Viongozi wa Kitaifa wapimwe afya ya ubongo na mwili mara kwa mara

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,006
3,643
Nchi yetu inahitaji kuwa na maendeleo ya kasi katika uchumi, elimu na masuala ya mengine ya kijamii. Ili kufikia lengo hilo, Taifa linahitaji viongozi imara wanaoelekeza fikra zao katika kuleta maendeleo.

Fikra nzuri hutokana na afya bora ya ubongo na mwili. Nimejaribu kudukua taarifa ktk media mbalimbali za afya za baadhi ya viongozi hasa maraisi nikagundua:
1. Wengi,hutibiwa nje ya nchi zao.

2. Taarifa za maradhi yao huwa siri.

3. Aidha,wakifariki,au kushindwa kuongoza,ndiyo siri huvuja.

4. Dalili za baadhi ya magonjwa huanza kujinyesha kwa wao kuwa wakali au kubadili tabia.

Kwa hiyo namba 4, kuna mfano dhahiri wa aliyekuwa Raisi wa Gambia Yahaya Jammeh. Mwaka 2013/14 aligundulika amedevelop cancer ya utumbo mpana na ubongo nchini Ufaransa. Nchini kwake aliaga anaenda kucheki afya yake. Kwa vile alishajiwekea utaratibu wa kutibiwa nje, hospitali za umma nchini kwake hawakuhusishwa.

Tabia ya Jameh kiutawala ilikuwa imeanza kubadilika hadi mwisho akatolewa kwa aibu. Ninaamini kuna umuhimu kama Taifa kuwa na taasisi maalumuya kufuatilia mwenendo wa tiba za nje na afya za viongozi wetu wa kitaifa. Tusiridhike tu kuwa tiba ya nje ya nchi ni sahihi bila kulisaidiaTaifa.
 
Uhai na uzima wa bindamu ni upendeleo kutoka kwa Mola! Angalia usije kujiletea kiburi cha uzima Mwenye Enzi Mungu akaamua kukushusha!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Uhai na uzima wa bindamu ni upendeleo kutoka kwa Mola! Angalia usije kujiletea kiburi cha uzima Mwenye Enzi Mungu akaamua kukushusha!
Sijapingana na Maamuzi ya Mola. Kwa mantiki hiyo,tunazo hospitali na wakati huohuo Mola yupo. Tutumie vyote pale inapowezekana kwa mustakabali wa Taifa letu na vizazi vijavyo!
 
Marais wote duniani wana team zao za Madaktari bingwa ndani ya nchi na ndiyo wenye dhamana ya Afya ya Rais ktk nchi.

Kwenda nje ya nchi kutibiwa hayo ni mambo ya Taasisi ya urais ktk nchi husika.

Taarifa za kiafya za kila Rais huwa Team ya Madaktari wake wa ndani ya nchi wanaijua na namna ya kuishughulikia in case kama Rais life standing disease mfano,Pumu,Allergy,Kisukari n.k
 
Pascal,nimekuelewa,na nimepitia thread. Ninachokiona mimi,sijawa na mfano kwa hapa Tz. Nimetoa mfano wa Yahya Jameh na baadhi ya wengine ambao hili limeshatokea,na bado halijawekewa mkakati. Kama kuna cha kujifunza,nasi tusiende huko bali tuanze sasa kutumia taasisi zetu za afya za umma . Mbona Saratani ya matiti wanafanya,na wamefanikiwa kuokoa maisha ya dada zetu? Wanatangaza matokeo (collectively) na kuchukua hatua ( individually). Bado ninaamini,tunaweza kufika mahala ambapo kwa nia njema,tukawa na maendeleo ya dhati kupitia fikra zenye tija kutokana na afya bora!
 
Kwa Tanzania pia kuna Siri hospital kwa sababu madaktari hula kiapo cha kutozitoa Siri za mgonjwa, hivyo hata wakipimwa wakakutwa ni vichaa majibu yao yatakuwa Siri hasa ukizingatia wanajipendekeza na kuogopa kutumbuliwa Jipu, kitendo cha kwenda bandarini kutengeneza Sinema kwa kontena za zamani kisha jana akaja na mikwara kwa vyombo vya Habari ni kipimo tosha kuwa kuna Tatizo, hata kumkumbatia Daudi msukuma mwenzenu akina pasco pia ni kipimo, vipimo Vizuri hupimwa kwa matamshi, matamko na vitendo.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Marais wote duniani wana team zao za Madaktari bingwa ndani ya nchi na ndiyo wenye dhamana ya Afya ya Rais ktk nchi.

Kwenda nje ya nchi kutibiwa hayo ni mambo ya Taasisi ya urais ktk nchi husika.

Taarifa za kiafya za kila Rais huwa Team ya Madaktari wake wa ndani ya nchi wanaijua na namna ya kuishughulikia in case kama Rais life standing disease mfano,Pumu,Allergy,Kisukari n.k
Ninajua hilo, ila tunae raisi mmoja Afrika (Bouteflika) ameugua several years bila nchi kuamua cha kufanya! Pia ujue ana timu bingwa ya madaktari wa ndani na wa nje! But katiba yao inatambua ni raisi probably till death! Hao madaktari kawaweka yeye,and its unlikely wasuggest otherwise! Nimetoa mfano wa Yahya Jameh na pitia decisions mbalimbali alizozifanya kama raisi! Laiti kungekuwa na statutory govt health organ ya kuexamine kwa undani behavioral changes vs healthy status kwa huyo raisi na kukawa na public debate, umma ungeamua vinginevyo.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwani Tz kuna tatizo la afya ya watawala?
Sina uhakika! Kupata jibu itahitaji utafiti. Mfano, MEWATA hufanya uchunguzi huru wa breast & cervix ca,s kwa kinamama wanaojiona fit,na kugundua wana dalili za kuwa na ca,s. Hivyo, kwa hii hoja yangu ni more sensitive na naamini tungekuwa na statutory organ inayowajibika kwa umma kuhusu niliyoyaeleza awali,na ishauri umma kwa tafiti,jibu la swali lako ungelipata!
 
Kuongoza watu siyo lele mama...
Hasa ikiwa huna dira ya wazi. Mwl Nyerere alijitahidi kwa kila wazo lake la maendeleo,aliliweka wazi na miongozo kibao ilichapishwa. Mf. "Mwongozo wa Azimio la Arusha".
 
Nimeangalia video clip ya majibizano na matamshi na maamuzi ya viongozi wa bunge,wabunge waliotoa lugha za kuudhi bungeni juzi,reactions za wabunge na baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali kufuatia uchaguzi wa wabunge wa EALA, naona kuna tatizo. Hivyo,bado nafikiri this thread still holds water.
 
Yule mwanamke alitoa ushauri kuwa huyo mnaenipatanisha nae hapaswi ku,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, upresidaaa ila anapaswa kupelekwa mirembe
 
Ipo haja ya viongozi kufanyiwa psyco analysis mara kwa mara,wengi hawako sawa kichwani
 
Ukiishi nchi kama Hii lazima upate matatizo ya aaili. Sasa hata ukienda kwa daktari unakuta nayeye pia ana matatizo ya akili kwahiyo mnaonekana wote mko normal.
 
Nchi yetu inahitaji kuwa na maendeleo ya kasi katika uchumi, elimu na masuala ya mengine ya kijamii. Ili kufikia lengo hilo, Taifa linahitaji viongozi imara wanaoelekeza fikra zao katika kuleta maendeleo.

Fikra nzuri hutokana na afya bora ya ubongo na mwili. Nimejaribu kudukua taarifa ktk media mbalimbali za afya za baadhi ya viongozi hasa maraisi nikagundua:
1. Wengi,hutibiwa nje ya nchi zao.

2. Taarifa za maradhi yao huwa siri.

3. Aidha,wakifariki,au kushindwa kuongoza,ndiyo siri huvuja.

4. Dalili za baadhi ya magonjwa huanza kujinyesha kwa wao kuwa wakali au kubadili tabia.

Kwa hiyo namba 4, kuna mfano dhahiri wa aliyekuwa Raisi wa Gambia Yahaya Jammeh. Mwaka 2013/14 aligundulika amedevelop cancer ya utumbo mpana na ubongo nchini Ufaransa. Nchini kwake aliaga anaenda kucheki afya yake. Kwa vile alishajiwekea utaratibu wa kutibiwa nje, hospitali za umma nchini kwake hawakuhusishwa.

Tabia ya Jameh kiutawala ilikuwa imeanza kubadilika hadi mwisho akatolewa kwa aibu. Ninaamini kuna umuhimu kama Taifa kuwa na taasisi maalumuya kufuatilia mwenendo wa tiba za nje na afya za viongozi wetu wa kitaifa. Tusiridhike tu kuwa tiba ya nje ya nchi ni sahihi bila kulisaidiaTaifa.
Naunga mkono hoja, 2015 vichaa wengi walishika madaraka na matokeo yake tunayaona
 
Yule mwanamke alitoa ushauri kuwa huyo mnaenipatanisha nae hapaswi ku,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, upresidaaa ila anapaswa kupelekwa mirembe
Yule mwanamke nae aliambulia kichapo akalazwa Sewa Haji Muhimbili.. Ni kweli Muhusika alikuwa apimwe akili vyema
 
Back
Top Bottom