Viongozi wa Serikali na Wanachuo wa Chuo Kikuu Bugando wafukuzwa Chuo

Mar 12, 2009
85
108
Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Elimu, M/kiti wa Tume ya Uchaguzi, Mbunge, Spika Mstaafu na Wanachuo wengine wanne kutoka CHUO KIKUU CHA BUGANDO wafukuzwa chuo!

Hii ni kutokana na Viongozi hawa kuwa wasumbufu kwa mkuu wa chuo kuwasilisha madai ya wanachuo waliyotumwa kutoka katika vikao rasmi vya kisheria.

Madai hayo yalikuwa ni:-
1. Kulipishwa laki 2 ya matibabu wakati wanatibiwa na Mfuko wa bima ya Afya NHIF kwa sh 50400/- hivyo chenji ya 149600 (ambayo kwa idadi ya wanachuo wote ni takribani Millioni 500 kwa mwaka ) inabaki na haijulikani inaenda wapi.

2. Madai ya chuo kupandisha ada kutoka 3.7m kwenda 4.3m bila ruhusa ya TCU.

3. Kupigwa penalti ya laki 2 (inakadiriwa kuwa milioni 300 kwa mwaka kutokana na idadi ya wanachuo wanaochelewa kulipa ada) kwa wanachuo maskini wanaoshindwa kulipa ada kwa wakati.

4. Kutozwa michango ya nyongeza Tsh 100,000 kila muhula.

FB_IMG_1528308150632.jpg


Habari zaidi, soma=>Unyonyaji na unyanyasaji ndani ya chuo kikuu Bugando
 
Mmmh!!!! Kazi kwelikweli, cha kufanya ni kuangalia sheria, sheria inasemaje!!!? Waende mahakamani.
 
Mnafukuza wanafunzi bila sababu za msingi mnatengeneza nini mtaani,kama si majambazi na machangu.yani saiz wema umekua uadui na uadui kuwa wema .nyie wanafunzi mliofukuzwa mkatumie vyema elimu mlioipata japo hamjamaliza kutatua maisha yenu, karibuni mtaani tupambane na hali zetu.
 
UKWELI UTAJULIKANA TUJIPE MUDA. WANAFUNZI WAKIISHA FUKUZWA NDO HUWA WANABADILIKA NA KUJIFANYA WALIKUWA WANATETEA KITUFLAN BUT KWATULIO NA UZOWEFU KUNAKITU HAPO NA SIO BURE, TUWENA SUBIRA TUJUE UKWELI.
 
nilijua utumbuaji wa pesa za wanafunzi ni chuo ninachosoma mm tu kumbe ni kila chuo alafu Dean of students ndo mnafiki akishirikia na mwanasheria wa chuo hawa ndo wakuwachoma moto
 
Back
Top Bottom