Viongozi wa juu wakiwa kigeugeu wa chini itakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa juu wakiwa kigeugeu wa chini itakuwaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akili, Jun 8, 2010.

 1. a

  akili Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anazindua mabasi ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi amesikika akisema yeyote anayetaka kuchangia mabasi kama hayo ana uhuru wa kupaka rangi yoyote anayotaka gari zima.
  Wakati huo huo, kama sikosei kuna Mamlaka ambayo nadhani imebarikiwa na mkuu huyo ambayo imetoa agizo kiserikali kwamba mabasi yote ya wananfunzi yapakwe rangi ya njano.
  Kwa mantiki hii, hata hao kina CRDB na wenzao wanatakiwa wapake rangi hiyo lakini wana weza kuweka na kubadili matangazo yao kwa jinsi watakavyo ili mradi gari lionekane lina rangi ya njano kwa asilimia kubwa zaidi ili kurahisisha kutofautisha mabasi ya wanafunzi mara moja na kutohatarisha usalama wao mabasi yawapo barabarani.
  Zipo sheria katika nchi nyingine ambazo zinalinda na kupendelea mabasi yenye rangi hiyo na hili limechangia sio haba usalama wa wanafunzi katika nchi kama hizo.
  Jambo lingine lililonishtusha ni lile la maelezo eti wanafunzi Dar ni laki tano na wanahitaji mabasi 10,000 ? Je, hii ni sahihi? Vigezo gani vimetumika kufikia hesabu hiyo. Ninaamini hiyo ni sawa na nusu ya daladala zilizopo jijini kama sikosei.
  Mipangilio na mahitaji ya mabasi Dar
  Kwa kiasi kikubwa shida ya usafiri Dar es salaam inaweza kupungua sana kama patakuwa na ratiba maalum ya mabasi kwenda na kurudi toka kati ya jiji na pembezoni mwa jiji.
  Kwanza, mabasi yote yenye namba witri yawe yanaanzia upande mmoja na mabasi yote yenye namba shufwa yaanzie upande mwingine.
  Pawe na aina mbili ya vituo. Aina ya kwanza, vituo ambavyo mabasi hayaruhisiwi kukaa bali kuacha na kubeba abiria papo kwa hapo. Aina ya pili iwe ni vituo ambavyo basi linaruhusiwa kukaa kwa dakika tano tu. Kukaa zaidi kutawezekana tu pale basi linapoanzia na sio vinginevyo. Utaratibu huu ambao unafuata mantiki ya nadharia ya mfuatano barabarani (queueing theory) pamoja na mikakati mingine ya logistiki na usafiri.
  Wanafunzi na muda wa masomo
  Haileti maana wala mantiki shule zetu kuonekana eti zinasomesha toka saa moja mpaka saa kumi na moja wakati matokeo ni mabovu kiasi hicho.
  Ninapendekeza kwamba tuwe na shule zinazoanza saa 1 na kumaliza saa saba; saa 1:30 hadi saa saba na nusu; saa 2:00 hadi saa 8 na saa saa 2:30 hadi saa nane na nusu.
  Maofisi yote yaanze kazi saa 3 kamili. Kwa namna hii mabasi ya wanafunzi yanaweza kuwa na tripu nne za kwenda na kurudi bila kukutana na foleni au misongamano ya kutisha.
  Kama hili litafanyika ni dhahiri basi mabasi yatakayohitajika kwa ajili ya usafiri wa wanafunzi yatakuwa kama mabasi 2,500 tu badala ya hayo 10,000 yaliyofikiriwa bila mchakato unaoeleweka.
  Hii inanitia wasiwasi kwamba serikali yetu ni ile ambayo mkono wa kulia haujui mkono wa kushoto unafanya nini?
  Ninaamini kwamba upo uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya viongozi wetu huwa hawana habari na asilimia sabini au zaidi ya maamuzi yanayofanywa ngazi za chini. Ingelikuwa hivyo, kuna kauli ambazo zinatolewa bila mpango hivi leo zisingelikuwepo.
   
 2. J

  JO KIBAHA Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAMA CHA MADEREVA NA MAKONDA DAR MLANDIZI kilisha fanya utafiti wake mabasi 300 yanatosha kabisa na mchanganyuo wote wanao na ndo maana wameiba mawazo yao na kuyaweka hadhalani si umeona hawajui kitu chochote hapo! wilaya zote za Mkoa wa dar ni mabasi 35 tu kila wilayaya na Mkoa jirani wa PWANI ni mabasi 25 tu kwa maana wilaya 4 tu zizungukayo mkoa wa Dar yaani Kibaha, Kisarawe, Bagamoyo, na Mkulanga.

  watendaji wa JK ni wababaishaji tu!

  hebu DCA wafanye hiyo azi kwa ushindani na UDA.

  Pili hata sisi tumeshangaa yaani kila mtu aweke rangi yake Mh! sasa si itakuwa UCHAFU tu ni nini maana ya school bus uniforms????? mi naona ibakie ile ile ya rangi ya NJANO kama wenzetu wa nje USA school buss zote ni NJANO na zinapendeza pia, matangazo yatakaa kama kawaida si vinginevyo.

  ila haya tuyaongeayo je wanayasoma????
   
Loading...