singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
HUKO nyuma, mwaka 2005, wakati Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akigombea kwa mara ya kwanza, tuliwahi kuambiwa na viongozi wa dini kuwa alikuwa ni chaguo la Mungu.
Kilichomaanishwa sio tu kuwa kila kiongozi anayechaguliwa huwa ni kwa ridhaa ya Mungu, bali ni kwamba Mungu kamteua Kikwete maalumu aje kuiongoza Tanzania akijua ataifaa nchi yetu.
Sisi wafuasi tukijua kuwa waliotoa kauli hizo ni viongozi wa dini tuliamini kuwa wamepokea maono kutoka kwa Mungu. Kikwete akachaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi ule. Kisha taratibu ukweli ukadhihiri.
Kikwete alikuwa ni kiongozi wa kawaida tu aliyejaaliwa vipawa fulani, aliyeweza kufanikisha mambo kadhaa kwa ajili ya nchi yake lakini pia alishindwa kwa kiasi kikubwa kujibu changamoto za maendeleo za nchi na wananchi, hususan wananchi masikini wa kawaida. Na hata alizalisha changamoto nyingine nyingi.
Katika kipindi cha uongozi wa Kikwete rushwa na ufisadi viliongezeka, biashara ya dawa za kulevya ilikomaa hadi Watanzania tukaogopwa huko nje na umasikini ukaongezeka maradufu. Wakati huo huo tukiambiwa uchumi mkuu lakini uliofaidisha wachache ukikua.
Kwa maana ile waliyokusudia, maana ambayo ilipandisha matumaini ya Watanzania wengi, Kikwete hakuwa chaguo la Mwenyezi Mungu na ndio maana kauli hizi zilikoma na lawama zikaanza kuibuka Kikwete akiambiwa hafai, na hadi watu wakatabiri CCM kufa chini ya uongozi wake.
Viongozi wa dini hawajakoma. Mwaka huu baadhi yao waliendelea kutoa matamshi yanayoashiria walipata maono ya kimungu katika mambo ya siasa na wamekosea tena katika utabiri wao. Tena viongozi hao walitoa kauli hizo wakizinasibisha na utumishi kwa Mungu.
Baadhi yao sasa wanakana kauli walizozitoa hadharani kweupe, tena zikirushwa katika katika vipindi vya moja kwa moja vya runinga, redio na kuhifadhiwa kwenye akaunti za mitandao ya kijamii, kama ‘YouTube’ wakiunga mkono wagombea waliowapenda na ambao waliamini wangeshinda.
Kwa mfano, Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufua na Uzima, ambaye ana wafuasi wengi nchi nzima, alitangaza wiki iliyopita kuwa hakuwahi kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, bali alikuwa akiunga mkono harakati za mabadiliko.
Kwa mujibu wa Gwajima yeye aliitwa tu kuomba katika mkutano wa Lowassa Arusha (bila shaka Lowassa akiwa CCM), na ule wa Jangwani ambao ulifanyika wakati Lowassa akiwa mgombea wa Chadema – Ukawa. Pia alisema alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya Dk. Willibrod Slaa kuzungumza na kumtaja!
Lakini tulichokiona wakati wa kampeni ni tofauti na maelezo yake. Gwajima alichagua mabadiliko lakini yaliyohubiriwa na Ukawa na Lowassa sio mengine yaliyohubiriwa na CCM au ACT. Ukisikiliza ‘maombi’ yake aliyoyafanya katika mikutano aliyoitaka hilo lilikuwa wazi.
Katika maombi yake ya Jangwani Gwajima akiongoza maelfu ya wafuasi wa Chadema na muungano wa vyama vya Ukawa alisema: “Kila jambo na majira yake na kila kusudi chini ya mbingu. Watu..majira hayafuati watu bali watu wanafuata majira. Ukifika wakati wa baridi watu wote wanavaa makoti, sio wanavaa makoti ili iwe baridi.
Sasa majira haya ni ya Edward Lowassa pamoja na Duni Haji na hakuna atakayewazuia……Kwa jina la Yesu, ninalazimisha kila roho ya mwanadamu atii nyakati hizi.”
Bwana umfanye Lowassa na Duni Haji kuwa wakina Joshua wetu watakaotuvusha kwenye mto Jordan watupeleke kwenye nchi ya ahadi katika jina la Yesu. Mungu kama vile ulivyowaangamiza watu wote walioshindana na watu wako ndivyo uwaangamize watu wote watakaonyoosha mkono juu ya Edward Lowassa na juu ya Duni Haji katika jina la Yesu.”
Ninaomba uwabariki wenyeviti wote wa Ukawa; na Tanzania uihamishe kutoka mikononi mwao (yaani CCM uiingize katika mikono ya Ukawa na haya yote niliyoyasema yameshakuwa kwa jina la Yesu; na watu waseme imeshakuwaaaa…(watu wakaitia ‘imeshakuaa’).”
Katika maombi yake yote hayo, hakuna neno mabadiliko, bali amemtaja Lowassa na Duni Haji mara kadhaa. Licha ya sala hiyo, bahati mbaya matamanio ya Gwajima hayakuwa. CCM walishinda labda hata kuliko ilivyotegemewa!
Aliyeshindwa hapa sio Mungu, bali ni Gwajima aliyetaka kumsemea Mungu katika mambo ambayo hakupewa maono bali ni matamanio yake tu! Wapo wanaosema CCM waliiba, lakini sala ile ilikusudia kuzuia hata hao wezi wasiweze kuiba kura!
Gwajima pia alitajwa kuwa ndiye mshenga wa ndoa ya Edward Lowassa na Chadema. Ilikuwaje akashiriki kufanya ushenga huo wa kisiasa katika jambo ambalo hana maslahi nalo? Katika mkutano ambao aliutumia kujibu madai ya Lowassa, Gwajima alielezea vizuri kazi kubwa aliyoifanya katika kuwezesha Lowassa kuhamia na kuwa mgombea wa Ukawa.
Ukizingatia kwamba Gwajima alikuwa ‘akimfanyia maombi’ Lowassa tangu akiwa CCM, ni wazi kuwa Gwajima sio tu kwamba aliunga mkono mabadiliko bali aliamini Lowassa ndiye anayeweza kufanya kazi hiyo ya kuleta hayo mabadiliko.
Mbali na Gwajima, wamekuwapo pia viongozi wengine wa kidini, Wakristo na Waislamu, waliowahi kutoa utabiri katika mambo ya siasa wakidai wamepewa ufunuo na Mungu. Yupo kiongozi mwingine aliyedai pia kapewa ujumbe Lowassa atakuwa rais na kama hiyo isipokuwa apigwe mawe hadi afe kwani hiyo ndio adhabu ya mwongo.
Wito wangu kwa viongozi wa dini ni kuwa wawe waangalifu na matamshi yao kwa sababu yanapunguza sio tu imani ya waumini wao kwao lakini hata imani ya watu kwa ujumla kwa viongozi wa dini.
Kwa mujibu wa vitabu vyote vya dini Mwenyezi Mungu hakosei, ni mjuzi wa kila kitu, anajua yaliyopita ya sasa na yajayo, anajua yaliyo dhahiri na yaliyojificha na pia Mwenyezi Mungu anajua hata ambayo sisi binadamu tumeyahifadhi vifuani mwetu.
Basi ni vema tusimsemee Mwenyezi Mungu katika mambo maalumu (specific) kama hatujapewa ujumbe huo, bali tuendelee kuhubiri kwa mujibu wa ujumbe wake uliomo katika vitabu vyake vitukufu.
Kadhalika, si vema kwa kiongozi wa dini kuanza kukanusha mambo aliyoyatamka hadharani ili tu kulazimisha fikra kwamba yeye hakukosea bali watu walimwelewa vibaya. Gwajima ameharibu heshima yake mbele ya Watanzania kwa kauli aliyoitoa.
Kila mtu anajua kuwa yeye, Gwajima aliunga mkono Lowassa akiamini ndiye mleta mabadiliko na ndiyo maana alianza kumuunga mkono akiwa CCM na baadaye akahama naye kwenda Chadema (Ukawa). Kama ilivyokuwa kwa wafuasi wengine wa Ukawa, kwa Gwajima, Lowassa ndio mabadiliko na mabadiliko ndio Lowassa.
Kutokana na uzoefu wa chaguzi zilizopita, ushauri wangu kwa viongozi wa dini ni kuwa wakae mbali na siasa za kugawa waumini wao kwa kushabikia vyama au wagombea; na badala yake wahubiri amani, utulivu, demokrasia, haki, usawa, ukweli, uaminifu, uadilifu na kadhalika.
Raia Mwema