Viongozi wa kiislamu kumkumbatia kikwete ni dhambi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa kiislamu kumkumbatia kikwete ni dhambi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAZETI, May 24, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kwa mtu kumkosoa kiongozi wa Imani yake hata pale anapofanya makosa ya wazi katika jamii. Lakini naamini kwa hili Mungu yuko pamoja na mimi, Kinachofanywa na viongozi wa dini ya kiislamu sasa hivi ni wazi kuwa viongozi hao wamenunuliwa. 1. Nieleze wazi kuwa mimi sio mshabiki wa CHADEMA 2. Mimi sio mshabiki wa CCM 3. Nilikuwa mshabiki mkubwa wa CUF lakini kwa sasa nimeamua kukaa pembeni kwa sababu ambazo kwa sasa sitaki kuzieleza hapa jukwaani.


  DHAMBI YA KUMKUMBATIA KIKWETE.
  1.Ni wazi kuwa Kikwete ni kiongozi muovu asiyejali na asiyejua haki ni nini. Mtu asiyejali haki ni dhalimu na uislamu unatukataza kuwakumbatia wanaodhulumu na kututaka tuwatetee wanaodhulumiwa hata kama sio waislamu.


  2. Dhambi nyingine ninayoiona hapa ni kuwa kuna mazingira yanayotia wasiwasi kuwa viongozi wa kiislamu mmepewa rushwa ili muweze kumtetea Bwana mkubwa huyo kwa kuitisha makongamano yanayochochea chuki za kidini. MUOGOPENI MUNGU HAKIKA MUTAULIZWA JUU YA MUNAYOYAFANYA.


  3. Kikwete sio muumini wa kweli, kuingia msikitini mara moja moja na kuteua viongozi wenye majina ya kiislamu hakumfanyi kuwa mtu muhimu wa kutetewa na viongozi wa kiislamu.


  4. Naomba mufahamumu kuwa miongoni mwa watu wanaoumizwa na kudhulumiwa na kikwete ni pamoja na waislamuwenyewe. Kwa hili nina mifano mingi lakini naomba nitoe mfano mmoja tu. Karibu asilimia 95 ya wakulima wa korosho ni waislamu, mwaka huu kikwete kwa kushirikiana na watendaji wake wa wilayani na mkoani amehusika kwa kiasi kikubwa kuwadhulumu wakulima hao korosho zao, wakulima waliamua kuunda kikundi chao na kuachana na mfumo ambao ulipendekezwa na Rais pamoja na waziri mkuu. Katika mfumo huo mkulima alikuwa analipwa Tsh 800, lakini wakulima walipoamua kuanzisha umoja wao kwa mara ya 1 wakauza Tsh 1,800. Dhuluma kubwa iliyofanywa na Kikwete ni kuwaagiza watendaji wa ngazi ya wilaya na mkoa kuuzuia umoja huo kukusanya korosho za wakulima hao. Mateso na mashaka makubwa yaliwakuta wakulima hao baada ya kitendo hicho cha muheshimiwa huyo ambaye binafsi namuweka katika kundi la WANAFIKI.


  3. Kuteua viongozi wasio na sifa kwa maslahi yake binafsi na si Taifa. Bi Sofia Simba alimfukuza Husna Mwilima ndani ya UWT (Hongera mama) baada ya kumuona hafai. Ni kweli alikuwa hafai. Katika hali isiyokuwa ya kawaida Bi Husna Mwilima akateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Tandahimba. Uovu na ubaya anaoufanya Tandahimba, nendeni mkawaulize wananchi wa kule. Ni kiongozi mbaya, muhuni na asiye na sifa hali inayopelekea wananchi kudhani kuwa ni hawara wa kikwete.


  Viongozi wangu MUOGOPENI MUNGU. Mmehusika kusambaza waraka ambao umetengenezwa na ccm ukionyesha kuwa Viongozi wa kikiristu wamewaita wachungaji na kuwataka wote wamchague Dr. Slaa kwa manufaa ya dini yao, Inawezekana lakini si kwa ule waraka. Kama unatumia akili ni wazi kuwa ule waraka umetengenezwa na kitengo cha Tambwe Hiza.
  Mwisho nataka kuwaambia kuwa ni bora kumchagua kiongozi ambaye si muislamu lakini ni muadilifu, kwani mtume wetu aliwahi kuwaambia waislamu waende kwa Mfalme wa Ethiopia ambaye alikuwa mkristu lakini ni Muadilifu. Kama hakuna kosa lililofanywa na Dr. Slaa kwa waislamu kwanini iwe dhambi kumchagua? Mimi sio Mshabiki wa Dr. Slaa kwa sababu zangu binafsi lakini si za kidini. Kama anafaa wanaompenda wamchague. Mwisho waombeni radhi waislamu kwa kuwataka wamchague kiongozi huyo muovu.
   
 2. M

  MPG JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi najua wanawatumia kwsababu wanajua wanaelimu NDOGO,ni watu ambao hawapo organized,CHA KUSHANGAZA WAISLAMU NITANGIA LINI WAKAWA RAFIKI WA CCM?kwa njia hi waislamu hawatakuja kuwa na maendeleo mana wao wanatumiwa,kuna matatizo mengi ya waislamu ambayo viongozi wao wanatakiwa kuyatatua na si kutumiwa na CCM kutetea maovu yao
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Respect mkuu!
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  "Siku zote hapa duniani usipojua unahitaji nini ili ufike wapi, wejanja watakutumia kama big-G wanakutafuna kwa faida yao ya kupata utamu na utamu ukiisha wanakutema.... Wao wamepata utamu wewe umekosa ule mvuto ulokuwa nao sababu ya ule utamu!!!" - Mtazamo tu!!
   
 5. z

  zamlock JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kaka kama wewe ni muislamu basi umesoma na unajua nchi yako nini kinatakiwa kufanyiwa ili iwe na maendeleo safi sana ndugu
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Hapo mtoa mada amenena, mashaka yangu ni kwa wale wafiadini wakija hapa patachimbika. Ila nimekugongea thanks.
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, na tuwe wakweli JK uwezo wake ni mdogo sana kuongoza nchi hii, Halafu si hivyo tuu hata washauli wake wa karibu ni VILAZA! Nasikitika sana kuwa ccm wameishiwa kiasi hicho wako wapi akina MKAPA, MWINYI, PHILIP MANGULA,
   
 8. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Waislam ni watu wazuri kweli wakipata shule.mfano waturuki hawa jamaa wako smart kweli uchumi ,jeshi na uongozi bora Wako G20.ole wake ndugu zetu hawa wakose shule!Chuki zake mfano somalia! Ila kama muslim mnamsapoti kikwete sababu ya dini !mtakuwa mabwege!ninampenda Salim Ahmed salim smart leader i wish he could be my Presidend kuliko huyu muuza Sura!
   
 9. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,473
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Labda ile rushwa ya kujengewa misikiti inawaponza
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mashekhe wetu ndio wanaotuzalilisha na kuonekana kama sisi Waislam hatukusoma kumbe sio hivyo kabisa, Sisi Waislam tumesoma na tunalipenda Taifa Letu, ila baadhi ya Mashekhe ndio wanaotudhalilisha kwenye Jamii ya Kitanzania kwa ulafi wao wa kununuliwa na Mafisadi Hasa Kikwete na Majambazi wenzake wanoa tuibia Rasilimali zetu kwa kuwafisadi Viongozi wetu wa Kiislamu.

  Kwa mimi ni Muislam na Sikubaliani na Kikwete kabisa jinsi anavyoiendasha nchi, sikumpenda Tangua 2005 na likuwa na juwafika kuwa Its National Disaster Kumchagua Kikwete bora ya Salim A Salim anauwezo kuliko Fisadi Huyu, alipotufikisha ni sehumu mbaya sana.

  Dr.Slaa Nimemkubali kuwa anao uwezo wa kuliongoza hili Taifa kuliko Kilaza Kikwete, Na nina amini kuwa Kikwete 2010 Hakushinda Uchaguzi bali aliiba akishirikiana na Kamati yao ya NEC kumuibia Dr.Slaa ambaye wengi wao au wetu tunaamini ndie Rais wetu wa ukweli, kwani hata Mungu anakaza wizi na Rushwa lakini Kikwete sio Muslam wa Kweli bali ni MNAFIKI NA ANATUDHALILISHA SISI WAISLAM na hatutokubalikudhalilishwa kwa ajili ya Mtu mmoja.
   
 11. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Natamani Dr Salim A Salim ndie angekuwa kiongozi wetu kama sio Dr.Slaa.. jamaa anaonekana ni smart sana katika maamuzi,sielewe ni nini hasa alichowafanya CCM hadi wawe wanambagua namna hii,mie naona jamaa ndie mwana mapinduzi wa kweli katika upande huo..tho ninawiwa kusema kuwa mpaka sasa haonekani kuwa na itikadi za kichama...jamaa anafaa, Mashekhe wetu ningewaona wa maana kama walau wangetambua uwepo wake wakati alipoonyesha nia ya kuliongoza taifa 2005.
  Allah amjalie mtu huyu barka tele
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kweli nimeamini wewe Gazeti la Udaku
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,029
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Toa sababu tafadhari.
   
 14. m

  mzambia JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Always be the changes you want to see and not the one to see the changes.
   
 15. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Avatar yako tu inanifanya nikuelewe u mtu wa namna gani. Si vizuri kuendelea kuyafumbia macho mambo yanayoturudisha nyuma na kutufanya tuwe na Taifa lenye kutegemea misaada kutoka kwa wahisani ambao wanadhulumu mali zetu kwa kushirikiana na manyapara wao.
   
 16. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Kama ningesema gari lake liliwahi kukamatwa mitaa ya Ohio alipokuwa anatafuta Changudoa wakati Makamba alipokuwa mkuu wa mkoa DAR huo ungekuwa ni udaku maana si kweli, narudia tena maana si kweli kwa sababu yeye ni mtu mwenye heshima zake bwana tena anajali ndoa!
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Lete aya kusaidia mada yako.
   
Loading...