Uchaguzi 2020 Viongozi wa serikali lindeni ndimi zenu, kauli hizi zinalivuruga Taifa

Huyo Mkuu wa Mkoa kwanza awahimize watawala wetu watende HAKI katika utendaji wake

Mithali 34:14
Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote

Pia imenenwa kuwa AMANI NI TUNDA LA HAKI
 
Wacha watu watoe ya moyoni. Uzuri wa majukwaa ya kisiasa mtu akishika maiki lazima rangiyake halisi utaijuatu
 
"Unapokwenda kulinda kura aga kabisa nyumbani kwako, uhakikishe familia yako umeiacha vizuri kwa maana utakutana na wenye kazi yao ya kulinda kura na unanaweza usirudi nyumbani ukaenda gerezani au ukarudi mlemavu"

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brg. Mwangela.
Aliwekwa makusudi kutisha watu, lakini na yeye anaweza akaishia kutoiona familia yake huko ICC! Ikitokea watu wakachinjana hapo Mbeya, hawezi kuchomoa
 
Naam ujumbe muruwa kabisa huo hasa kwa mtu muelewa
Hali ya maisha awamu hii imekuwa ngumu kuliko awamu zote.vijana wamesoma hawana ajira,wanaona heri kufa akitafuta haki maana hana cha kupoteza,nyumbani hapakaliki.
 
Aliwekwa makusudi kutisha watu, lkn na yeye anaweza akaishia kutoiona familia yake huko ICC!
Inaweza hata isiwe ICC, maana mlenga hulengwa.

Kuna kitu PoliCCMtz wanajisahaulisha, kwenye vurugu, hakuna aliyesalama. Police ataua raia, na raia ataua police. Police hawez kuchoma nyumb wala gari la mtu, ila raia watachoma vituo vya polis, magari na ofis nying za serikali.

Yeyote atayekufa hapo, ni hasara kwake, ila faida kwa taifa maana utakuwa mwanzo wa utawala bora.
 
Wafuasi wa Chadema mmeshaanza kutia huruma, Kila siku mnaleta uzi wa kulalamika subirie tumalize mabishano maana kura humaliza mabishano

sent from HUAWEI
 
Aisee...tumeanza kutishana sasa...consequences za haya matamshi zitaonekana mambo yakiharibika baada ya uchaguzi
Hakuna kutishana hapa! Mkuu wa mkoa anatoa maelekezo wala hatoi vitisho. Kuna kazi za aina mbili hapa lazima tuzielewe. Moja ,kazi ya kupiga kura.. Mbili, kazi ya kulinda kura. Raia kazi yetu ni kupiga kura wale wa vyombo vya dola ni kulinda kura
 
Mgombea wa Chadema ameshakata tiketi ya kurudi kwao ubeligiji baada ya kuona Watanzania wamamkataa

Ila anahamasisha vijana waandamane

Ni ajabu yaani, niandamane kwa ajili ya mtu anayeishi ubeligiji yeye familia ipo inakula bata. Ati mimi nianze kumpigania mtu ambaye hata nikipigiwa kirungu na polisi hawezi kunisaidia kwa lolote
 
"Unapokwenda kulinda kura aga kabisa nyumbani kwako, uhakikishe familia yako umeiacha vizuri kwa maana utakutana na wenye kazi yao ya kulinda kura na unanaweza usirudi nyumbani ukaenda gerezani au ukarudi mlemavu"

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brg. Mwangela.
Aliye jitolea kajitolea hata umtengenezee hofu vipi hata rudi nyuma, ila viongozi walipaswa kunena busara sii mbavu sana.
 
Uongozi wa mabavu ndo anakionyesha tu alafu yeye haruhusiwi kwenye Mambo ya uchaguzi na kazi ya ulinzi awaache polisi Sasa hivi hizo kauli za mabavu zinaleta chuki na Kura ni Siri ya mtu.
 
"Unapokwenda kulinda kura aga kabisa nyumbani kwako, uhakikishe familia yako umeiacha vizuri kwa maana utakutana na wenye kazi yao ya kulinda kura na unanaweza usirudi nyumbani ukaenda gerezani au ukarudi mlemavu"

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brg. Mwangela.
Huo ndiyo ukweli sasa hapo kuna ubaya gani? Kweli ukijifanya kwenda kulinda kura utakutana na walinda kura halisi. Hivyo anawashauri waage kabisa majumbani kwao kwa kuwa hawatarudi majumbani mwao au wakarudi walemavu.
 
Raia kazi yetu ni kulinda kura wale wa vyombo vya dola ni kulinda kura
Kwa hiyo wote tuna kazi moja? Unaona ulivyojiaibisha? Maana kitokacho roho ndicho kilichoijaza roho! Unajidai kupotezea lakini unajua kabisa raia ana wajibu wa kulinda kura yake!
 
Aliwekwa makusudi kutisha watu, lakini na yeye anaweza akaishia kutoiona familia yake huko ICC!
Nakushauri kama unaweza jitokeze hiyo tarehe ya kupigakura ukalinde kura mkuu ili tujue kama kweli na yeye ataenda ICC. Kwa nini tuishi kwa hisia badala ya hali halisi?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom