Viongozi wa siasa msichezee maisha ya watu kwa faida zenu

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Hili la wabunge wa viti maalumu kutinga katika viunga vya Bunge na kula kiapo ni shambulio la fedhea la maisha ya watu.

Vyama vya siasa vinapaswa kujua kuwa uwepo wao si kwa maslahi yao tu, kwani wanachama waingia gharama kubwa Sana ili chama kiwe na uhai.

Ndugu zetu wameuliwa, wametekwa, wapo magerezani, wametiwa ulemavu na familia zao zimekua kwenye mashaka afu nyie mnafanya as if hakuna kilichotokea!!!

Hatukatai kuwa na juhudi za maliziano na kutengeneza mambo yaliyovurugwa. Ila ni hekima karekebisha mambo haya kwa uwazi ili kutoa fursa ya kupata uhalali wa kisiasa na kijamii na kuzuia uhuni usije ukajirudia tena.

Hii tabia ya kufikia makubaliano kimya kimya, gafla tunawaona mnakaribia mezani na kuanza kula bila kutujulisha mlichokubaliana ni usariti juu ya wanachama wenu.

Ifike mahali tuoneane huruma , sisi mnatuhamasisha kuwaunga mkono hata kwa gharama ya kifo au kuachwa walemavu afu nyie mnaenda kula fedha na kutembelea magari meusi . Huu ni usariti wa hali ya juu.

CDM msimamo wenu tunaungoja kwa hamu Katika hili lililotokea leo la wanachama wenu kuonekana kukubali ubunge viti maalumu na kula kiapo bungeni leo.

Iwe gizani au mchana tutawapinga na kuwakataa kwa dhambi hii. Hujuma hii itakua ni dhambi kubwa kuliko ata hao mnaosema waliharibu uchaguzi na kupora ushindi.

Hatutawasamehe na tutawashitaki kwenye mahakama ya mbinguni muazibiwe ipaswavyo . Hamtakuwa salama , roho zenu katu hazitopata amani, na umauti hautoondoka katika vizazi vyenu na roho ya usariti haitokoma kwenye vizazi vyenu vyote.

Msituone wananchi wa taifa ili Kama misukule mnaoweza kutugeuza na kutuchezea kadri mnavyopenda kwa kuendekeza mambo ya gizani na ushetani.

Yakiweko makubaliano na maliziano yafanyeni kwa uwazi. Tujue nani yuko nyuma yake kwa madhumuni yapi na wapi na yanapewa baraka na wananchi wapi.
 
Mtakoma ambao mnaweka rehani vichwa vyenu kisa mwanasiasa fulani.

Wengine tuliishashtuka,tunahangaika na maisha yetu.
 
Waliouliwa na kutekwa hawakufanya kosa lolote?

"Kaa ukijua hakuna binadamu anayeweza kujadili masilahi yako kwanza pasipo kujadili masilahi yake kwanza"
 
Mkuu bado kitambo kidogo Tutajua magugu na ngano... magugu yamesepa tiali...
 
Kuna mambo ya kuweka wazi, kuna mambo ya siri. Muhimu ni kwa maslahi mapana ya taifa letu. Siku nyingine ukiambiwa andamana, usishangilie kwa kukimbilia barabarani.
 
Mliapa kua hamtaitambua serikali iliyoingia madarakani kwa janja janja...iki mlichokifanya leo mbona hatuwaelewi au mmeshanunuliwa?!
 
Halima Mdee na genge lake lililohongwa 500m kila mmoja pamoja na wahongaji wanapaswa kufutika katika uso huu wa dunia.
 
Exactly , mkuu uko sahihi yaani hapa bila kupepesa macho kwanza Chadema wawafukuze wote hao , ingawa Ndugai atawalinda kwa maagizo ya Mhutu lakini chama kitakuwa kimelinda legacy yake . Pili taarifa ipelekwe kule Mhutu anakolenga kupata fedha kwa kutimiza masharti ya kuundwa kwa kamati za PAC na LAAC ili Jiwe akose hizo hela , uzuri hata wenyewe wanafuatilia sana .
 
Mleta mada.
Kwanini mnakuwa wagumu kuelewa somo halafu badala yake mnateseka bure.
Inarudiwa: Siasa ni ajira. Mwanasiasa anafanya siasa kwanza kwa maslahi yake na familia yake. Hutaki kuamini hili basi hakikisha una mganga mzuri wa stress.
 
Pamoja na hayo yote ila bado watu watawatetea chadema na kusahau hayo yote na kuendelea kuamini kuwa chadema kuwa ndio mtetezi wao.

Tuliojiweka pembeni na hizi siasa tunajionea mengi kweli na hizi siasa za bongo.
 
Back
Top Bottom