Viongozi wa Jeshi la Polisi waache viti waende mabarabarani kusimamia Trafiki wazembe

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Kati ya mambo yanayoudhi wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni kero ya foleni ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na udhaifu wa kikosi cha usalama barabarani kushindwa kusimamia sheria zilizowekwa ambazo kama zingefuatwa ukubwa wa tatizo la foleni usingekuwa kwa kiasi hiki.

Trafiki wa mkoa wa Dar es S alaam wamekuwa watu wakulaumiwa kila kukicha kutokana na ukweli kuwa sio watu ambao wanania ya dhati kusimamia sheria za barabarani kwani wamekuwa wakifanya kazi yao hiyo kwa mazoea na kwa ulegelege mkubwa huku wakifumbia macho makosa ya wazi ambayo hata mtu wa kawaida angeweza kuchukuwa hatua. Mathalani jana nilipita barabara ya Mandela kwenye mauingio ya barabara iendayo segerea nilikuta magari yamefungamana kila mmmoja akitaka kupita, kitu ambacho kilinisikitisha nikuona kuwa Askari wa Trafiki alikuwa pale lakini alishindwa kabisa kuwachukulia hatua madererva ambao kwa makusudi baada ya kuona foleni waliingia barabara nyingine ambapo kisheria hilo ni kosa la jinai, hata hivyo Trafiki aliendelea kusimama na kuonyesha kabisa kushindwa kuchukuwa hatua huku akionyesha kabisa kufahamiana na madereva wa daladala ambao wengi ndiyo walikuwa wamehama barabara.

Eneo la Tazara kwa sasa nafikiri ndiyo linaloongoza kwa foleni, unapoita asubuhi utakuta askari zaidi ya kumi wamesimama eneo moja kama vile wanataka kuimba kwaya, wakati huo huo kuna maeneo hatua chache yanahitaji msaada wa askari ili kuzuia madereva wanaovunja sheria. Nafikiri wana JF mna ushuhuda mwingi wa mpango mbaya wa kazi wa trafiki ambao hauna nia ya dhati ya kutokomeza foleni, sina uhakika kama viongozi wajuu wa jeshi la Polisi wanamuda wa kusimamia hawa askari wazembe. Mara kadhaa nimekuwa nikipiga simu trafiki makao makuu ndiyo baada ya muda unaona askari aliyekuwa anamejibanza pembeni kwenye mti akitimua mbio kuja kusaidia kunasua magari yaliyosongamana sasa huu si mzaha kwenye kazi? Inamaana askari hawezi kutimiza wajibu wake mpaka tuombe msaada makao makuu? Rais wetu ameshaagiza watendaji waache viti na chai waende kuona kero za wananchi, Polisi wasijitenge na kauli ya Rais watoke waje mabarabarani waone wananchi wanavyoteseka bila sababu za msingi. Askari tunao wengi sana ila mpango wao wa kazi ni mbaya ndiyo maana hawana uwezo wa kukabiliana na tatizo la foleni ambalo halihitaji mzungu kutoka ulaya bali ni swala la kutumia akili tu!!
 
mkuu tupe na sisi hizo namba maana hii ni kero

Ukiona tatizo piga hii ya Trafiki Makao makuu wako fasta 0732928723 kuna nyingine ninayotumia nikikwama kabisa ila ni binafsi ngoja nisiitoe hapa. ila kila mara nilipotumia hiyo hapo juu nilipata msaada
 
Back
Top Bottom