Viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa watakiwa kutanguliza maslahi ya umma mbele na kujituma

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
VIONGOZI WA KUCHAGULIWA NA KUTEULIWA WATAKIWA KUTANGULIZA MASLAHI YA UMMA MBELE NA KUJITUMA;

Akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani Dodoma Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa Ndg. Lailah Ngozi ambaye pia ni mlezi wa kichama Mkoani humo amewataka viongozi wa CCM,wabunge,madiwani,wenyeviti wa Serikali za Mitaa,vitongoji,vijiji na watendaji wa Serikali kuzingatia maadili na kuwajibika kikamilifu kuwatumikia wananchi.

*"Ndugu viongozi wenzangu leo nahitimisha ziara yangu Dodoma lakini sio mwisho wa mimi kuendelea kuitembelea Dodoma,mimi hapa ni mlezi wenu kichama ninawajibika kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuhakikisha katika chaguzi zijazo CCM inashinda kwa kishindo hivyo nisingependa kuona mtu yeyote anayetaka kuutia doa Mkoa huu wa Dodoma wenye historia ya kipekee kwa Nchi yetu na Chama chetu."*

Ndg. Ngozi aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika kikao cha majumuisho kati yake na viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma,wabunge wa Mkoa wa Dodoma na madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa.

Katika kikao chake hicho aliwataka viongozi hao kutambua kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekaribia waache kukaa maofisini wawatembelee wananchi vijijini kusikiliza shida zao wasisubiri wakati wa uchaguzi kwenda kuomba kura,

*"Ndugu viongozi kila mmoja wetu sasa akafanye ziara ili kujua shida za watu wetu na kuzitatua maana uchaguzi haupo mbali na kila mmoja wetu atapimwa kwa matendo yake lakini wewe usiwe kikwazo kwa Chama kutokuaminika kwa uzembe wako."* Alisema Ndg. Ngozi.

Mwisho kabisa aliwashukuru sana viongozi na wana CCM wa Mkoa wa Dodoma kwa ushirikiano waliompatia toka mwanzo wa ziara yake mpaka kuhitimisha hapo jana na kuwaahidi kuwa ataendelea kushirikiana nao kwa kila hali katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 - 2020.

*"Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitaondoka hapa bila kuwashukuru wana Dodoma kwa ukarimu wenu,mmenipa mapokezi mazuri sana na ushirikiano mzuri naahidi kuilinda heshima hii mliyonipa kwa kushirikiana nanyi kikamilifu katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya ccm."* alisema Ndg.Ngozi katika hotuba yake

Lakini pia aliwasisitiza viongozi wa CCM kuyatangaza mambo yote mazuri yanayofanywa na Serikai ya awamu ya tano chini ya Dr.John Pombe Magufuli.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
IMG-20190211-WA0041.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom