Viongozi wa kisiasa wawe wanastaafu wakifikisha miaka 70 ili wapate muda wa kusimamia afya zao

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,900
141,836
Katika nyakati hizi ni heri hawa wazee wetu waliotumia muda mwingi kwenye siasa wakapumzishwa ili waweze kusimamia afya zao na kulea wajukuu.

Kwa mfano mzee Mrema, Mzee Cheyo, mzee Rungwe, mzee Shibuda , mzee Malecela na wengine wote wafananao na hao.

Tuwaachie watu wenye fikra mpya!
 
Suala la kusimamia afya halina uhusiano na siasa. Suala la afya sio la wakati mhusika kufika miaka 70 ni swala la kufanya kila siku na aina ya maisha ambayo mhusika mwenyewe amechagua.
 
Bwana mbatizaji, waambie ukweli sio kusimamia afya zao bali wapishe wengine angalau kutatua tatizo la ajira tena ikiwezekana wengine wastaafishwe wakiwa na 50yrs tu...
 
Siasa haina kustaafu...

Uliza Joe Biden na Trump wana umri gani

Umri huo tunahitaji uzoefu wao na hekima yao kubwa
 
Back
Top Bottom