tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Ukipitia mitandao mingi ya kijamii mara baada ya kikao cha Rais na Viongozi wa Dini kumekuwa na lawama nyingi sana na kuwakosoa Viongozi wa Dini kuhusu hoja walizozitoa kwa Rais kuhusu masuala mazima ya ustawi wa watanzania na changamoto wanazopitia taasisi za dini na serikali ya Tanzania.
Viongozi wengi wa dini walitoa namna ambavyo wanatoa michango yao kustawisha jamii ya kitanzania kiroho na kimwili na changamoto wanazokumbana nazo namna ambavyo mahali pengine wanakwama kabisa na Rais amejaribu kuzipitia na baadhi kuzitolea ufafanuzi na zingine kuzichukua na kuahidi kuzifanyia kazi yeye na watendaji wake kwa kadri inavyofaa ili changamoto nyingi ziweze kutatuliwa kwa wakati.
baadhi ya michango mingi huku katika mitandao ni kama vile viongozi wa dini hawajauliza au kutoa hoja ambazo walitegemewa kuzitoa kwa maoni ya wanasiasa lakini ukiangalia mambo ya dini hayaingiliani na mambo ya kisiasa ingawaje yupo aliyejaribu kuuliza kuhusu demokrasia na Rais alilifafanua vizuri tu
Mambo mengi yameulizwa kuhusu afya,elimu,maji,maadili,mahusiano kati ya serikali na taasisi za dini,kodi,sheria,vyombo vya dola,watendaji wa serikali,masomo ya wanadini nje ya nchi,unyanyasaji wa wanadili pale uwanja wa ndege,mambo ya mirathi na ndoa kwa dini ya kiislamu kutambulika kisheria na mengine mengi tu kadha wa kadha.
Kwa mtazamo wangu viongozi wa dini hawawezi kuuliza mambo ya kisiasa kama ambavyo viongozi wa kisiasa wanataka na walitaka hivyo ikifika zao yao viongozi wa kiasiasa kuongea na Rais basi wauulize mambo yao ya kisaisa kwasababu kuna uwezekano mkutano wao na Rais kwa viongozi wa kisiasa unakuja kwa jinsi itakavyo mpendeza Rais.
Tuwaheshimu viongozi wetu wa dini kwa kuonyesha moyo wa unyenyekevu mbele ya Rais maana wanajua kuwa mamlaka zote hutoka kwa Mungu ukifika muda wa wanasiasa kuongea na Rais basi waulize hayo mambo yao ya kisiasa na si kuwatukana na kuwabeza viongozi wa dini.
Hata wadau wa madini hawakuuliza mambo ya kisiasa katika mkutano wao na Rais siku walipofanya mkutano naye.