Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,768
Mods unganisha huu na ule uzi wangu mwingine tafadhali.
Mods naomba maoni haya yamfikie Mhe. Tundu Lissu kama mwanasheria na mpigania haki na utawala wa Sheria katika nchi yetu.
Kwa miaka mingi tangu ujio wa vyama vingi, Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikiwatumia Mabalozi wa mashina ya Chama kwa shughuli za kiserikali isivyo halali. Mabalozi hawa ambao hawamo katika mlolongo wa uongozi wa serikali kikatiba na kisheria wamekuwa wakifanya yafuatayo isivyo halali:
Mwaka 1992 vilipoanza vyama vingi ilipendekezwa kuwa viongozi hawa warudishwe serikalini kama ilivyokuwa wakati wakiwa Wajumbe wa Nyumba Kumi ili serikali ianzie hapo, lakini kwa mshangao wa wenye akili CCM na serikali yake walikataa na kuendelea kuwatumia kufanya kazi za kiserikali kinyemela.
Wakati umefika na ni sasa, kwa wanasheria nguli kama akina Mhe Lissu kupeleka hoja mahahakamani ili watu hawa wapigwe marufuku nchi nzima kujihusisha na masuala ya kiserikali huku mitaani hadi hapo serikali itakapokubali kuanzisha utaratibu wa kisheria unaohuruhusu serakali za mitaa kuanza kwenye ' Nyumba Kumi'.
Nchi ni lazima iongozwe na Katiba na Sheria kuanzia chini hadi juu ili kuepuka kuwafanya watu wasiyotambuliwa kikatiba kuwa sehemu ya uongozi wa nchi bila utaratibu.

- Kusikiliza kesi na mashauri katika maeneo yao huku wakijuwa wazi kuwa hawana mamlaka kisheria ya kufanya hivyo. Tabia hii imesababisha Chama cha Mapinduzi kupitia kwa mabalozi hawa kupoka mamlaka ya viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
- Kushiriki kuuza maeneo kwa kugonga mihuri yao ya shina katika karatasi za mauziano yanayofanywa na wananchi kinyume cha utaratibu. Miongoni mwa lawama wanazotupiwa viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji juu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa hakika wahusika wakuu ni mabalozi waliojivika majukumu ya kiserikali kinyume cha utaratibu wa kikatiba na kisheria.
- Kutambuliwa na taasisi mbalimbali za kiserikali na za kibinafsi kama polisi, mahakama, mabenki n.k ni ishara mbaya ya vyombo vyetu kutojali kanuni za utendaji wa serikali, hivyo kusababisha mkanganyiko wa kuchanganya utendaji wa viongozi wa Chama cha Siasa na ule wa serikali. Inashangaza kwamba hata mahakama ambayo ndiyo inapaswa kusimamia tafsiri ya sheria, huweza kumwita balozi wa shina kutoa ushahidi wa masuala ambayo yanatakiwa yasimamiwe na viongozi wa serikali wa eneo husika.
- Kurubuni wananchi wakati wa chaguzi mbalimbali kwa kuwa kichocheo cha rushwa. Hapa itoshe kusema tu kuwa ikiwa kuna Mwana JF ambaye nyumbani kwao/kwake balozi wa shina hajawahi kufika na furushi la chumvi n.k. ili kuwashawishi kutoa kura kwa wagombea wa CCM, ajitokeze na awe mkweli mbele za Mwenyezi Mungu.