hospitali kama Mwananyamala kutoa huduma kwa wagonjwa na kusafisha Mazingira yanayozunguka eneo hilo,hayo ndio machache ambayo tunaona yanaweza kutusogeza karibu na jamii yetu kama uongozi mpya wa TAHLISO kwa mwaka huu.

  Shukrani kwa Serikali kutusaidia katika Nyanja mbali mbali tunaelewa kwamba tunachangamoto nyingi katika Nyanja ya elimu,Mh.Rais kusaidiana na serikali waliweza kuanzisha Chuo cha Dodoma University mpaka miaka ya baadaye Tanzania itakuwa imeboreka katika kutoa elimu ya juu pia tumshukuru kwa kutupatia Mh.Waziri mkuu kushiriki nasi katika Nyanja mbali mbali za kijamii.
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  The TAHLISO we currently know is that of traitors; they are CCM fanatics and treacherous against the poor peasants, pastoralists and workers.
  Why not going to Loliondo to help defending the rights of evicted persons?!
  Traitors are always hypocrites. We know them!
   
Loading...