Viongozi wa kijiji mbaroni kwa wizi wa milioni 16 za umma

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita, wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.

Mwanri alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa, viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42) kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).

Kamanda huyo alisema "Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma."

Alieleza kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.

Alisema, fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka yaliyopo kijijini hapo.

Alifafanua kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani zilipokwenda.

Kamanda Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili.
 
Ulivyo mnafiki na uzi wako huu umeamua kuandika kwa maandishi kiongozi mmoja aliyetokea Chadema ila hao watatu wa ccm hukutaka kuwataja kwa vyama vyao,,,kama amekula pesa za umma hata kama katokea chadema tunaomba atajwe kwa jina na hatua kali zichukuliwe ndo tunachokitaka wananchi,,,,ila mtoa maada amejaa unafikki tena sana maana kati ya hao wamo viongozi wa ccm watatu,,be fair with country unless otherwise time will tell u!!!!!
 
Wanatoa agizo la kukamata wadogo mbona wenyewe hawakamatani?.wanakubaliana kurudisha fedha walizo iba.bila kuwajulisha watz ni kiasi gani kimerudishwa kama ni kweli zinarudishwa.
 
Ulivyo mnafiki na
uzi wako huu umeamua kuandika kwa maandishi kiongozi mmoja aliyetokea
Chadema ila hao watatu wa ccm hukutaka kuwataja kwa vyama vyao,,,kama
amekula pesa za umma hata kama katokea chadema tunaomba atajwe kwa jina
na hatua kali zichukuliwe ndo tunachokitaka wananchi,,,,ila mtoa maada
amejaa unafikki tena sana maana kati ya hao wamo viongozi wa ccm
watatu,,be fair with country unless otherwise time will tell
u!!!!!

si uwataje hao wa ccm kama unawajua!
 
Kama kweli wametafuna hela no msamaha wafungwe tu na kuchapwa viboko ikiwezekana
 
Ulivyo mnafiki na uzi wako huu umeamua kuandika kwa maandishi kiongozi mmoja aliyetokea Chadema ila hao watatu wa ccm hukutaka kuwataja kwa vyama vyao,,,kama amekula pesa za umma hata kama katokea chadema tunaomba atajwe kwa jina na hatua kali zichukuliwe ndo tunachokitaka wananchi,,,,ila mtoa maada amejaa unafikki tena sana maana kati ya hao wamo viongozi wa ccm watatu,,be fair with country unless otherwise time will tell u!!!!!

Kumbe kwenye kula huwa wanaungana! Kwenye kula kunakuwa hakuna kupingana?
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Yeyote anayekula mali ya umma na awajibishe kwa mujibu wa sheria
 
Wanajf,m/kiti wa kijiji anatunza hela ya kijiji?hakuna kesi hapo ni propaganda za siasa...ule ni ukanda wa chadema
 
GEITA, TANZANIA
Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita, wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.

Mwanri alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa, viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42) kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).

Kamanda huyo alisema “Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma.”

Alieleza kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.

Alisema, fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka yaliyopo kijijini hapo.

Alifafanua kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani zilipokwenda.

Kamanda Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili.
 
GEITA,
TANZANIA

Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na
upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani
Geita, wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa
kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA),
wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na
upotevu wa fedha hizo.
....

Hapo ndio bado hawajapewa Nchi! itakuwaje wakipata ridhaa ya wananchi? wezi!
 
Wanaharakati kiboko wakituhumiwa CCM ni mafisadi wakitihumiwa Chadema ni propaganda, sijui kama wanaharakati wanajua maana ya meneno hayo, hata Slaa kuiba mke mtu tuliambiwa ni propaganda!

Chama

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Wakiwa wa chadema wanakamatwa mara baada ya agizo, wangekuwa magamba ungeona kama wangekamatwa, hata hivyo bado ni watuhumiwa, inaweza kuwa c kweli kwamba wamekula pesa, kama wamekula sheria ichukue mkondo wake.
 
Hao wengine lazima ni CCM. Siyo kwamba chadema hamna wezi ,tofauti na ccm ni kwamba kwa chadema wezi wanashughulikiwa na chama wakati ccm wezi wanapongezwa
 
Mwandishi ameandika habari kiukuda sana,mbona hao Magamba hujawataja? mijizi ya Mabilioni yanadunda mtaani yakiwemo yanatoa order kukamatwa kwa hawa viongozi wa CDM
 
Hawa ndio wanataka tuwape nchi si watabakisha magofu matupu..mtu kama Lema umkabidhi wizara ya ujenzi pesa zote za miradi anatafuna.
mimi naona unamtaka sana mwandikie barua akuoe uishi nae kabisa!
 
mwanri ni mw*hu,.anakamata dagaa anaacha kambale,kama ameiba huyo mmoja wa chadema akamatwe,mwizi ni mwizi tu,mbona hayo magamba mengine huyataji
 
Chadema.jpg

Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita, wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.
Mwanri alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa, viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42) kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).
Kamanda huyo alisema "Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma."
Alieleza kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.
Alisema, fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka yaliyopo kijijini hapo.
Alifafanua kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani zilipokwenda.

Kamanda Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kwani katika wizi huo CCM hawapo ????
 
Back
Top Bottom