Viongozi wa kisiasa tambueni hili

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
NITACHUNGA MIDOMO YANGU

Zaburi 141:3
Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

Katika matumizi ya lugha, pengine hakuna kosa ambalo wazee na vijana ni rahisi kulichukulia kuwa jepesi zaidi kuliko maneno ya haraka na makali. Wanadhani ni udhuru wa kutosha wanapojieleza kuwa, “Ulimi umeteleza tu, na sikumaanisha hasa nilichosema.” Lakini neno la Mungu halichukulii jambo hilo kirahisi...

Sehemu kubwa ya udhia, huzuni kubwa, na usumbufu, katika maisha hutokana na hasira isiyotawaliwa. Wakati mmoja, kwa njia ya maneno yakitamkwa kwa ghafla, kwa hamaki, ya ovyo ovyo, yanaweza kuleta madhara ambayo toba ya maisha yote haiwezi kuyarekebisha. Ndiyo, mioyo imevunjwa, marafiki wametengana, maisha yao yameharibika, kwa sababu ya maneno yaliyosemwa kwa ukali na haraka na wale ambao walitarajiwa kusaidia na kuponya!... Kwa maana hiyo, nguvu yake mwenyewe mwanadamu hawezi kuitawala roho yake. Lakini kwa njia ya Kristo anaweza kukuza uwezo wa kujitawala.

Uimara thabiti na kujitawala, ni muhimu kwa mwanasiasa, ili kudumisha nidhamu katika jamii. Sema kile unachokikusudia kwa utulivu, tenda kwa kujali, na tekeleza unachokisema pasipo kuyumba. Usiruhusu uso kukunjamana wala neno kali kutoka katika midomo yako. Mungu huandika maneno yote katika kitabu cha kumbukumbu.

Kufanya kazi kupita kiasi wakati mwingine husababisha upotevu wa kujitawala. Lakini Bwana halazimishi kamwe mabadiliko ya haraka, yenye utata. Wengi hujikusanyia mizigo ambayo Baba wa mbinguni mwenye rehema hajawatwisha.

Majukumu ambayo Mungu hakupanga wayafanye huwafanya wengine wakimbizane sana. Mungu hutamani tutambue kuwa hatulitukuzi jina Lake tunapochukua mizigo mingi na kusababisha tufanye kazi kupita kiasi mpaka tuichoshe mioyo yetu, tuzichoshe akili zetu, tuudhike na tukasirike na tufoke. Inatupasa kubeba majukumu ambayo Bwana ametupatia, tumtumaini Yeye, na hivyo tuitunze mioyo yetu katika hali ya usafi na uzuri na huruma.


MUNGU AKUBARIKI, KWA NENO LAKE, EWE MWANASIASA, KABLA HUJAFUNGUA KINYWA CHAKO
 
Back
Top Bottom