Micro E coli
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 938
- 192
Upo kwenye ofisi yenye viyoyozi,unatembelea gari la wizara, hujui manesi tunavyozalisha bila kuvaa gloves mikononi huku tukimwagikiwa na amniotic fluid na damu usoni. Hujuhi tunavyotumia mwanga wa Nokia kuzalisha huku vichanga vikitufia mikononi kwa ukosefu wa vifaa kupumulisha vichanga hivyo. Hufahamu kabisa jinsi ndugu na jamaa za wagonjwa wanavyotumwagia mvua za matusi kwa kushindwa kuwahudumia wagonjwa wao kisa dawa na vifaa hamna.
Nikukumbushe ulivyokuja Mwanza pale ukumbi wa Gandhi, unakumbuka wauguzi walivyokwambia: Tulikwambia hatuijuhi TANA hata kirefu chake, tulikwambia tunavyokatwa hela hiyo NGO yenu kwa lazima tena ada hizo huunganishwa na malipo ya leseni kwa kulazimishwa,sasa BOSI hao wauguzi unaowahimiza wasigome ni wa hapo Dar-es-salaam au?
Unakumbuka tulivyokuuliza uhalali wa sisi kulipia leseni sh. 50,000 huku kada zingine za afya hawalipi chochote na ukatujibu kwa kiburi hasa huyo raisi wa TANA (luteni kanali wa jeshi) huyo jama mwenye mikogo mingi, kiburi,mjivuni,eti ana master ya Uuguzi kutoka UK,kuwa na master ndio kuwa mwizi? Ndiyo wewe ni mwizi, kuna mpango umeuanzisha unataka wauguzi wakatwe ada ya TANA moja kwa moja kwenye mishahara kupitia hazina. Hiyo janja yako tumeshaijua,na ndio sababu mnahimiza wauguzi wasishiriki kwenye mgomo. Umelewa madaraka wewe,kwa akili zenu tana mnadhani bila daktari 'ku-prescribe'muuguzi wa Tanganyika anaweza kufanya lolote? Hata nursing care za kawaida tunaandikiwa tu!
Mwisho wauguzi wote wa Tanzania pamoja na kutojiamini kwetu,pamoja na shida zetu,tusikubali wanyonyaji TANA watwambie la kufanya, kama ni kugoma au kutogoma uamuzi tunao sisi,wanaovaa disposable gloves kuzalishia huku zinatutobokea ni sisi,TANA kazi yao kutembeza bakuli kwa wafadhiri kuomba fedha za kutembelea 'matawi' yao!
umeniongezea hasira kwa hawa nyau nilipo kuwa mganga mfawadhi kituo cha afya fulani hapo Morogoro manurse wangu tulikuwa tunaishiwa gloves mpaka tunashika damu na amniotic fluid kulitokea kipindupindu ilikuwa balaa drip hakuna halafu leo jitu linajitokeza kwenye TV na kuanza kubwatuka mpaka povu linawatoka huyu hatakama ana masters hiyo masters haijamsaidia kitu bado halija elimika limenunuliwa na magamba ndio linafanya propaganda za kitoto kisa njaa,njaa hizo zitawafikisha pabaya hawa nyang'au.