battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,672
- 2,540
Imekuwa ni jambo la kawaida kutoka habari za ubadhirifu kwa viongozi wa Kiafrika.
Kila kiongozi anapotolewa madarakani kwa nguvu ya umma au mapiduzi ya kijeshi au kushindwa kwenye uchaguzi halali katika ballot boxa basi siri hufichuka jinsi gani viongozi wetu walivyokuwa malimbukeni wa kujikusanyia mali binafsi.
Sijui wana hofu kuwa pension haita watosheleza? Ni viongozi hao hao huwapigia wananchi mbiu ya kuongeza juhudi ya kazi ili nchi iweze kujitegemea na huku wakiranda duniani kutafuta usaidzi wa kimaendeleo.
Lakini la Kushangaza ,kila kukicha nchi zao zina didimia kwenye dimbwi la umasikini na ugumu wa maisha. Imekuwa hivyo kwa nchi zote za Afrika, hata kule Afrika ya Kusini hali ni mbaya zaidi,tena la kushangaza wale waliojiita wakombozi ndo hao hasa wanaoponda mali za nchi ,huku wakiwaachia jamii ya Kiafrika ikiogelea kwenye umasikini kila uchao.
Jacob Zuma ni wa mfano huo. Ama kule Zimbabwe Ndo siri imeibuka hivi karibuni ,kumbe Mugabe alikuwa na Cash isiyopungua $10 Milioni, Mashamba makubwa na majumba mbali mbali ya kifahari. Wakati yeye kawanyanganya Wazungu mashamba yao na kuwagawia wazalendo ekari 3 kila kaya ili wajisaidie.
Kumbe yeye ndo kawa Mzungu kwa kujimilikisha maelfu ya ekari. Hatimaye nchi yake imekumbwa na upungufu mkubwa wa chakula na uchumi kufa kabisa.
Ninachojifunza hapa, hawa viongozi wanatawala viumbe wajinga? Basi vipi wale wanao walinda(Jeshi) na kufanya uhuni huu nao hawana hisia? Basi hata wale marafiki basi wa nchi jiraniu hawawezi kuwaasa mienedo yao hii? Wazungu nao pia huwa wanayajua haya ,Mbona na o Huufyata Kimyaa hadi pale wanapotolewa madarakani? Kulikoni? au na wao wazungu hufaidika kwenye wizi huu?
Hebu chungulieni hapa habari ya Mugabe, Robert Mugabe died with $10m in cash and several houses, but left no will
Kule Sudani bado habari hazijatoka, lakini kule Kongo mnajuwa Mabutu Sese Seko alivyoikausha nchi. Hapa Zanzibar yasemekana,Waziri fulani wa fedha zama za Karume Mzee aliweka pesa nyingi nje, kule India na alipokufa Serikali ilizidai zile fedha,lakini serikali ya india ilikataa kuzitoa kesh,bali iliiwalazimisha wanunue bidhaa, ndio ukaona magari ya aina ya Tata hadi miaka ya karibuni na Vespa zilikuwa zinaletewa, na serikali ya Zanzibar ilianzisha shirika la kuuza magari na mengine yalitumika kama magari ya umma.Hii ikiwa kama ni sehemu ya fidia ya pesa Zile zilizoibwa .
Afrika na umasikini wa kudumu,viongozi kukwapua ,nani wa kulaumiwa?
Nawakilisha

The first official list of assets to be made public says the late Zimbabwean dictator left behind $10 million - AP The wealth of Zimbabwe's former longtime president Robert Mugabe was long a mystery. Now the first official list of assets to be made public says he left behind $10 million and several houses when he died in September. Some in Zimbabwe view that estate as far too modest for Mugabe, who ruled for 37 years and was accused by critics of accumulating vast riches and presiding over grand corruption. The report by the state-run Herald newspaper on Tuesday does not mention any overseas assets, though it is thought that Mugabe had properties in neighboring South Africa and in Asia. The report says there appears to be no will, though lawyers are still looking for one. The report cites the lawyers as saying the law stipulates that Mugabe's wife, Grace, and children will inherit the property in that case. Mugabe also left behind a farm, 10 cars and 11 hectares (27 acres) of land that included an orchard at his rural home where he was buried. His daughter, Bona, registered the estate on behalf of the family, the report said. |