Chumchang Changchum
JF-Expert Member
- Nov 1, 2013
- 5,935
- 6,157
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Dar es Salaam. Kama ulidhani ‘mtiti’ wa watu aliotinga nao aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba makao makuu ya chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam ungemsaidia kurejesha nafasi yake hiyo, basi umekosea.
Profesa Lipumba aliyetengua uamuzi wake wa kung’atuka kwenye wadhifa huo na kuomba kurejea madarakani, amekumbana na kizuizi cha viongozi wa juu wa chama hicho ambao wamepinga hatua hiyo wakisema katiba haimruhusu na nakwenda kukiua chama.
Awali, msomi huyo alitangaza nia ya kurejea uongozini jana kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, huku akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kuombwa.
Chanzo: Mwananchi