Viongozi wa ruvuma press club wajificha mafichoni kutokana na maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa ruvuma press club wajificha mafichoni kutokana na maandamano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Stephano Mango, Sep 11, 2012.

 1. S

  Stephano Mango Verified User

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na Stephano Mango, Songea.

  MGOGORO mkubwa umeibika kwa waandishi wa habari mkoani Ruvuma baada ya Viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoani humo kutoitisha maandamano na kuingia mafichoni kwa muda ili kuepusha kufanyika maandamano ya kuunga mkono maombolezo ya kifo cha mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi aliyefariki kwa kupigwa na mlipuko uliosababishwa na polisi katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.

  Mgogoro huo umewagawa waandishi wa habari na kuwafanya baadhi ya waandishi kutishia kujitoa nafasi zao za uongozi na uanachama katika umoja huo kwa sababu ya kutokuwa na imani na viongozi wao ambao wanaonekana kufanya kazi kutokana na maslahi ya kisiasa. Waandishi wa habari mkoani Ruvuma walianza kwa kushangazwa na hatua ya viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho kutowajulisha muda na njia zitakazotumika kwa maandamano hayo hadi pale kwa njia ya simu na baadhi ya waandishi wa habari ambao walishapanga waandamane saa 10.

  Jioni baada ya kujihakikishia kuwa viongozi wao wamewatosa na hawana ajenda muhimu ya kupinga maandamano hayo kwa hula. Awali baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoani humo (RPC) walijikusanya pamoja na kufuatilia matangazo ya vyombo mbali mbali vya habari yaliyokuwa yakiendelea huku wakiangalia baadhi ya picha zilizopigwa wakati na baada ya kifo cha mwandishi huyo wa habari ambaye alipatwa na mauti wakati akiwa kazini na walipanga wandamane saa 10 jioni muda ambao ndio Marehemu Mwangosi aliuawa kinyama kupigwa na bomu na Polisi.

  Katibu Msaidizi wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma , Julius Konala, alionyesha ushirikiano mkubwa kwa wanachama ambao muda wote walikuwa wanadai ratiba na hatua iliyofikiwa na viongozi wa chama hicho kwaajili ya maandamano na kuwajulisha kuwa viongozi wake hawajulikani waliko na wanapinga kufanyika kwa mnaandamano hayo.

  "Jamani mimi mtanionea tuu, Mwenyekiti na katibu wamesema kuwa UTPC imeyasimamisha maandamano yetu bila kutaja sababu," alisema Konala ambaye alichukua hatua ya kuwasiliana na viongozi wa Polisi mkoani hapa waliotaka kujua ni njia zipi zitakazotumika katika maandamano hayo ili walete askari wa kuyalinda maandamano hayo ya amani.

  Tukio hilo limewakasirisha sana viongozi wa Chama hicho na kulazimika kuitisha mkutano wa dharura kwa baadhi ya wanachama wengi wao wakiwa ni mamluki na kusababisha viongozi hao kuomba radhi kwamba wamekosa mawasiliano nao na baadhi ya wanachama wametishia kujiuzulu akiwemo Katibu msaidizi Julius Konala kwa madai kwamba chama hicho kimeingiliwa na mikono ya wanasiasa.

  "Naona mbele yangu kuna wingu kubwa na zito ambalo mwisho wake siujui, nafikiria kujiuzulu uongozi na kujitoa katika chama, " alisema Konala. Baadhi ya wadau wa habari mkoani humo wameonesha kushangazwa na ukimya wa wanahabari wa mkoa huo licha ya wanahabari wote nchini wakionekana kwenye runinga wakiandamana kupinga ukatili huo uliofanywa dhidi ya Mwandishi wa habari akiwa kazini.

  Hata hivyo Mkurugenzi wa muungano wa Vyama vya waandishi wa habari nchini UTPC Abubakar Karsan akiongea na Tanzania Daima kwa njia ya Simu amekanusha vikali kuzuia maandamano bali wao waliyabariki na ndio maana walijumuika na waandishi wengine nchini na kutoa matamko mbalimbali katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam na kwamba wao walitoa maelekezo kwa Ruvuma Press Club kuungana na Press Club zingine nchi kufanikisha maandamano ya amani ambayo yameitishwa kiuhalali.
   
 2. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,721
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Duh! Huko songea si ndio kwa nchimbi, yaani mbunge wao?
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  haswaa!
   
 4. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,378
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Hivi mtwara,lindi,tanga na Zanzibar hawa jamaa hawana waandishi wa habari?Manake sijasikia maandamano!
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Huko ndiko kwa Nchimbi na nina wasiwasi walishafikiwa tayari. Wasubiri siku litakapowafika sijuia watafanya nini.
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Duh nchimbi wanamlamba miguu huko..maadili yanapindishwa.
   
 7. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu waandishi wa habari ni juzi tu hapa niliandika juu ya uvamizi wa waziri wa mambo ya ndani kwenye maandamano ya waandishi wa habari haukuwa wa bahati mbaya,pamoja na hayo nasema baadhi ya waandishi wa habari nchii mpaka mje iheshimiwe kwa kazi yenu bado mnasafari ndefu sana,tumesikia matamko na maandamano mbalimbali kutoka pande zote za nchi TANZANIA na dunia kwa ujumla kulaaani mauaji ya kinyama ya Daud Mwangosi,kituko kikubwa ni songea waandishi walipanga maandamano viongozi wa juu wakaingia mitini na miongoni mwa viongozi hao mmoja ni katibu wa mbunge emmanuel nchimbi (waziri wa mambo ya ndani-mbunge songea mjini) ninajiuliza hivi kwa nini waandishi wa habari wasiheshimu taaluma yao badala ya kuendeleza njaaa hebu soma hii habari hapa chini

  VIONGOZI WA RUVUMA PRESS CLUB WAJIFICHA MAFICHONI KUTOKANA NA MAANDAMANO


  [​IMG]

  KATIBU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA( RUVUMA PRESS CLUB) AMBAYE PIA NA KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA SONGEA MJINI DKT EMMANUEL NCHIMBI) ANDREW CHATWANGA

  Na Stephano Mango, Songea

  MGOGORO mkubwa umeibika kwa waandishi wa habari mkoani Ruvuma baada ya Viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoani humo kutoitisha maandamano na kuingia mafichoni kwa muda ili kuepusha kufanyika maandamano ya kuunga mkono maombolezo ya kifo cha mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi aliyefariki kwa kupigwa na mlipuko uliosababishwa na polisi katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.

  Mgogoro huo umewagawa waandishi wa habari na kuwafanya baadhi ya waandishi kutishia kujitoa nafasi zao za uongozi na uanachama katika umoja huo kwa sababu ya kutokuwa na imani na viongozi wao ambao wanaonekana kufanya kazi kutokana na maslahi ya kisiasa.

  Waandishi wa habari mkoani Ruvuma walianza kwa kushangazwa na hatua ya viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho kutowajulisha muda na njia zitakazotumika kwa maandamano hayo hadi pale kwa njia ya simu na baadhi ya waandishi wa habari ambao walishapanga waandamane saa 10. Jioni baada ya kujihakikishia kuwa viongozi wao wamewatosa na hawana ajenda muhimu ya kupinga maandamano hayo kwa hula.

  Awali baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoani humo (RPC) walijikusanya pamoja na kufuatilia matangazo ya vyombo mbali mbali vya habari yaliyokuwa yakiendelea huku wakiangalia baadhi ya picha zilizopigwa wakati na baada ya kifo cha mwandishi huyo wa habari ambaye alipatwa na mauti wakati akiwa kazini na walipanga wandamane saa 10 jioni muda ambao ndio Marehemu Mwangosi aliuawa kinyama kupigwa na bomu na Polisi.

  Katibu Msaidizi wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma , Julius Konala, alionyesha ushirikiano mkubwa kwa wanachama ambao muda wote walikuwa wanadai ratiba na hatua iliyofikiwa na viongozi wa chama hicho kwaajili ya maandamano na kuwajulisha kuwa viongozi wake hawajulikani waliko na wanapinga kufanyika kwa mnaandamano hayo.

  “Jamani mimi mtanionea tuu, Mwenyekiti na katibu wamesema kuwa UTPC imeyasimamisha maandamano yetu bila kutaja sababu,” alisema Konala ambaye alichukua hatua ya kuwasiliana na viongozi wa Polisi mkoani hapa waliotaka kujua ni njia zipi zitakazotumika katika maandamano hayo ili walete askari wa kuyalinda maandamano hayo ya amani.

  Tukio hilo limewakasirisha sana viongozi wa Chama hicho na kulazimika kuitisha mkutano wa dharura kwa baadhi ya wanachama wengi wao wakiwa ni mamluki na kusababisha viongozi hao kuomba radhi kwamba wamekosa mawasiliano nao na baadhi ya wanachama wametishia kujiuzulu akiwemo Katibu msaidizi Julius Konala kwa madai kwamba chama hicho kimeingiliwa na mikono ya wanasiasa.

  “Naona mbele yangu kuna wingu kubwa na zito ambalo mwisho wake siujui, nafikiria kujiuzulu uongozi na kujitoa katika chama, “ alisema Konala.

  Baadhi ya wadau wa habari mkoani humo wameonesha kushangazwa na ukimya wa wanahabari wa mkoa huo licha ya wanahabari wote nchini wakionekana kwenye runinga wakiandamana kupinga ukatili huo uliofanywa dhidi ya Mwandishi wa habari akiwa kazini.

  Hata hivyo Mkurugenzi wa muungano wa Vyama vya waandishi wa habari nchini UTPC Abubakar Karsan akiongea na Tanzania Daima kwa njia ya Simu amekanusha vikali kuzuia maandamano bali wao waliyabariki na ndio maana walijumuika na waandishi wengine nchini na kutoa matamko mbalimbali katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam na kwamba wao walitoa maelekezo kwa Ruvuma Press Club kuungana na Press Club zingine nchi kufanikisha maandamano ya amani ambayo yameitishwa kiuhalali.
  Mwisho
  RAI YANGU KWA UONGOZI WA (RUVUMA PRESS CLUB)

  Kwamba leo imemtokea mwangosi kesho ninyi ruvuma mko tayari???
  liko wapi tamko lenu kulaaani mauaji ya daud mwangosi??
  Mtaendelea kumlinda nchimbi hadi lini songea wakati mara zote amechakachua matokeo ya ubunge???
  Sio ninyi mlificha ukweli kwenye uchaguzi wa meya songea kuwa nchimbi alikimbia na masanduku ya kura???.
   
 8. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Dr.Nchimbi amejipenyeza sana ktk Taaluma ya habari na kuwanunua waandishi njaa wengi. Hata ile kauli aliyoitoa katika mkutano na waandishi "kama nikijiuzulu, hamtapata waziri kama mimi" ni mfano tosha wa JEURI yake. Jamaa anandoko za Urais na anajipanga, filimbi ikipigwa, awapite wote. JK yupo nyuma yake
   
 9. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Na ndio huyu huyu nchimbi aliratibu mtandao wa kikwete na kuagizwa kwenda kuchukua jimbo songea kibabe kutoka kwa mzee lawrence gama na mara baada ya kushinda kwa kuchakachua akamweka kizuizini mzee gama zanzibar kwa kigezo cha kuwa akajenge chama,mzee wa watu amekufa na stress,na ndio maaana pale jangwani hakwenda kimakosa kama sio msimamo wa kina nyanyolo kichere alikuwa anapewa mic na angehutubia sasa hata hili la mwangosi tutegemee kujipenyeza kwa waandishi waendekeza njaa kama ilivyofanyika songea!!!!!!!
   
 10. C

  CHITEMBEJA Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Tatizo la vilabu hivi havina mwongozo UTPC inaongozwa na mtu mmoja anavyotaka yeye ndiyo kuwa

  Kwa mfano Morogoro Press club waliadhibiwa kisa Abububakar karsan kwa madai yakuwa kiongozi mmoja wa ana wadhifa wa kisiasa.

  lakini huko Ruvuma kiongozi mmoja Press Club ana wadhifa wa Katibu wa Mwanasiasa wa ngazi ya juu serikali ndugu yangu karsan hajaona na kuwalazimisha kumuondoa kwa kuwa ni swahiba yake kama alivyo kiongozi mmoja wa Press Club ya Pwani.
  kila siku Karsan anavuruga Katiba za Press Club hivi sasa Press Club ni matawi ya UTPC na wala haijulikani kama zina katiba sijui huyu bwana akiachia ngazi ndiyo kuwa UTPC itakuwa imekufa na kama ndiyo hivyo kwa nini isiwe kampuni yake.

  kwa mfano mwingine utakuta viongozi wengine wa vilabu mpaka UTPC yenyewe ni waandishi wa vyombo vya serikali na CCM sasa hawa watamtumikia nani wakati linapojitokeza tatizo la kisiasa na waandishi wanaowaongoza? kama hivi la Mwangosi haoni kuwa suala conflict of interest litaadhiri umoja wa waandishi hao na Karsan anaejinadi kusimamia UTPC hajasema kitu shida sana
   
 11. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Kalamu kwa tumbo bana. Leo tulikuwa tuna kipindi kizuuuri cha POLISI NA WIKI YA NENDA KWA USALAMA hapa kwetu STAR TV. Kama nyie huko Iringa mmegomea kivyenu.
   
 12. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha Tabora nako kimya, hakuna cha kukataliwa na polisi wala kuahirishwa kana kwamba Tabora ni nchi jirani na TZ!
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  baadhi ya waandishi wa Ruvuma njaa itawauwa aisee...
   
 14. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  njaaa mbaya kweli jamani!!!!!!
   
Loading...