viongozi wa manispaa ya kinondoni wauza ufukwe wa masaki;WIZI mtupu;PINDA UNALIJUA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

viongozi wa manispaa ya kinondoni wauza ufukwe wa masaki;WIZI mtupu;PINDA UNALIJUA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Wana Jf KAMA MNAKUMBUKA MWAKA HUU TULIKUJA NA MALALAMIKO YA WATU WA MASAKI NA COCOBEACH BAAADA YA VIONGOZI WA MANISPAA HII YA KINONDONI KUUZA COCOBEACH BILA UTARATIBU...SAKATA HILI ILIBIDI LIINGILIWE KATI NA WAZIRI MKUU NA KUWAAMURU JAMAA WARUDISHE 10% WALIYOKULA,....
  HIVI SASA KUNA SEHEMU ILIO WAZI UPANDE WA MASKI KARIBU NA BAHARI SEHEMU AMBAYO WATOTO WAMEKUWA AKIPUMIZIKA NA WANANCHI WENGINE,...HIVI MAJUZI IMEVAMIWA NA WAHINDI NA KUANZA KUJENGA KABLA YA WANA MASAKI KUANZA KWENDA NA KUZIA UJENZI HUU KWA MINAJILI YA "WIZI MTUPU" UMETENDEKA KUMGAIA SEHEMU HII.....
  MWENYEKITI WA SERIKALI YA MITAA YA MASAKI JANETH MBENE ALLIUNGA MKONO AKISEMA HUU NI UFISADI ULIOVUKA MPAKA,,WAKAZI WA MASAKI TULIIDHINISHWA ENEO HILI TANGU AGOSTI MWAKA JANA KUWA LA WAZI NA TAYARI TUMEENDELEZA KWA KUPANDA MITI NA USAFI ,..TUNASHANGAA BILA TAARIFA TUNASHANGA KUONA WATU WANAJENGA HAPANA HII AIWEZEKANI,... ALISEMA KATIBU WA UCHUMI WILAYANI KINONDONI ZAIDEUN ADAMJEE..HUKU AKIONYESHA RAMANI IKIONYESHA NI ENEO LA WAZI NA WAMETUMIA MILLION 50KULIENDELEZA.. MMOJA WA WAHINDI ALIPOFWATA ALISEMA HILI ENEO TUMENUNUA KIHALALI NA KAMA MNA MALALAMIKO NENDENI MANISPAA KAMA WAMEUZA SI TUFANYAJE,...

  WAZIRI MKUU PINDA KAMA ULIVYOTUMIA MAMLAKA YAKO KUUZUIA COCOBEACH TUNAOMBA USAIDIE NA HILI.WANAMASAKI TUKO CHINI YA MIGUU YAKO

  XMASS NJEMA
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivi kwanini Manispa/Halmashauri zetuwasiwe wanaomba maoni ya Wadau , mfano wakazi wa eneo husika kabla ya kubadili matumizi ya ardhi kuongeza uwazi wa maamuzi yao na kuangalia masilahi ya pande zote. Pia kupunguza dalili pamoja na Rushwa Yenyewe. Waziri Husika/Waziri Mkuu chukueni hatua hiyo haraka ilituepukane na migogoro na kupoteza kwa pesa kusiko kwisha.


  Date::12/17/2009Manispaa Kinondoni watuhumiwa kuuza eneo ufukwe wa wananchi Masaki[​IMG]Na Leon Bahati

  KATIKA hali inayoashiria kuzidi kuimarika kwa ufisadi, viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wanatuhumiwa kuuza kwa wawekezaji kutoka nje eneo pekee la wazi lililo Masaki, wilayani Kinondoni.

  Eneo hilo lililo karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi limekuwa likitumiwa kwa mapumziko, lakini sasa wananchi hawataweza kulitumia, Mwananchi imeambiwa.

  Wakazi wa Masaki wameeleza kuwa wameshabaini ufisadi huo na wameahidi kusimama kidete ili kuhakikisha eneo hilo linarejeshwa na kuendelea kutumiwa kwa mapumziko na michezo ya watoto.

  Manispaa ya Kinondoni imekuwa ikihusishwa na ufisadi wa maeneo kwa muda sasa na mwaka jana ilihusishwa na kashfa ya kuuza eneo la ufukwe wa Coco Beach ambao umekuwa ukitumiwa zaidi na walala hoi kupumzika.

  Iliwalazimu viongozi hao wabatilishe uamuzi wao baada ya kilio cha walalahoi kumfikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye aliingilia kati akisema kuwa ubinafsishwaji huo haukufuata taratibu.

  Baadhi ya wakazi wa Masaki jana walikusanyika eneo hilo wakiwa na mabango mbalimbali kulaani kitendo kilichofanywa na viongozi wao.

  Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Masaki, Janeth Mbene aliwaunga mkono akisema kuwa huo ni ufisadi uliovuka mipaka.

  “Wakazi wa Masaki tuliidhinishiwa eneo hili kuwa la wazi tangu Agosti mwaka jana. Tayari tumeliendeleza kwa kupanda miti na kutengeneza bustani. Tunashangaa bila hata taarifa tunaona watu wanaanza kujenga,” alisema.

  Katibu wa uchumi na fedha wa CCM wilayani Kinondoni, Zainudeen Adamjee alionyesha ramani kudhihirisha kuwa ardhi hiyo imeidhinishwa kuwa eneo la wazi na walitumia Sh40 milioni kuliendeleza, lakini sasa bustani hizo zimeharibiwa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi.

  Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni miongoni mwa waliolinunua eneo hilo na ambaye ana asili ya Kiasia alifoka akisema eneo hilo amelinunua kihalali na kwamba kama kuna tatizo walaumuwe manispaa.

  “Mimi nimefuata taratibu zote kulinunua. Kama lina matatizo siyo kosa langu. Ni kosa la Manispaa,” alisema na alipoona waandishi wanazidi kumbana aliwatishia kuwa angewafyatulia risasi.

  “Ondokeni nitawafyatulia risasi,” alitishia mwekezaji huyo ambaye alikuwa amefika eneo hilo akiwa ameandamana na mwenzake mwenye asili ya kizungu, ambaye wakati wote alionekana kuwa kimya na kutotaka kusema chochote.
  Mwenyekiti wa Mipango Miji wa Baraza la Madiwani Kinondoni, Hassan Rajabu alisema eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na mtu binafsi na walichofanya ni kuliidhinisha kwenda kwa mtu mwingine.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
Loading...