Viongozi wa Serikali ya CCM hawapati thawabu wala Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,934
3,805
Ni lazima wajitokeze watubu na kuwaomba radhi waTanzania walio wengi kutokana na kadhia ya Uchaguzi mkuu uliopita,hakuna asiejua kilichotokea.
Watafanya mengi mazuri ya kufurahisha lakini yatakuwa hayana baraka ,hivi hela ya wizi inatenda Jema mbele ya Mwenyezi Mungu?

Wanatia huruma sana viongozi wa nchi hii,wanajitahidi kufanya makubwa lakini mwisho wa siku waliyoyakusudia yanaporomoka ,wapo madarakani kwa kura za wizi ? Hivi watu hawa hawaamini kama Mwenyezi Mungu yupo na anawaona?

Ili mikakati yao ifanikiwe na iwe na baraka na yenye manufaa basi wajitokeze na kutomba adhi wananchi kwa ujumla na kukiri kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu hakitajirudia tena,vinginevyo wanayoyafanya ni kujaza maji kwenye pakacha ,mikataba mingi mwisho wake watakuja kuona mikataba yote imekuwa hasara.

Viongozi wa serikali jitokezeni mtubu kwa Mwenyezi Mungu vinginevyo mnazidi kuingia kwenye matatizo na Mwenyezi Mungu. Msione mnaweka saini kwenye mikataba na mikakati ya Maendeleo mkaona ndio mafaniki,Ya Mwenyezi Mungu hamuyawezi ni mazito.
 
Hii tabia ya kuhusisha dini na kumuhusisha Mungu na siasa za nchi inazidi kutia fora. Hakuna nchi duniani iloyoendelea kwa kutegemea miujiza au wengine mnachoita kudra
 
Nchi yetu tangu imetaifisha mali za watu na kupora shule za taasisi za dini ilikwishajitenga na Mungu. Dhuluma ni jambo linalomkasirisha sana Mungu, soma maandiko kwa uraisi wa rejea.
 
Angalia nchi walizokuletea dini na maasi waliyofanya lakini leo nd wamebarikiwa kila kitu wanakuongoza kiuchumi na kuwapa mikopo na wana kila kitu kukuzidi nchi uchwara za Afrika.
 
Back
Top Bottom