Viongozi wa Kiroho toka enzi walichukiwa kwa kusema kweli, kwa sasa tuna viongozi wa Dini wanaokumbatia uongo kuwafurahisha watawala dhidi ya Haki

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Kitabu cha Injili ya Marko sura ya Sita mstari wa Kumi na saba unaelezea kisa cha Yohane Mbatizaji kufariki.

Mfalme Herode alikuwa akimwogopa sana Yohanne mbatizaji. Hii ni kwa sababu Yohane alikuwa akimweleza wazi wazi Mfalme Herode pale alipokosea.

Mara ya Mwisho Yohane Mbatizaji alimkanya na kumwambia wazi wazi Kuwa Herode alifanya vibaya kumuoa mke wa ndugu yake aliyekuwa akiitwa Herodia. Huyu Herodia alikuwa mke wa Filipo ndugu yake Herode.

Ndio maana siku siku ya sikukuu ya Herode ya kuzaliwa baada ya binti yake Herode ambaye alizaa na huyu Herodia kucheza vizuri na baba yake kumwambia achague Zawadi mama yake binti huyu alipendekeza mtoto wake achague kichwa cha Yohane kwa kuwa alikuwa kauzibe katika penzi lao na Herode.

Mtume Paulo alichukiwa sana na wagalatia kutokana na maudhui ya mahubiri yake kuwa ya kweli. Hakuna mtume aliyekuwa na maadui wengi kama Paulo soma wagalatia 4:16 Paulo analalamika kuwa kwa nn watu wanamchukua na kumfanya adui yao kwa kusema ukweli?

Yeremia aliwahi kuingia kwenye mzozo na viongozi wa Dini kwa kusema ukweli, walimshtaki na kutaka auawe kabisa kwa kuwa alisema kweli Soma Yeremia 26 mstari wa saba.

Timotheo rafiki yake mkubwa na Paulo, kwa wale ambao walikuwa hawajui Timotheo alikuwa amefungwa na Paulo Gereza moja ila baadaye alitangulia kutoka. Mara kwa Mara alikuwa akienda kumsalimia Paulo Gerezani ndiye aliyekuwa akichukua barua za Paulo kwa makundi mbalimbali ndio hizi zinazoitwa Waraka za Paulo.

Paulo aliwahi kumwandikia yeye Mwenyewe Timotheo barua (Waraka) katika barua hiyo Sura ya tatu Paulo anamwambia Timotheo kuwa mtu akitamani kazi ya uaskofu atamani kazi njema, awe ni mtu asiyelaumika, Mume wa mke Mmoja, mwenye kiasi na busara, asiwe mwenye kupenda fedha, asiwe mlevi, hapa Paulo aliwaasa kweli tabia za viongozi wetu wa Dini....

Ole Mushi
0712702602.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom