Viongozi wa Serikali mnaopenda kufanya maamuzi ya kujijenga binafsi kisiasa muache. Sikubaliani na hili tamko la RC Mtaka

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,213
22,273
RC Mtaka ni kiongozi mzuri lakini naona huwa anavuka kabisa mipaka labda kwa kujua au kutokujua ila mwishoni huonekana ni kama vile maamuzi binafsi ya kujijenga kisiasa. Mara kadhaa ameshawahi kuleta misuguano hadi na waziri wa elimu kutokana na maamuzi yake ambayo huwa hataki kabisa yapingwe.

Hii sio sawa kwasababu serikali haifanyi kazi kwa kufuata busara za mtu bali sheria zilizowekwa. Hata kama ni busara lazima iendane na sheria.

Leo nimeona tena RC akisema hata wanafunzi wa mkoa wake wasio na uniforms wakaripoti shuleni. Huu uamuzi unashangiliwa sana na wananchi wa huo mkoa lakini uko kinyume kabisa na utaratibu wa serikali. Kama serikali inatoa elimu bure iweje wazazi/walezi washindwe hata kununua sare za shule? Kwanini RC anataka kuondoa wajibu wa mzazi/mlezi na kuibebesha Serikali lawama?

Mimi naona ni kuwaletea tu matatizo watendaji wanaohusika na elimu kwa huu uamuzi wake wa kisiasa. RC Mtaka anachofanya ni kujijenga yeye binafsi huku akipandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali. Iko wazi kuna watendaji wanaweza kuwakataa wanafunzi watakaoripoti bila sare na matokeo yako ukawa tu mvurugano kati ya wananchi na serikali. Halafu huu uamuzi ni sawa na kurudi nyuma kabisa kimaendeleo.

20221217_163437.jpg
 
Nakumbuka nili-report form 6 nikakutana na jamaa hana uniform na alikaa km mwezi.
Badae akapewa suruali nyeusi na jamaa mmoja kutoka Arusha.
Mtaka yuko sahihi; pia kumpinga waziri alikua sahihi. Mtaka kwenye swala la elimu ndo mtu pekee sahihi anayewasemea wasio na sauti
 
Si mmekuwa mkimsifu na ameshalewa sifa punde atakuwa km Makonda maana Makonda alijiona yuko juu ya mawaziri alikuwa hawaheshimu. Mgema akisifiwa... Anafanya mambo ambayo hata rais hawezi kuyafanya maana rais hawezi kutoa kauli km hiyo ni mlevi tu anaweza kufanya hivyo.
 
Nakumbuka nili-report form 6 nikakutana na jamaa hana uniform na alikaa km mwezi.
Badae akapewa suruali nyeusi na jamaa mmoja kutoka Arusha.
Mtaka yuko sahihi; pia kumpinga waziri alikua sahihi. Mtaka kwenye swala la elimu ndo mtu pekee sahihi anayewasemea wasio na sauti
mlevi mwenzake, huoni hata aibu
 
RC Mtaka ni kiongozi mzuri lakini naona huwa anavuka kabisa mipaka labda kwa kujua au kutokujua ila mwishoni huonekana ni kama vile maamuzi binafsi ya kujijenga kisiasa. Mara kadhaa ameshawahi kuleta misuguano hadi na waziri wa elimu kutokana na maamuzi yake ambayo huwa hataki kabisa yapingwe. Hii sio sawa kwasababu serikali haifanyi kazi kwa kufuata busara za mtu bali sheria zilizowekwa. Hata kama ni busara lazima iendane na sheria.

Leo nimeona tena RC akisema hata wanafunzi wa mkoa wake wasio na uniforms wakaripoti shuleni. Huu uamuzi unashangiliwa sana na wananchi wa huo mkoa lakini uko kinyume kabisa na utaratibu wa serikali. Kama serikali inatoa elimu bure iweje wazazi/walezi washindwe hata kununua sare za shule? Kwanini RC anataka kuondoa wajibu wa mzazi/mlezi na kuibebesha serikali lawama? Mimi naona ni kuwaletea tu matatizo watendaji wanaohusika na elimu kwa huu uamuzi wake wa kisiasa. RC Mtaka anachofanya ni kujijenga yeye binafsi huku akipandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali. Iko wazi kuna watendaji wanaweza kuwakataa wanafunzi watakaoripoti bila sare na matokeo yako ukawa tu mvurugano kati ya wananchi na serikali. Halafu huu uamuzi ni sawa na kurudi nyuma kabisa kimaendeleo.
Ulaya hawana uniform kabisa na hairuhusiwi kabisa hata baadhi ya nchi graduation ni marufuku maana ni ujinga. Kichoangaliwa ni competency ya mhusika.
 
Kama serikali inatoa elimu bure iweje wazazi/walezi washindwe hata kununua sare za shule?
Usiwalinganishe wananchi na wewe mwenye uwezo wa kukaa nyuma ya keyboard, kuna watu hawajui hata chupi inafananaje, hawajui hata sabuni ipoje, ingekuwa busara umwambie Mtaka kuwa akishauri Chama kiboreshe maisha ya watanzania waweze kumudu gharama za maisha, pengo kati ya masikini na matajiri ni nene mno hivi sasa
 
mbona nyie ccm mnapoenda kuangalia miradi ya serikali mnaenda kichama na maguo yenu
 
Back
Top Bottom