Viongozi wa Kamati ya Maji Geita watiwa mbaroni kwa ubadhilifu wa pesa

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
753
3,096
Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia viongozi watatu wa kamati ya jumuiya ya maji inayosimamia mradi wa maji wa Mharamba uliopo wilayani Geita, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha wanazokusanya kwa wananchi kwa kuwauzia maji kwa kipindi cha miaka sita.

Baada ya waziri kuvuja jumuiya hiyo Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Joseph Musukuma ameomba viongozi hao wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengine huku mkuu wa wilaya hiyo akiagiza kamati ya ulinzi kuwakamata kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Yaani watu unapiga hesabu milioni 20 halafu wana laki tano halafu wanachekacheka namna hii, mimi ni mbunge na tunamuheshimiwa DC hawa watu lazima watoe hesabu kama hawana kamata hatuwezi kuwa wapole hivyo, lazima washughulikiwe hawa wezi kama wezi wengine,” amesema Mhe. Msukuma.

Mradi wa maji wa Mharamba umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na ulikabidhiwa kwa kamati hiyo mwaka 2015 na unakadiriwa kuhudumia wananchi zaidi ya 4,000 wa kata ya Nkome.

Mbali na hilo waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea mradi wa maji Mharamba katika jimbo la Geita vijijini na kuridhishwa na maboresho yaliyofanyika na kupelekea vituo vilivyokuwa havitoi maji kuanza kutoa huduma.

Waziri Aweso ametoa maagizo kuwa vituo 3 vilivyobakia vianze kutoa huduma katika kipindi cha wiki mbili ikiwa ni pamoja na kufanya upanuzi wa mradi huu mkubwa pamoja na kuwaunganishia wananchi majumbani.
Mradi huu una jumla ya vituo 20 na kwa sasa jumla ya vituo 17 vinatoa huduma kutoka katika tanki la lita 135,000.

Aidha Mh.Aweso amezitaka kamati za maji vijijini kuweka utaratibu mzuri wa matumizi na ukusanyaji wa fedha kutokana na uwepo wa baadhi ya kamati kufuja fedha zinazokusanywa kwenye miradi.

Aweso ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Wilayani #Geita kwenye kijiji cha Mrahamba ,Kata ya #Nkome.
Kufatia uwepo wa taarifa kutokuwa sahihi ya kamati ya Maji kijiji cha Mwaramba kwenye suala la makusanyo.

kahama.jpg

Chanzo: Bongo5
 
Back
Top Bottom