Viongozi wa Kiislamu wajitoa suala la madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa Kiislamu wajitoa suala la madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, JULAI 12, 2012 04:24 ELIZABETH MJATTA NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

  *Wadai hawaonyeshi dalili za kutaka usuluhishi
  *Watishia kuwafikisha mahakamani waliogoma

  VIONGOZI wa Baraza la Kiislamu Tanzania (BAHIKITA) wamejitoa katika kushughulikia suala la mgomo wa madaktari kwa kile wanachodai kuwa madaktari hawaonyeshi dalili za kutaka suluhisho.

  Baraza hilo kupitia Katibu wake, Said Mwaipopo pia limesema linajadiliana na wanasheria wake kuangalia namna ya kuwafungulia mashitaka ya mauaji madaktari wote walioshiriki katika mgomo ambao umesababisha vifo vya wagonjwa katika Haspitali ya Taifa ya Muhimbili.

  “Sisi tuliingilia kati mgomo huu kwa nia njema ya kutapata suluhu kati ya madaktari na serikali…lakini baada ya taarifa zetu kutoka kwenye vyombo vya habari Ikulu ilitoa tamko la kukataa kukutana na sisi

  “...lakini Ikulu walieleza vizuri kwamba hawajawahi kukataa kukutana na viongozi wa madaktari kwa maana hiyo basi serikali imeonekana dhahiri kutaka suluhu.

  “Baada ya taarifa hizo sisi tuliwatafuta viongozi wa MAT ambao tuliwaeleza kwamba kutokana na taarifa hizo wao waombe msamaha kwa serikali na umma wa watanzania kwa kuendesha mgomo ambao umesababisha vifo.

  “Lakini baada ya kuwaeleza hivyo hawa viongozi wa MAT hawakukubali…sisi kama viongozi ambao lengo letu ilikuwa kutafuta suluhu tukaona hawa vijana (madaktari) wana nia mbaya.

  “Lakini sisi si kujitoa tu bali tutawafungulia mashtaka ya mauaji wote walioshiriki katika mgomo huo. Tutafanya hivyo ili fundisho kwa wengine ambao wana nia kama za madaktari wanaoendesha migomo.

  Kwa hiyo sisi tunaunga mkono kufikishwa mahakamani kwa Rais wao ni njia sahihi kabisa ya kurudisha nidhamu, lakini pia tunaunga mkono matamko yote yaliyotolewa na serikali dhidi ya madaktari,”alisema Mwaipopo.

  Akijibu hoja hizo, Katibu wa MAT, Dk. Edwin Chitage amesema hawaogopi kufikishwa mahakamani na kwamba wao waliwapokea viongozi hao kwa nia njema wakiamini ni viongozi wa dini.

  “Kama wamesema watatufikishwa mahakamani wao waende halafu tutakutana nao…sisi tuliwapokea kwa nia njema kabisa kwa sababu walituomba wenyewe..lakini baada ya kikao cha Jumamosi siku ya Jumapili wakatupigia simu kuomba tukutane nao,sisi tulikutana nao lakini cha kushangaza walitueleza kwamba wamepigiwa simu na mtu wa Ikulu akiwataka kutuambia kwamba inabidi tuandike barua ya kuomba msamaha halafu tuwape wao ili waipeleke…sisi tulishangaa jambo hili… sisi hatutafanyi kazi hiyo,” alisema Dk.Chitage.

  Wakati huohuo, siku moja baada ya Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi kufikishwa mahakamani kwa madai ya kuchochea mgomo, chama hicho kimesema hali hiyo imewashtua na lolote linaweza kutokea.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa MAT, Dk. Edwin Chitage alisema hali hiyo imeongeza hasira na kushusha morali wa madaktari.

  “Kweli hiki kitendo cha Dk. Mkopi kufikishwa mahakamani kimetushtua na ukweli kimesababisha kuwepo na fukuto la chinichini.

  Madaktari wamekatishwa tama… lakini kitendo hiki pia kimeshusha morali ya wale ambao walirudi kazini…kwa hiyo wapo madaktari ambao wapo kazini kwa maana ya eneo la kazi lakini wanachokifanya hiyo wanajua wao,”alisema Chitage.

  Akizungumzia suala la madaktari wa walioko katika mafunzo (Interns) 390 kufutiwa leseni alisema kitendo hicho walikitegemeakilitegemewa na hakikuwashtua kwa sababu ni kitu ambacho tayari kilipangwa.

  “Kwetu sisi tulitegemea jambo hilo kwa hiyo hatukushtuka sana…kwetu hiki ni kitu kidogo sana, kwa sasa viongozi wa Interns wanafanya kikao na wanasheria wao wanaangalia jinsi uamuzi huo ulivyotolewa na baadaye tutakutana nao kwa ajili ya kuangalia ni namna gani tutalifanyia katika suala hili,”alisema Dk. Chitage.

  Akizungumzia hali ya Dk.Stephen Ulimboka alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na ameanza kutembea na kufanya mazoezi vizuri.

  “Hivi sasa hali yake imeanza kuimarika. Anaweza kutembea na anafanya mazoezi yake vizuri.

  “Kinachoendelea kumkalisha hospitali ni uangalizi wa karibu wa figo…lakini ingekua si figo angekuwa amesharudi nchini,” alisema.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Baada ya Vasco Da Gama kugoma kuonana na Viongozi wa Chama Cha Wanahabari Waislamu Ikulu

  Wakatishia kuwashitaki Madaktari Mahakamani; nadhani wakaona hiyo haina Misuli baada ya Vasco kutowaona

  Wameamua kujitoa kabisaaaa na kuingia mitini... hiyo ni bora ilikuwa sio kazi yao...
   
 3. A

  Alhabaad Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Said Mwaipopo na Msopa washakuwa viongozi wa kiislam?hawo jamaa nawajua km pesa ni matapeli wakubwa!Kwanza hakuna taasisi ya kiislam inayoitwa Bahakita!ilo ni jina wamejitungia tu kwa kuwaibia waislam.watu km hawa ndio wanautukanisha uislam.Huyo Said Mwaipopo ashawahi kwenda congo akaritadi akatembezwa congo na maaskofu wakitangaza Shehe kutoka Tanzania kauona ukweli kaingia ktk ukiristo leo eti kawa Kiongozi wa waislam!!!!????
   
 4. a

  afwe JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  By the way wao ni akina nani katika nchi? Nani anatakiwa kumaliza mgomo wa madaktari? Bila shaka ni serikali na madaktari kama sio wananchi kwa ujumla bila kujigawa katika makundi yenye kutaka sifa zisizo na maslahi kwa taifa letu
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nashangaa viongozi wa dini wengine wanapokosa mambo muhimu ya kushughulikia na kuishia kuwa mbele ya microphone kila wakati kama vile wao ni MCs.

  Viongozi wa dini walitakiwa kusaidia kuondoa tofauti baina ya madakatari na serikali kwa kutumia nguvu yao ya ushawishi lakini sasa hawa wanageuka kuwa serikali ya kuwashitaki madakatri; huku ni kama kuchochea mgomo huo zaidi. Mashtaka ya jinai (mauaji) yanafanywa na serikali, iweje leo mashehe ndio wayafanye?

  Upuuzi mwingine hauhitaji hata kisomo cha ngumbaru kuachana nao.
   
 6. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Wanajikomba kwa serikali wala si viongozi wa waisilam. Tatizo la waislam kila mtu akiibuka kwa masilahi yake anajiita kiongozi. Mbona viongozi wa waislam twawajua!
   
 7. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hata mimi imenishangaza kuibuka ghafla na kusema "Tunaunga mkono matamko yote yaliyotolewa na Serikali",,Viongozi wa Waislam,,,Uislam unaingiliwa hakika! "Tunawasiliana na wanasheria wetu" pheeeeeew!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Afadhali sana umenisaidia kuelewa jambo lililopo mbele yetu kwa uwazi zaidi; nililielewa kijuujuu kwa kulisoma tu.
   
 9. share

  share JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Tukisema "hawana akili" watajibu kwa hasira na majambia mkononi eti tumewatukana! Ukweli ni kwamba uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo mno! Aaah! kumbe jamaa wa magogoni ni muislamu!!
   
 10. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hawa waislamu tangu walipojishushia hadhi na tamko la "hijabu", hawana credibility tena!
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
  Ufisadi unauwa watu wengh kuliko migomo, mbona hawakuwahi kufungua hata kesi moja?
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wanamtetea Alhaj mwenzao wa ikulu kwani kumsema vibaya ni dhamb
   
 13. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi waislamu hawana utaratibu wa kutoa taarifa? Au kila anayejisikia anakurupuka tu? Hizi habari mbona kama siyo za waumini na ni kama za wanasiasa waliofilisika kama wana CCM?
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa ni waganga njaa tu wala sio wasemaji wa waislam.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu kibaya kama mtu mzima kutumiwa......... Nia yao ilikuwa nini? Umaarufu? Walipewa mpunga?

  Yaani mtu mzima unatumwa halafu bila kutafakari unayabeba uliyotumwa na kuwaamuru madaktari wayafuate?

  Ama kweli heri unyimwe pesa lakini upewe akili........ Ndo maana kila siku wanatumiwa na kutupwa kama karatasi za chooni.......
   
 16. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Tatizo hii nchi tunawatukuza sana viongozi wa dini, as if walichaguliwa na waumini wao kuwa mawaziri.
   
 17. sister

  sister JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  wangefanikiwa wala usingesema hayo maneno.
   
 18. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wapendao kusifiwa ndivyo walivyo. WAANGALIENI MIISHO YAO TU, aibu tupu. Wameona hakuna dili kwa madaktari. Nadhani pia Hawauguagi hawa.
   
 19. w

  wakitei Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama kawaida yao hawana jipya wao kila kitu wanapenda kulalamika hoja zao ni pumba tuu angalia ohh tunaonewa serikali yote inaongozwa na wakristu matokeo yake wanachukua MADARAKA angalia uupuzi wao TISA KUMI ASILIA 99 YA DOCTOR WOTE NI wakristo andamaneni basi kulipinga na hilo na kama haitoshi andamanani tena kuwapeka madrassa
   
 20. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyu Mwaipopo aliwahi kuukana UISLAMU na kujiunga na UKRISTU. Waliwahi kuendesha mihadhara ya kuchambua Quran na Biblia ktk viwanja vya Furahisha Mwanza. Mwaipopo akiwa upande wa wakiristu (biblia). Nakumbuka huo mhadhara uliisha kwa WAISLAMU NA WAKRISTU kupigana, kabla ya FFU kuingilia kati. Kumbe amesharudi tena kwenye UISLAMU?

  Mimi ninafikiri UUMINI wa MWAIPOPO unategemea na mtu aliyeko MAGOGONI kwa wakati huo. Sitashangaa kama 2015 akija wa dini nyingine basi Mwaipopo atahamia DINI ya huyo atakayeingia Magogoni.

  Kweli Bongo sarakasi!
   
Loading...