Viongozi wa kiroho mnatakiwa kuheshimu chaguo zetu za maisha.

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
271
484
Ndugu zangu, salaam.
Binafsi nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa zawadi ya uhai.

Nilibahatika kukutana na video niliyoambatanisha na ilinikwaza nafsi yangu mpaka nikafikia kuandika humu labda itamfikia mhusika.

Kama mwanaume nimekuwa katika mausiano na mwenzangu kwa zaidi ya miaka 13 sasa. Katika kipindi chote hiki tukiwa wapenzi, baadae kuwa wanandoa, nilijiapiza kutofanya mahusiano nje ya ndoa na kutofanya mapenzi na mtu zaidi yake. Niliweka nadhiri hii na yeye, lakini zaidi niliiweka na nafsi yangu.

Siyo kwamba sikuwahi kupata matamanio au vishawishi katika kipindi hiki chote, isipokuwa niliamua kutoendeshwa na mwili, bari niendeshwe na akili pamoja na utashi.

Katika muda huu wote nimeishi maisha ya amani siyo na mke wangu pekee hata na nafsi yangu, huwa najisikia vizuri sana ninapomwambia "Nakupenda sana Mke wangu" huku ikitoka Moyoni bila makando kando.

Kukutana na video hii na nyingine zenye kujiapiza kwa haiwezekani mwanaume kuwa mtulivu kwa mke wake mmoja nikutukosea heshima tulio chagua kuwa wakweli kwa wenzetu. Binadamu ni dhaifu, mwenzio anaweza anza kukutilia mashaka pale unaposisitiza kuwa ni yeye tu katika nafsi yako.

Niwashauri wanaume wenzangu, hata kama inachekesha au kusema baadhi ya ukweli, tusiisambaze kwa mstakabari wa watoto wetu wa kiume tunaowalea.

Mwisho, tuwe wakweli kwa wake zetu na wapenzi wetu na tuwapende bila kutegemea chochote toka kwao na tutaishi kwa amani isiyokuwa na kipimo.

*HAIJALISHI YEYE ANAFANYA NINI, KAMA NAFSI YAKO NI NYEUPE, BASI WEWE NDIYE MSHINDI*
 
Daaah,wewe kaka,,,nimekupenda bure.. Mungu akubariki sana ,,hapa wanaume wengi watakushambulia ila huu ndo ukweli... Wanaume wastaarabu na wanaojiheshimu wapo. Hongera sana Mungu azidi kukuwezesha
 
Yaani ungekua karibu ningekupa zawadi maana umeweza kujua kusudu la Mungu kua na mke na mme mmoja ndio maana aliumba adam na hawa na si adam na hawa na adija nooooo
 
Ili jambo la kutulia na mmoja limenishinda kabisa japo linawezekana hongera mkuu kwa kifanikisha
 
Ndugu zangu, salaam.
Binafsi nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa zawadi ya uhai.

Nilibahatika kukutana na video niliyoambatanisha na ilinikwaza nafsi yangu mpaka nikafikia kuandika humu labda itamfikia mhusika.

Kama mwanaume nimekuwa katika mausiano na mwenzangu kwa zaidi ya miaka 13 sasa. Katika kipindi chote hiki tukiwa wapenzi, baadae kuwa wanandoa, nilijiapiza kutofanya mahusiano nje ya ndoa na kutofanya mapenzi na mtu zaidi yake. Niliweka nadhiri hii na yeye, lakini zaidi niliiweka na nafsi yangu.

Siyo kwamba sikuwahi kupata matamanio au vishawishi katika kipindi hiki chote, isipokuwa niliamua kutoendeshwa na mwili, bari niendeshwe na akili pamoja na utashi.

Katika muda huu wote nimeishi maisha ya amani siyo na mke wangu pekee hata na nafsi yangu, huwa najisikia vizuri sana ninapomwambia "Nakupenda sana Mke wangu" huku ikitoka Moyoni bila makando kando.

Kukutana na video hii na nyingine zenye kujiapiza kwa haiwezekani mwanaume kuwa mtulivu kwa mke wake mmoja nikutukosea heshima tulio chagua kuwa wakweli kwa wenzetu. Binadamu ni dhaifu, mwenzio anaweza anza kukutilia mashaka pale unaposisitiza kuwa ni yeye tu katika nafsi yako.

Niwashauri wanaume wenzangu, hata kama inachekesha au kusema baadhi ya ukweli, tusiisambaze kwa mstakabari wa watoto wetu wa kiume tunaowalea.

Mwisho, tuwe wakweli kwa wake zetu na wapenzi wetu na tuwapende bila kutegemea chochote toka kwao na tutaishi kwa amani isiyokuwa na kipimo.

*HAIJALISHI YEYE ANAFANYA NINI, KAMA NAFSI YAKO NI NYEUPE, BASI WEWE NDIYE MSHINDI*
View attachment 1075670

Uliemnukuu dini yake haiamini katika roho, kwa hiyo huyo si kiongozi wa kiroho.
 
Du mi sifanyi makusudi nahisi nmerogwa nmejaribu kufanya ivo nmeshindwa.Japo sio mtu wa totoz ila siwezi nikajiapiza kwamba nitakaa njia kuu.wife nampenda Ila kuna emergency zingine zinakuja mara mojamoja hasa kikazi lazima tu nta do.
 
Mie nilijaribu ila siwezi na lawama zote nazipeleka kwa fweza

Yani hata nikitulia mwezi mzima NIKIPATA MSHAHARA TU naanza kuona mademu wazur wazur wengi tofaut na waifu
 
Ukilibeba nafsini utafanikiwa bro.
 
Mie nilijaribu ila siwezi na lawama zote nazipeleka kwa fweza

Yani hata nikitulia mwezi mzima NIKIPATA MSHAHARA TU naanza kuona mademu wazur wazur wengi tofaut na waifu
imebidi nicheke, kwamba ukiwa umepigika unakuwa mwema sana kaka? Anyway, jitahidi utaweza.
 
Back
Top Bottom