Viongozi wa mataifa ya Magharibi na taasisi za Kimataifa wamekemea vikali mashambulizi dhidi ya Ukraine na kuahidi kuiwajibisha Urusi

Viongozi wa mataifa ya Magharibi na taasisi za Kimataifa wamekemea vikali mashambulizi dhidi ya Ukraine na kuahidi kuiwajibisha Urusi.

Mara baada ya kuripotiwa taarifa ya milipuko katika miji mbalimbali ya Ukraine, Rais wa Marekani Joe amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kusema “Urusi pekee itawajibika kwa vifo na uharibifu utakaotakana na mashambulizi, Marekani na washirika watajibu kwa njia stahiki, dunia itaiwajibisha Urusi”.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema “Nimeshtushwa na matukio ya kuogofya Ukraine na nimeongea na Rais Zelenskyy kujadili hatua inayofuata. Rais Putin amechagua njia ya umwagaji damu na uharibifu kwa kuanzisha mashambulizi ya uchokozi dhidi ya Ukraine. Uingereza na washirika wake tutajibu mapigo kikamilifu”.

Rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwa upande wake amesema “Tunakemea vikali mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine. Katika nyakati hizi, tuko pamoja na Ukraine na wanawake, wanaume na watoto wasio na hatia wakati wakikabiliana na mashambulizi haya ya kichokozi na hofu dhidi ya maisha yao. Tutaiwajibisha Kremlin”.

Nae Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema “kwa hali inayoendelea nabadili ombi langu, Rais Putin, kwa wito wa ubinadamu, rudisha vikosi vyako Urusi. Mgogoro umalizike sasa”.

Usiku wa kuamkia leo, Urusi ilianza mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine, huku milipuko ikiripotiwa katika miji mingi na nje ya maeneo yenye machafuko ya mashariki yanayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
wanaonekana ka mbwa muoga anaebwaka sauti kubwa
 
Back
Top Bottom