pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,636
- 6,261
Viongozi Africa magharibi wameazimia matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Adama barrow yaheshimiwe na watahudhuria kuapishwa kwake January 19.
Uamuzi huo umeafikiwa katika mkutano wao wa jumuia ya ushirikiano kiuchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS) uliomalizika mwishoni mwa wiki mjini Abuja Nigeria, na kusisitiza kuwa wote watakwenda Banjul, Gambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Barrow.
Pia marais wote 11 wamekubaliana kuchukua hatua zozote za lazima kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa, huku wakimtolea wito rais wa sasa yahaya jammeh ambae hakuhudhuria sherehe hizo kutokuzuia ukabidhiaji wa madaraka kwa amani, mkutano huo pia ulihudhuriwa na rais john dramani wa Ghana aliyekubali kushindwa kwenye uchaguzi uliofanyika siku chache baada ya ule wa Gambia, pia ndiye aliyechaguliwa kuwa msuluhisho katika mgogoro huo pamoja na rais wa Nigeria.