Viongozi wa manesi TANA kuwaponda madaktari ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa manesi TANA kuwaponda madaktari ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by yeto, Mar 9, 2012.

 1. y

  yeto Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  Taarifa ya habari ya sa 2 ya ITV wameonesha viongozi wa TANA wakisema kuwa madaktari hawajafanya vizuri kugoma hivyo wao wamejipanga vizuri kuwafariji na kuokoa maisha.
   
 2. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Upo kwenye ofisi yenye viyoyozi,unatembelea gari la wizara, hujui manesi tunavyozalisha bila kuvaa gloves mikononi huku tukimwagikiwa na amniotic fluid na damu usoni. Hujuhi tunavyotumia mwanga wa Nokia kuzalisha huku vichanga vikitufia mikononi kwa ukosefu wa vifaa kupumulisha vichanga hivyo. Hufahamu kabisa jinsi ndugu na jamaa za wagonjwa wanavyotumwagia mvua za matusi kwa kushindwa kuwahudumia wagonjwa wao kisa dawa na vifaa hamna.

  Nikukumbushe ulivyokuja Mwanza pale ukumbi wa Gandhi, unakumbuka wauguzi walivyokwambia: Tulikwambia hatuijuhi TANA hata kirefu chake, tulikwambia tunavyokatwa hela hiyo NGO yenu kwa lazima tena ada hizo huunganishwa na malipo ya leseni kwa kulazimishwa,sasa BOSI hao wauguzi unaowahimiza wasigome ni wa hapo Dar-es-salaam au?

  Unakumbuka tulivyokuuliza uhalali wa sisi kulipia leseni sh. 50,000 huku kada zingine za afya hawalipi chochote na ukatujibu kwa kiburi hasa huyo raisi wa TANA (luteni kanali wa jeshi) huyo jama mwenye mikogo mingi, kiburi,mjivuni,eti ana master ya Uuguzi kutoka UK,kuwa na master ndio kuwa mwizi? Ndiyo wewe ni mwizi, kuna mpango umeuanzisha unataka wauguzi wakatwe ada ya TANA moja kwa moja kwenye mishahara kupitia hazina. Hiyo janja yako tumeshaijua,na ndio sababu mnahimiza wauguzi wasishiriki kwenye mgomo. Umelewa madaraka wewe,kwa akili zenu tana mnadhani bila daktari 'ku-prescribe'muuguzi wa Tanganyika anaweza kufanya lolote? Hata nursing care za kawaida tunaandikiwa tu!

  Mwisho wauguzi wote wa Tanzania pamoja na kutojiamini kwetu,pamoja na shida zetu,tusikubali wanyonyaji TANA watwambie la kufanya, kama ni kugoma au kutogoma uamuzi tunao sisi,wanaovaa disposable gloves kuzalishia huku zinatutobokea ni sisi,TANA kazi yao kutembeza bakuli kwa wafadhiri kuomba fedha za kutembelea 'matawi' yao!
   
 3. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  hao sio viongo ni madikteita wa TANA,hasa huyo raisi wa TANA (luteni kanali),manesi hatuwatambui. Jiulize mmoja wao ni mtumishi hapo wizara ya afya makao makuu kwa mzee Mponda na Nyoni...unategemea atasema gomeni wauguzi? Hao ndio wachumia tumbo wanatafuna ada za 'wanachama'
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,908
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Sasa ukigoma una uhakika gani wa kupata kile unchokitaka?
   
 5. E

  Escherichia Coli Senior Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa hatuna uhakika wa kupata usalama wa maisha yetu na clients kwa mgomo tuendelee kurisk maisha kwa uzembe wa watawala wanaofuja rasilimali za taifa???Hatujagoma lkn uamuzi tuachiwe sisi,tumechoka kutukanwa na wazazi.
   
 6. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Si sahihi kabisa. Kwa nini wasingetafuta audience na viongozi wa Madaktari kama kweli wao wamekwenda shule na kujua umaana wa kushirikiana na Madaktari katika kumasaidia / kumwokoa Mgonjwa? Tangu lini kukimbilia kwenye vyombo vya habari kunatatua matatizo ya namna hiyo.

  Pamoja na yote hata nilivyowasikiliza hao viongozi wa TANA nimegundua kuwa ni watu wenye upeo mdogo sana na kauli zao hazina weledi.
   
 7. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Manesi wanapata shida zaidi ya madaktari, ni vizuri/lazima serikali iwajali watu wake.
   
 8. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,145
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Kwani asipogoma ana uhakika gani wa kupata hicho anachokitaka?.?????
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  manesi,clinical officers na assistant medical officers ndio waliochafua sekta ya afya.badala ya kudai maslahi yao kwa serikali wao wamebaki kuchukua rushwa kwa wagonjwa.ni bora ya madaktari waliogoma mara mia kuliko hawa wanafiki wasiogoma kwani huchukua rushwa na kuumiza watanzania.daktari aweza kumuandikia dawa mgonjwa lakini nesi anamchakachua kwa kutompa dawa inayostahili so sad!!tuangalie ni visa vingapi vya kupigwa wanavyovipata,mfano mzuri ni pale mwananyamala hospital ambapo leo tunaambiwa ni wema sana hawajagoma
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nasema wale waliojitokeza wote hawafai waliua chama cha wauguzi TARENA nashangaa kuna kitu kinaitwa TANA yule mwenye meno makubwa mwenye shati la pinki anaitwa Msele toka alivyomaaliza chuo hajawahi kukaa nje ya nyumba za Muhimbili kuanzia chai mpaka chakula cha usiku cha watoto wake anadoea kwenye majiko ya wagonjwa Muhimbili.

  Mwambinghu ni manesi walioamua kujiunga na jeshi baada tu ya kugraduate ni muuguzi mkuu wa hospitali ya lugalo anaitwa luteni Kanali Mwambingu hata chuo alikuwa bogus kama alivyo sasa was not man enough, alikuwa banchi moja na luteni Chiku Galawa (Mkuu wa Mkoa wa Tanga) yule chief nursing officer ni sipukupuku ameuaa division ya nursing manesi wa siku hizi wako kama mahousegirls sio proffesionals.

  Manesi hapo Muhimbili wamewahi kuanzisha mgomo ukasambaa nchi nzima na mambo mengi yaliboreshwa,Aibu kubwa chief nursing officer kuwa against na madakatari angalia bifu litakalokuwepo kati ya madaktari na manesi kwa sababu ya waapumbavu hao wa wwizarani na jeshini

  Manesi wengine wawaunge mkono madaktari katika vita hii haipaswai kutangana Daktari na Nesi centre yao ni mgonjwa kwa hiyo madai ya madaktari yatawanufaisha na wao
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  manesi huku vijijini wanauza pamba,gloves na viguo vya watoto ili wakabiliane na hali ngumu ya maisha halafu anaibuka ''kiongozi dikteta'' kutoa matamshi ya kipuuzi namna ile lol.
  Magesa yuko wapi awapindue hawa?wizara nzima ya afya ni ya kusafisha kabisa kwani hawa ndio washauri wa waziri
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ndo maana hata mazungumzo ya mwanzo doctors waliamua kujitoa. Wale ndio watu walioletewa wajadili nao,badala ya kutoa hoja za kuboresha sekta ya afya wakaishia kuimba taarabu. Huko kujipanga wanakosema waende wakasome md ili waje kuprescribe madawa.
   
 13. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Asante sana mkuu wangu lakini itawalazimu manesi wachukue hatua kusafisha hali ya hewa baada ya matamshi ya kijinga ya viongozi wao leo.
   
 14. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  naamini yule kiongozi wa manesi muhimbili anaweza hili jambo.ndugu magesa pale muhimbili ndiye alikuwa nurse student wa kwanza kuingoza serikali ya wanafunzu,huko nyuma serikali ya wanafunzi ilikuwa ikiongozwa na M.Ds pekee.ana mapungufu yake lakini hayajafikia ya hawa wachumia tumbo.
   
 15. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,908
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Froida unaongea mpka povu linakutoka mdomoni.
  Kazi hiyo kama inawaboa jiungeni na sisi wa mitaani katika shughuli zisizo rasmi na biashara.
  Leo tunalipa kodi kibao watu hawafanyi kazi,huduma hatupati na hata ukipata ndo kama unafanyiwa favor.
  Tijue moja ,hospitali zote ziuzwe ili hii huduma isituumize walipa kodi.
   
 16. gimmy's

  gimmy's JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 2,362
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  msione sisi wananchi tumekaa kimya mkafikiri ni wajinga,tunawatafakari tu ila tutafika.
  Tunajua kiburi chenu ni huo uchache wenu katika taaluma yenu.
  Nyinyi pia hua ni chanzo cha matatizo,tunajua ni wauzaji wakubwa wa dawa na vifaa vya serikali zinazosambazwa na MSD ktk mahospitali.Leo unalalamika unazalisha bila gloves una risk maisha wakati gloves mnazifanyia biashara.Na kama ni isue ya kudai maslahi yenu hamkatazwi ila si kwa style hii ya mateso kwa wa tz wasio na hatia yoyote!
   
 17. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...wewe rais wa Tana uliye na degree ya UK ulikuja Mwanza tukakueleza shida zetu ukasema utapeleka kwa wahusika,kwenye kikao kikubwa kilichofanyika Singida ukatupa mrejesho kwamba wizara imetuahid kutatua matatizo yetu hukusema ni lini watatatua shida hizo,kwa uelewa wako huo mbovu na kutuburuza sisi wauguzi unaona ni sawa kwa sababu wewe uko kwenye kimvuli na familia yako,wauguzi tukae natukatae hiyo Tana kwan haina msaada kwetu,uoga wetu unatupeleka sehemu mbaya,toka lini mtwana akamsaliti bwana?

  Huyo Rais wa Tana yuko wizarani hivyo lazima aseme pumba kupalilia ajira yake,wauguzi tukimwage hicho chama cha Tana tutengeneze chama chetu ambacho kinajitegemea,na pia tung'ang'ane tuwe na utawala wetu wenyewe sio kila kitu tupite kwa daktari mkuu.

  Mwanza wauguzi wa jiji tuna shida hadi tunatamani kuachana hii kazi, watawala hawatutendei haki hata tone,huyu afsa utumishi mkuu Mungu atamlaani kwa kutunyanyasa wauguzi,tumejikunyata kwa uoga wetu na pia hatuoni chama gani cha kututetea, bora tujiunge na chama cha wafanyabiashara wa mboga mboga kwa sababu tutapata lishe bora, na kujiongezea kipato kidogo kwa hiyo biashara nakusahau maswala ya hawa wajinga waliojichagua kutoka wizaran, huyu Rais ni mwanajesh hivyo kila kitu anapata kwa nafuu hata akili yake imedumaa tu, wauguzi mnafikiri atafanya nini kwa maslahi yetu?

  Wauguzi tushikamane tutetee haki zetu, namalizia kwa kusema TANA kufa kabisa.
   
 18. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Majuzi nesi mmoja hapa Igoma health centre amedakwa na Star Tv 'live' akimuuzia kadi mama mjamzito sh.500,kibarua kiote nyasi kwa 'jero' tu!
   
 19. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Majuzi nesi mmoja hapa Igoma health centre amedakwa na Star Tv 'live' akimuuzia kadi mama mjamzito sh.500,kibarua kiote nyasi kwa 'jero' tu! Kugoma kudai haki zenu hamtaki,hadi shida ziwaumbue?
   
 20. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu! Umenisaidia kumfahamu luteni kanali! Jamani wauguzi mpo wapi tuanzishe mapinduzi kwenye kada hii?
   
Loading...