Viongozi wa dini wasemavyo kuhusu Madaktari: Yupi mkweli na kwanini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wasemavyo kuhusu Madaktari: Yupi mkweli na kwanini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msengapavi, Jul 3, 2012.

 1. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo alisema madaktari hao wanatakiwa kurudi kazini kwa kuwa tayari Serikali imeshasema kuwa haina fedha za kuwalipa na kuongeza kuwa hata kama wana madai yao, wadai wakiwa kazini.

  "Asilimia kubwa ya madaktari wamesomeshwa na Serikali… Serikali hiyohiyo inawaeleza kuwa haina fedha za kuwalipa kama wanavyotaka, binafsi nawaomba tu warudi kazini kwa kuwa mgomo wao unawaathiri zaidi wananchi kuliko hata hao viongozi wa Serikali.

  "Tunajua tulikotoka ila hatujui tunakokwenda, kama ni kuboreshwa kwa sekta nzima ya afya, Serikali imesema itatekeleza hilo, haiwezi kuyatekeleza kwa siku moja, haya mambo yanajadilika.

  Alisema kama Serikali itakuwa na makosa yake, itayajibu mbele za Mungu... "Madaktari watekeleze wajibu wa kazi yao kwa uwezo wa Serikali iliyopo madarakani."

  Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kagera, Dk Methodius Kilaini alisema kanisa hilo haliwezi kuunga mkono mgomo huo.

  Alisema pamoja na kuwa madaktari wana madai yao, jukumu lao kubwa ni kufuata maadili ya kazi yao ambayo hayawaruhusu kugoma.

  Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Askofu David Mwasota alisema madaktari wanatakiwa kutenganisha siasa na maadili ya kazi yao.

  "Hata kama Serikali ina makosa yake lakini, wao kuendelea kugoma si jambo zuri kwa jamii na hata mbele za Mungu, watumie njia nyingine kudai madai yao, lakini waendelee kutoa huduma. Madaktari ni watu muhimu, kurudisha viungo vya binadamu katika hali ya kawaida si kazi ndogo, warudi kazini kuokoa mamia ya Watanzania maskini."

  Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Arusha Abdulkarim Jonjo alisema ipo haja kwa Serikali kukaa meza moja na madaktari hao.

  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mjini Kati, Thomas Laizer alisema mgogoro wa madaktari umalizwe kwa mazungumzo.

  Alisema Serikali inapaswa kuwa wazi inapozungumza na madaktari kwa kueleza ni mambo gani yanawezekana na kwa muda gani ili, kuondoa migogoro.

  Akizungumza juzi katika ibada maalumu katika kanisa la KKKT Kimandolu, alisema ili kuondoa hisia kuwa Serikali inahusika na tukio la kutekwa Dk Ulimboka ni lazima iundwe tume huru.

  "Nadhani ili kuondoa haya maneno ambayo si jambo dogo, Serikali inapaswa kuunda tume huru kuchunguza tukio hili, kwani inawezekana waliohusika ni watu wengine tu wenye nia mbaya na Serikali lakini ili ukweli ujulikane ni muhimu kuwepo tume huru," alisema Askofu Laizer.

  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum aliwataka madaktari kutii agizo lililotolewa na Mahakama kwa kurudi kazini.

  "Rais ameshaeleza wazi kwamba Serikali haina fedha za kuwalipa kama wanavyotaka, warudi tu kazini na kuweka masilahi ya Watanzania mbele na kuacha kutanguliza masilahi binafsi," alisema Sheikh Salum.


  Source: Mwananchi
   
 2. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Mimi sio Daktari ila nimefanya kazi na watumishi wa afya kwa miaka minne. Nimekuwa na bahati ya kutembelea mikoa na wilaya kadhaa katika mikoa minne ya Tanzania. Ukweli unaosemwa na viogozi wa serikali kwa mara zote ni tofauti na hali halisi. Kinachosemwa na viongozi wa serikali yetu kinatiwa chumvi kupindukia. Utasikia huduma za afya kwa mama na mtoto ni bure, huduma za wazee ni bure, bajeti ya afya imepanda tangu awamu hii iingie madarakani. Tumetengeneza barabara nyingi za lami sawa na ardhi yote ya Nchi ya Burundi, nk. Wakati hayo yanasemwa hayalinganishwi na kukua kwa deni la taifa, nyongeza ya vyanzo vya mapato na wala ufisadi umechukua kiasi gani!!!!

  Serikali ingekuwa na jeuri ya kusema kama ingekuwa inasema ukweli unaothibitika. Hali kama hii inatupa shida kuunga mkono mgomo wa madaktari au kupinga.
   
Loading...