Viongozi wa serikali nendeni nyumba za ibada kusali na kuondoka matamko ya kiserikali upo utaratibu wake rasmi msiige tabia ngeni zisizo faa..

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,362
5,808
Kwanza kabisa niwaombe msiwe waongeaji sana hii itaanza kushusha heshima yenu maana kupitia kuongea sana ndipo watu hupima busara zenu na kila neno litokalo vinywani mwenu hubebwa kama hoja na yaweza zua mjadala kama sio kuchora picha halisi ya mwenendo wa serikali hivyo vinywa vyenu mjitahidi kuvipunguzia maneno na hasa pale pasipo ulazima

Rais aliye pita alikuwa anaongea sana tena sana hadi anapitiliza kitu kilicho fanya ajianike sana madhaifu yake na ya serikali kwa ujumla maneno yake ya hovyo hovyo mengi yaliichora vyema tabia yake .

Naona ndugu Philip Mpango anataka kuendeleza tabia za aliye kuwa rais wa tanzania JPM kutumia madhabahu kama sehemu ya kutolea matamko ya serikali

Naomba nishauri tu achaneni na hii kitu nendeni kwenye nyumba za ibada kama waumin wengine na endapo mtapewa nafasi za upendeleo kuongea ili kutambua uwepo wenu niwaombe sana busara ziwaongoze msipende sana kutumia mda huo kuanza hotuba za kiserikali na maneno meengi.

Msiige tabia hii iliyo kuwa ya mtangulizi wenu maana alipenda sana kutumia madhabahu takatifu kujibu vijembe kutoa matamko nk. haikuwa njema sana hii kwa sababu mna mda mwingi sana wa kutoa matamko ya kiserikali nje ya nyumba za ibada

Niwaombe sana.
 
Nyumba za ibada zitumike kumwabudu Mungu tuu.siasa Zina mahali pake.
 
Back
Top Bottom