Viongozi wa Ecowas kuudhuria kuapishwa kwa rais Gambia.

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,636
6,261
Viongozi Africa magharibi wameazimia matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Adama barrow yaheshimiwe na watahudhuria kuapishwa kwake January 19.
Uamuzi huo umeafikiwa katika mkutano wao wa jumuia ya ushirikiano kiuchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS) uliomalizika mwishoni mwa wiki mjini Abuja Nigeria, na kusisitiza kuwa wote watakwenda Banjul, Gambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Barrow.
Pia marais wote 11 wamekubaliana kuchukua hatua zozote za lazima kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa, huku wakimtolea wito rais wa sasa yahaya jammeh ambae hakuhudhuria sherehe hizo kutokuzuia ukabidhiaji wa madaraka kwa amani, mkutano huo pia ulihudhuriwa na rais john dramani wa Ghana aliyekubali kushindwa kwenye uchaguzi uliofanyika siku chache baada ya ule wa Gambia, pia ndiye aliyechaguliwa kuwa msuluhisho katika mgogoro huo pamoja na rais wa Nigeria.
 
Afrika Magharibi wanajitahidi sana.Hata wakisema wanajitoa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita unaweza ukawaelewa.
Wameunda mpaka Jeshi lao linaloitwa ECOMOG.Kauli hii inaonyesha wapo tayari kumtoa kwa nguvu za kijeshi.
 
Bwana yahaya jammeh alishasema familia imemshaur na kumwambia alichakachuliwa katika kura....kwel kwel hapa tz mkulu 2020 ashindwe useme amechakachuliwa wakat Lubuva wake, jecha yupo ktk kamat yake nan wa kufanya haipo hyo.
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
kwa kweli kuna nchi za kiafrika nimezikuballi sana kuhusu swala la kubadilishana uongozi kidemokrasia mfano zambia, malawi, ghana, nigeria na senegal. huko demokrasia ipo bwana.
 
Tatizo Jammeh hakujipanga mapema labda hakusoma alama za nyakati. Wazoefu wanadhibiti mapema kabisa tume ya uchaguzi, jeshi, na wasimamizi wa uchaguzi kuhalikisha mambo yanaenda sawa.
 
Nimefurahi kwamba John Dramani ameteuliwa kuwa msuluhishi. Hiyo huwa tukaweka "mchawi mpe mwana alee" naamini atamshauri vizuri.
 
Yahya Jammeh Nimemshangaa Sana, alishindwa kuwaomba ushauri ccm?
Angekuja Dar kujipendekeza aisee, ma ccm yangemwonyesha jinsi ya kuji lubuva na kuji jecha.
 
angalau hao wa afrika magharibi wameuweka mbali unyani wa kiafrika sasa wametambua kua wao ni binadamu na si wanyama.maana binadamu hufanya maamuzi ki binadaam.
 
Wa Afrika Mashariki ni club inayolea madikteta.
Ukiondoa Kenya walobaki hataki kuondoka.
Tanzania imeonekana huko Zanzibar . Kuna kagame museveni na wa burundi. Wote vinganganizi.
Na club hii ikawaingiza sudan kusini taifa lisilojua hako za raia wake.
Tupo tofauti sana na nchi ingine..EA ni matatizo
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom